Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 13 Aprili
Kalenda ya Kiorthodoksi · 31 Machi (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 13 Aprili 2027
Jumanne · Wiki ya 5 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 4
Sikukuu na watakatifu
Mfiadini wa Kikasisi Hipatio, Askofu wa Gangra (karibu 326)
Kwaresima Kuu
Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Saa ya 6
18Ni nanibasi utayemlingalisha na Mungu? Ni kwa sanamu ipi utakayomfananisha nayo? 19Sanamu! ambayo fundi ameitupa: Mfua dhahabu ameka pamoja na mikufu bandi ya fedha. 20Kuafanya sadaka hii mtu atachagua kuni ambayo haiozi; anamtafuta fundi mwenye ujuzi wa kutengeneza sanamu ambayo haitaanguka. 21Je hamkujua? Je hamjasikia? Je hamkuambiwa tokea mwanzo? Je hamkuelewa toka misingi ya nchi? 22Yeye ndiye aketie juu ya upeo wa macho ya nchi? na wenyeji wake ni kama panzi mbele yake. Akijinyoosha nje ya mbingu ni kama pazia na kutawnya nje kama hema la kuishi. 23Anawapunguza viongozi kuwa si kitu na amewafanya viongozi wa nchi kwa sio wenye umuhimu. 24Tazama wamekuwa wagumu kuotesha; tazama wamekuwa wagumu kupanda; imekuwa ni vigumu kuchukua mzizi katika nchi, kabla ajapuliza juu yao, na wakanyauka, na upepo unawaondosha mbali kama majani. 25Ni nani tena utakayemfananisha na mimi, ni nani ninayefanan nae?'' amesema mtakatifu. 26Tazama juu kwenye anga! Nani aliyeziumba nyota hizi zote? Analileta nje jeshi na anawaita kwa majina yote. Kwa ukuu wa nguvu zake na kwa uimara wa nguvu zake, hakuna hata mmoja atakayekosa. 27Kwa nini unasema, Yakobo, na kutangaza, Israeli, ''Njia yangu imefichwa Yahwe asione, na Mungu wangu hakuwekwa wazi kuhusiana na uthibitisho wangu''? 28Je hakufahamu? Mungu wa milele, Yahwe, Muumbaji wa miisho ya nchi, apatwi na uchovu wala hachoki; hakuna mipaka katika ufahamu wake. 29Anawapa nguvu waliochoka; na atawapa nguvu mpya waliowadhaifu. 30Hata vijana wadogo watapatwa na uchovu na kuchoka, vijana wadogo watapata mashaka na kuanguka: 31Lakini wale watakao mngojea Yahwe watapewa nguvu mpya; na watapaa kwa mbawa kama malaika; watakimbia wala hawatachoka; watatembea wala hawatazimia.
Sala ya Jioni: somo
1Baada ya mabo haya neno la Yahwe likamjia Abram katika maono, likisema, “Usiogope, Abram! mimi ni ngao yako na thawabu yako kubwa sana.” 2Abram akasema, “Bwana Yahwe, utanipatia nini, kwa kuwa naenda bila mtoto, na mrithi wa nyumba yangu ni Eliezeri wa Dameski?” 3Abram akasema, “Kwakuwa hujanipatia uzao, tazama, mwangalizi wa nyumba yangu ndiye mrithi wangu.” 4Kisha, tazama, neno la Yahwe likaja kwake, kusema, “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako; isipokuwa atakaye toka katika mwili wako ndiye atakuwa mrithi wako.” 5Kisha akamtoa nje, na akasema, Tazama mbinguni, na uzihesabu nyota, ikiwa unaweza kuzihesabu.” Kisha akamwambia, hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa. 6Akamwamini Yahwe, na akamuhesabia jambo hili kuwa mwenye haki. 7Akamwambia, Mimi ni Yahwe, niliye kutoa katika Uru ya Wakaldayo, na kukupatia nchi hii kuirithi.” 8Akasema, “Bwana Yahwe, nitajua je kuwa nitairithi?” 9Kisha akamwambia, “Nipatie ndama wa umri wa miaka mitatu, mbuzi mke wa umri wa miaka mitatu, na kondoo mume wa umri wa miaka mitatu, na njiwa na mwana njiwa.” 10Akamletea hivi vyote, akavipasua katika sehemu mbili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuawapasua. 11Wakati ndege walipokuja juu ya mizoga, Abram akawafukuza. 12Kisha wakati jua lilipokuwa likizama, Abram akalala usingizi mzito na tazama, hofu ya giza kuu ikamfunika. 13Kisha Yahwe akamwambia Abram, “Ujuwe kwa hakika kwamba uzao wako watakuwa wageni katika nchi ambayo si ya kwao, na watatumikishwa na kuteswa kwa miaka mia nne. 14Nitahukumu taifa ambalo watalitumikia, na baadye watatoka wakiwa na mali nyingi. 15Lakini utakwenda kwa baba zako kwa amani, na utazikwa katika uzee mwema.
Sala ya Jioni: somo
7Midomo ya wenye hekima husambaza maarifa, bali mioyo ya wapumbavu haifanyi hivyo. 8Yehova anachukia sadaka za watu waovu, bali maombi ya watu waadilifu ndiyo furaha yake. 9Yehova anachukia njia ya watu waovu, bali anampenda yule ambaye huandama haki. 10Marudi ya ukatili hungojea kwa yeyote ambaye huiacha njia na yule ambaye huchukia masahihisho atakufa. 11Kuzimu na uharibifu vipo wazi mbele za Yehova; je si zaidi sana mioyo ya wana wa wanadamu? 12Mwenye mzaha huchukia masahihisho; hatakwenda kwa wenye hekima. 13Moyo wenye furaha husababisha uchangamfu wa uso, bali huzuni huvunja moyo. 14Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa, bali kinywa cha wapumbavu hujilisha kwenye upuuzi. 15Siku zote za watu waliokandamizwa ni taabu, bali moyo wenye furaha unakaramu daima. 16Bora kitu kidogo pamoja na kumcha Mungu kuliko hazina kubwa pamoja na ghasia. 17Bora mlo wenye mboga kukiwa na upendo kuliko kuandaliwa ndama aliyenona kwa chuki. 18Mtu mwenye hasira huchochea mabishano, bali mtu ambaye hukawia kukasirika hutuliza ugomvi. 19Mapito ya mtu goigoi ni kama sehemu yenye uwa wa miiba, bali mapito ya mtu mwadilifu ni njia kuu iliyojengwa imara.
Watakatifu wa siku
- Askofu Mtakatifu Yona, Mitropoliti wa Moscow na Urusi yote, mtenda miujiza († 1461)
- Askofu Mtakatifu Inokenti, Mitropoliti wa Moscow (1879)
- Mfiadini wa Kikasisi Yohana, padri (1938)
- Mtakatifu Mtawa Apolonio, mkaa jangwani wa Misri (karne ya 4)
- Wafiadini wa Kikasisi Abda, Askofu wa Uajemi, na Benyamini, shemasi (418-424)
- Mtakatifu Mtawa Hipatio, abati wa Rufiniana (karibu 446)
- Mtakatifu Mtawa Hipatio, mponyaji, wa Mapango ya Kyiv (karne ya 14)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 31 Machi katika kalenda ya kanisa ni 13 Aprili katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki