Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 14 Aprili

Kalenda ya Kiorthodoksi · 1 Aprili (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 14 Aprili 2027

Jumatano · Wiki ya 5 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 4

Sikukuu na watakatifu

Mtakatifu Mtawa Maria wa Misri (522)

Kwaresima Kuu

Mfungo: pamoja na mafuta

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Saa ya 6

Isa 41:4–14

4Ni nani aliyeyafanya na kukamilisha matendo haya? Ni nanialiyechagua kizazi kutoka mwanzo? Mimi, Yahwe ni mwanzo na mwisho, mimi ndiye. 5Visiwa vimeona na kuogopa; miisho ya dunia yatetemeka; walikaribia n kuja. 6Kila mmoja amsaidie jirani yake, na kila mmoja asemezane na mwenzake, 'Kuwa mfariji; 7Hivyo basi seremala anamfariji mfua dhahabu, na yule anayefanya kazi kwa kutumia nyundo anamfariji anayefanya kazi kwa chuma, akisema kwa msemo wa kurehemu, ''Ni mizuri; Naye ataupigilia kwa makini misumari ili isipinduke. 8Lakini wewe, Israeli mtumishi wangu, Yakobo niliyekuchagua, mtoto wa Ibrahimu rafiki yangu, 9wewe ambaye ninakurudisha kutoka miisho ya nchi, na ambaye niliyekuita kutoka sehemu ya mbali, na kwako niliyekuambia, 'Wewe ni mtumishi wangu,; 'Nimekuchagua wewe na sijakukataa. 10Usiogope maana mimi niko pamoja na wewe. Usiwe na wasiwasi, maana mimi ni Mungu wako. Nitakutia nguvu, na nitakusaidia, wewe, na Nitakushika kwa mkono wa haki yangu. 11Tazama, watakuwa na aibu na hawataheshimiwa, wale wote waliokuwa na hasira na wewe; watakuwa si kitu na watatokomea, wale watakao kupinga wewe. 12Utawatafuta na wala hautawapata wale wanaopingana na wewe; wale wafanyao vita dhidi yako watakuwa kama si kitu, si kitu kabisa. 13Maana mimi Yahwe Mungu wako, nitawashika mkono wako wa kiume, nikikuambia wewe, 'Usiogope; Nitakusaidia wewe. 14Usiogope, Yakobo wewe mdudu, na enyi watu wa Israeli; Nitawasaidia''- hili ni tamko la Yahwe, Mkombozi wako, Mtakatifu wa Israeli.

Sala ya Jioni: somo

Mwa 17:1–9

1Wakati Abram alipokuwa na umri wa miaka tisini na tisa, Yahwe alimtokea Abram na akamwambia, “Mimi ni Mungu wa uwezo. Uende mbele yangu, na uwe mkamilifu. 2Kisha nitalithibitisha agano langu kati yangu mimi na wewe, na nitakuzidisha sana. 3Abram akainama uso wake hadi chini ardhini na Mungu akazungumza naye, akisema, 4“Mimi, tazama, agano langu liko nawe. Utakuwa baba wa mataifa mengi. 5Wala jina lako halitakuwa tena Abram, bali jina lako litakuwa Abraham - kwa kuwa ninakuchagua kuwa baba wa mataifa mengi. 6Nitakufanya uwe na uzao mwingi zaidi, na nitakufanya mataifa, na wafalme watatoka kwako. 7Nitaimarisha agao langu kati yangu mimi na wewe na uzao wako baada yako, katika vizazi vyao vyote kwa agano la milele, nitakuwa Mungu kwako na kwa wazao wako baada yako. 8Nitakupa wewe, na wazao wako baada yako, nchi ambayo ulikuwa unaishi, nchi yote ya Kanaani, kuwa miliki ya milele, na nitakuwa Mungu wao.” 9Kisha Mungu akamwambia Abraham, “nawe lazima ulishike agano langu, wewe pamoja na uzao wako baada yako kwa vizazi vyao.

Sala ya Jioni: somo

Mit 15:20–16:9

20Mwana mwenye busara huleta furaha kwa baba yake, bali mtu mpumbavu humdharau mama yake. 21Upuuzi humfurahia mtu ambaye amepungukiwa akili, bali mwenye ufahamu hutembea katika njia nyofu. 22Mipango huharibika ambapo hakuna ushauri, bali washauri wengi wanafanikiwa. 23Mtu anapata furaha wakati anapotoa jibu la kufaa; je ni zuri kiasi gani neno kwa wakati muafaka! 24Njia ya uzima huwapeleka juu watu wenye hekima, ili waondoke kutoka chini kuzimu. 25Yehova hurarua urithi wa mwenye kiburi, bali huzilinda mali za mjane. 26Yehova huyachukia mawazo ya watu waovu, bali maneno ya upole ni safi. 27Mporaji huleta shida kwenye familia yake, bali yeye ambaye huchukia rushwa ataishi. 28Moyo wa yule atendaye haki hutafakari kabla ya kujibu, bali kinywa cha watu waovu humwanga ubaya wake wote. 29Yehova yupo mbali na watu waovu, bali husikia maombi ya wale watendao haki. 30Nuru ya macho huleta furaha moyoni na habari njema ni afya kwenye mwili. 31Kama utazingatia wakati mtu anapokurekebisha jinsi ya kuishi, utabaki miongoni mwa watu wenye busara. 32Yeye anayekataa karipio hujidharau mwenyewe, bali yule asikilizaye masahihisho hujipatia ufahamu. 33Kumcha Yehova hufundisha hekima na unyenyekevu huja kabla ya heshima. 16:1Mipango ya moyo ni ya mtu, bali Yehova hutoa jawabu kutoka kwenye ulimi wake. 2Njia zote za mtu ni safi kwenye macho yake mwenyewe, bali Yehova huipima mioyo. 3Kabidhi kwa Yehova kazi zako zote na mipango yako itafanikiwa. 4Yehova alifanya kila kitu kwa kusudi lake, hata waovu kwa ajili ya siku ya taabu. 5Yehova anamchukia kila mtu mwenye moyo wa majivuno, ingawa wanasimama imara, hawakosi kupata adhabu. 6Kwa agano la uaminifu na udhamini uovu husafishwa na kwa kumcha Yehova watu hujitenga na ubaya. 7Njia za mtu zinapompendeza Yehova, huwafanya hata adui zake huyo mtu wawe na amani naye. 8Bora kitu kidogo pamoja na haki, kuliko mapato makubwa pamoja na udhalimu. 9Katika moyo wake mtu hunuia njia yake, bali Yehova huziongoza hatua zake.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 14 Aprili

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 1 Aprili katika kalenda ya kanisa ni 14 Aprili katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki