Mwanzo › Biblia inasema nini › Kuteswa kwa ajili ya imani
Nyakati ngumu
Biblia inasema nini kuhusu Kuteswa kwa ajili ya imani
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Mt 5:10
Heri wale wanaoteswa kwa ajili ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao.2 Tim 3:12
Wote wanaotaka kuishi katika maisha ya kumcha Mungu katika Kristo Yesu watateswa.Yn 15:18
Kama ulimwengu utawachukia, mjuwe kwamba ulinichukia mimi kabla haujawachukia ninyi.Mt 5:44
Lakini nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanao waudhi,2 Kor 12:10
Kwa hiyo ninatosheka kwa ajili ya Kristo, katika udhaifu, katika matukano, katika shida, katika mateso, katika hali ya masikitiko. Kwa kuwa wakati nikiwa dhaifu, kisha nina nguvu.Lk 6:22
Mmebarikiwa ninyi ambao watu watakapowachukia na kuwatenga na kuwashutumu ninyi kwamba ni waovu, kwa ajili ya Mwana Adamu.1 Pet 4:12–14
Wapendwa, msihesabu jaribu ambalo huja kuwajaribu kama kitu kigeni, ingawa kuna kitu kigeni kilichokuwa kinatukia kwenu. Lakini kwa kadri mnavyozidi kupata uzoefu wa mateso ya Kristo, furahini, ili kwamba mfurahi pia na kushangilia katika ufunuo wa utukufu wake. Iwapo mmetukanwa kwa ajili ya jina la Kristo, mmebarikiwa, kwa sababu ya Roho wa utukufu na Roho wa Mungu anakaa juu yenu.Mt 10:22
Nanyi mtachukiwa na kila mtu kwa sababu ya jina langu. Lakini yeyote atakayevumilia mpaka mwisho mtu huyo ataokolewa.1 Pet 3:17
Ni vizuri zaidi, ikiwa Mungu anatamani, kwamba mwateseka kwa kufanya mema kuliko kwa kufanya mabaya.1 Pet 3:14
Lakini kama mkiteseka kwa haki, mmebarikiwa. Msiogope yale ambayo wao wanayaogopa. Msiwe na wasiwasi.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0