Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Yakobo 1:19

Mstari wa Biblia · ULB

Yakobo 1:19

Mnajua hili, ndugu zangu wapendwa. Kila mmoja anapaswa kuwa mwepesi wa kusikia, siyo mwepesi wa kuongea wala kukasirika,

Soma sura nzima: Yakobo 1

Katika muktadha

16Ndugu zangu wapendwa, msidanganyike.

17Kila zawadi iliyo nzuri na kila zawadi iliyokamilika hutoka juu, hushuka chini kutoka kwa Baba wa nuru. Kamwe habadiliki kama kivuli kibadilikavyo.

18Mungu alichagua kutupa sisi uzima kwa Neno la kweli, ili kwamba tuweze kuwa kama uzao wa kwanza miongoni mwa viumbe vyake.

19Mnajua hili, ndugu zangu wapendwa. Kila mmoja anapaswa kuwa mwepesi wa kusikia, siyo mwepesi wa kuongea wala kukasirika,

20kwa kuwa hasira ya mwanadamu haiwezi kutenda haki ya Mungu.

21Kwa hiyo wekeni mbali uchafu wa dhambi na ubaya wote ulio mahali popote, na kwa unyenyekevu lipokeeni neno lililopandwa ndani yenu, ambalo lina uwezo wa kuokoa roho zenu.

22Litiini neno, msilisikie tu, mkijidanganya nafsi zenu wenyewe.

Yakobo 1

Kwa Kiingereza

Berean Standard BibleJames 1:19My beloved brothers, understand this: Everyone should be quick to listen, slow to speak, and slow to anger,

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Mit 17:27Mwenye maarifa hutumia maneno machache na mwenye ufahamu ni mtulivu.
Mit 21:23Anayelinda kinywa chake na ulimi wake hujilinda mwenyewe na taabu.
Mit 14:29Mtu mvumilivu anaufahamu mkubwa, bali mtu mwepesi wa kuhamaki hukuza upuuzi.
Mit 10:19Katika maneno mengi, hapakosi uhalifu, bali aliyemwangalifu katika usemi wake ni mwenye busara.
Mit 18:13Anayejibu kabla ya kusikiliza- ni upuuzi na aibu yake.
Efe 4:26Mwe na hasira, lakini msitende dhambi.” Jua lisizame mkiwa katika hasira zenu.
Mit 13:3Yeye anayelinda kinywa chake huyalinda maisha, bali anayefumbua sana midomo yake atajiangamiza mwenyewe.
Mit 16:32Ni bora kukawia kuwa na hasira kuliko kuwa shujaa na mwenye kutawala roho yake ni imara zaidi kuliko yule anayeuteka mji.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki