Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 12 Aprili
Kalenda ya Kiorthodoksi · 30 Machi (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 12 Aprili 2027
Jumatatu · Wiki ya 5 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 4
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Yohana wa Ngazi (649)
Kwaresima Kuu
Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Saa ya 6
33Hivyo basi Yahwe asema hivi kuhusu Asiria: ''Atakuja katika miji, wala kurusha mkuki hapa. Wala atakuja hapa mbele kwa ngao au kujenga uzio njia panda dhidi yao. 34Njia atakayojia itakuwa njia hiyo hiyo atakayorudia; ataingia katika mji huu. Hili ni Tamko ya Yahwe. 35Maana nitaulinda huu mji na kuuokoa, kwa niaba yangu mimi mwenyewe na kwa niaba Daudi mtumishi wangu.'' 36Halafu malaika wa Yahwe alienda nje na kuvamia kambi ya Waasiria, na kuwauwa askari 185,000. Watu walipoamka asubuhi na mapema, miili iliyokufa imelala kila mahali. 37Hivyo Sennacheribi mfalme wa Asiria aliiacha Israeli na kwenda nyumbani na akakaa Ninewi. 38Baadaye, na alipokuwa anabudu katika nyumba ya Nisrochi mungu wake, mtoto wake Adramaleki na Shareza alimuua kwa upanga. Halafu wakakimbilia kwenye nchi ya Ararati. Halafu Esarhadoni mtoto wake akatawala katika sehemu ya baba yake. 38:1Siku zile Hezekia alikuwa anaumwa karibia na kufa. Hivyo Isaya mtoto wa Amozi, nabii alikuja kwake na kumwambia, ''Yahwe amesema, 'panga mambo yako maana utakufa, hautaishi.' 2'Halafu Hezekia akaugeukia ukuta na akamuomba Yahwe. 3Na akasema, ''samahani Yahwe, kumbuka jinsi nilivyoenenda kwa uaminifu mbele zako kwa moyo wangu wote, na jinsi nilivyofanya matendo mema katika macho yako.'' Na Hezekia akalia kwa sauti. 4Basi neno la Yawe likamjia Isaya, na kusema, 5''Nenda ukamwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, ''Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Daudi babu yenu, amesema: Nimeyasikiliza maombi yako, na nimeyaona machozi yako. Ona ninakaribia kuongeza miaka kumi na tano katika maisha yako. 6Na nitakukomboa wewe pamoja mji huu kutoka kwenye mkono wamfalme wa Asiria, na nitaulinda huu mji.
Sala ya Jioni: somo
12Abram akaishi katika nchi ya Kanaani, na Lutu akaishi katika miji ya tambarare. Akatandaza hema zake hadi Sodoma. 13Na sasa watu wa Sodoma walikuwa waovu na wenye dhambi nyingi dhidi ya Yahwe. 14Yahwe akamwambia Abram baada ya Lutu kuondoka kwake, “Angalia kuanzia mahali ulipo simama hadi kaskazini, kusini, mashariki, na magharibi. 15Nchi yote hii uionayo, nitakupatia wewe pamoja na uzao wako milele. 16Nitawafanya uzao wako kuwa wengi kama mavumbi ya nchi, kiasi kwamba kama kuna mtu anaweza kuhesabu mavumbi ya nchi, ndipo na uzao wako pia utahesabika. 17Inuka, tembea katika urefu na upana wa nchi hii, kwa kuwa nitakupatia.” 18Kwa hiyo Abram akachukua hema yake, akaja na kukaa katika mwaloni wa Mamre, ambao uko Hebroni, na pale akajenga Madhabahu ya Yahwe.
Sala ya Jioni: somo
27Kumcha Yehova ni chemchemi ya uzima, ili kwamba mtu aweze kujiepusha kutoka katika mitego ya mauti. 28Utukufu wa mfalme upo katika idadi kubwa ya watu wake, bali pasipo watu mfalme huangamia. 29Mtu mvumilivu anaufahamu mkubwa, bali mtu mwepesi wa kuhamaki hukuza upuuzi. 30Moyo wenye raha ni uzima wa mwili, bali husuda huozesha mifupa. 31Anayemkandamiza masikini humlaani Muumba wake, bali anayeonyesha fadhila kwa wahitaji humtukuza yeye. 32Mtu mwovu huangushwa chini kwa matendo yake mabaya, bali mtu mwenye haki anakimbilio hata katika kifo. 33Hekima hukaa katika moyo wa ufahamu, bali hata miongoni mwa wapumbavu hujiachilia mwenyewe kwa kujulikana 34Kutenda haki huliinua taifa, bali dhambi ni chukizo kwa watu wowote. 35Fadhila ya mfalme ni kwa mtumishi mwenye kutenda kwa hekima, bali hasira yake ni kwa yule atendaye kwa kuaibisha. 15:1Jawabu la upole huondoa ghadhabu, bali neno la ukatili huchochea hasira. 2Ulimi wa watu mwenye hekima husifu maarifa, bali kinywa cha wapumbavu humwaga upuuzi. 3Macho ya Yehova yapo kila mahali, yakiwatazama juu ya waovu na wema. 4Ulimi unaoponya ni mti wa uzima, bali ulimi wa udanganyifu huvunja moyo.
Watakatifu wa siku
- Askofu Mtakatifu Sofronio, Askofu wa Irkutsk (1771)
- Nabii Yoadi (karne ya 10 K.K.)
- Mitume Sosthene, Apolo, Kefa, Kaisari na Epafrodito (karne ya 1)
- Mtakatifu Eubula, mama wa Mfiadini Mkuu Panteleimoni (karibu 305)
- Mtakatifu Mtawa Yohana, mnyamavu, aliyekuwa Askofu wa Kolonia (558)
- Mtakatifu Mtawa Zosima, Askofu wa Sirakusa (karibu 662)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 30 Machi katika kalenda ya kanisa ni 12 Aprili katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki