Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 28 Februari
Kalenda ya Kiorthodoksi · 15 Februari (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 28 Februari 2027
Jumapili · Sauti ya 6
Sikukuu na watakatifu
Jumapili ya Mwana Mpotevu
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Injili ya 6 ya Sala ya Alfajiri
36Wakati wakiongea mambo hayo, Yesu mwenyewe alisimama katikati yao, na akawaambia, “Amani iwe kwenu.” 37Lakini waliogopa na kujawa na hofu, na wakafikiri kwamba waliona roho. 38Yesu akawaambia, Kwanini mnafadhaika? Kwanini maswali yanainuka mioyoni mwenu? 39Angalieni mikono yangu na miguu yangu, kwamba ni mimi mwenyewe. Niguseni na muone. Kwa maana roho haina nyama na mifupa, kama mnionavyo mimi kuwa navyo.” 40Alipokwisha kusema hivi, akawaonyesha mikono yake na miguu yake. 41Walipokuwa bado na furaha iliyochanganyikana na kutokuamini, na kustaajabu, Yesu akawaambia, “Je mna kitu chochote cha kula?” 42Wakampa kipande cha samaki aliyechomwa. 43Yesu akakichukua, na kukila mbele yao. 44Akawaambia, “Nilipokuwa nanyi, niliwaambia kwamba yote yalioandikwa kwenye sheria ya Musa na manabii na Zaburi lazima yatimilike.” 45Kisha akafungua akili zao, kwamba waweze kuyaelewa maandiko. 46Akawaambia, “Kwamba imeandikwa, Kristo lazima ateseke, na kufufuka tena kutoka katika wafu siku ya tatu. 47Na toba na msamaha wa dhambi lazima ihubiriwe kwa jina lake kwa mataifa yote, kuanzia kutokea Yerusalemu. 48Ninyi ni mashahidi wa mambo haya. 49Angalia, nawapelekea ahadi ya Baba yangu juu yenu. Lakini subirini hapa jijini, mpaka mtakapovishwa nguvu kutoka juu. 50Kisha Yesu akawaongoza nje mpaka walipokaribia Bethania. Akainua mikono yake juu, na akawabariki. 51Ikatokea kwamba, wakati alipokuwa akiwabariki, aliwaacha na akabebwa juu kuelekea mbinguni. 52Basi wakamwabudu, na kurudi Yerusalemu na furaha kuu. 53Waliendelea kuwepo hekaluni, wakimbariki Mungu.
Waraka
12“Vitu vyote ni halali kwangu”, lakini si kila kitu kina faida. “Vitu vyote ni halali kwangu,” lakini sitatawaliwa na kimoja cha hivyo. 13“Chakula ni kwa ajili ya tumbo, na tumbo ni kwa ajili ya chakula,” lakini Mungu atavitowesha vyote. Mwili haujaumbwa kwa ajili ya ukahaba, badala yake, mwili ni kwa ajili ya Bwana, na Bwana atauhudumia mwili. 14Mungu alimfufua Bwana na sisi pia atatufufua kwa nguvu zake. 15Hamjui kwamba miili yenu ina muunganiko na Kristo? Mwawezaje kuvitoa viungo vya Kristo na kwenda kuviunganisha na kahaba? Haiwezekani! 16Hamjui kwamba anayeungana na kahaba amekuwa mwili mmoja naye? Kama andiko lisemavyo, “Wawili watakuwa mwili mmoja.” 17Lakini anayeungana na Bwana anakuwa roho moja pamoja naye. 18Ikimbieni zinaa! “Kila dhambi aifanyayo mtu ni nje na mwili wake. Lakini zinaa, mtu hutenda dhambi dhidi ya mwili wake mwenyewe. 19Hamjui kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu, akaaye ndani yenu, yule ambaye mlipewa kutoka kwa Mungu? Hamjui kwamba si ninyi wenyewe? 20Kwamba mlinunuliwa kwa thamani. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu kwa miili yenu.
Injili
11Na Yesu akasema, “Mtu mmoja alikua na wana wawili 12yule mdogo akamwambia babaye, Baba nipe sehemu ya mali inayonistali kuirithi. Hivyo akagawanya mali zake kati yao. 13Siku si nyingi yule mdogo akakusanya vyote anavyomiliki akaenda nchi ya mbali, na huko akatapanya hela zake, kwa kununua vitu asivyo vihitaji, na kutapanya fedha zake kwa anasa. 14Nae alipokua amekwisha tumia vyote njaa kuu iliingia nchi ile naye akaanza kuwa katika uhitaji. 15Akaenda na kujiajiri mwenyewe kwa mmoja wa raia wa nchi ile, naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. 16Na akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe kwa sababu hakuna mtu aliempa kitu chochote apate kula. 17Ila yule mwana mdogo alipozingatia moyoni mwake, alisema 'ni watumishi wangapi wa baba yangu wanachakula kingi cha kutosha na mimi niko hapa, ninakufa na njaa! 18Nitaondoka na kwenda kwa baba yangu, na kumwambia, “Baba nimekosa juu ya mbingu na mbele ya macho yako. 19Sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.” 20Ndipo akaondoka akaenda kwa baba yake. Alipokua angali mbali baba yake alimuona akamwonea huruma akaenda mbio na kumkumbatia na kumbusu. 21Yule mwana akamwambia, 'baba nimekosa juu ya mbingu na mbele ya macho yako sistahili kuitwa mwana wako.' 22Yule baba aliwaambia watumishi wake, 'lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike mtieni na pete kidoleni na viatu miguuni. 23Kisha mleteni ndama yule alienona mkamchinje tule na kufurai. 24Kwa kuwa mwanangu alikua amekufa naye yu hai. Alikua amepotea nae ameonekana wakaanza kushangilia. 25Basi yule mwanae mkubwa alikuwako shamba. Alipokuwa akija na kuikaribia nyumba alisikia sauti ya nyimbo na michezo. 26Akaita mtumishi mmoja akamuuliza mambo haya maana yake nini? 27Mtumishi akamwambia mdogo wako amekuja na baba yako amemchinjia ndama aliyenona kwa sababu amerudi salama.' 28Mwana mkubwa akakasirika akakataa kuingia ndani na babaye alitoka nje kumsihi. 29Ila akamjibu babayake akisema, 'Tazama mimi nimekutumikia miaka mingi, wala sijakosa amri yako, lakini hujanipa mwana mbuzi, ili niweze kusherehekea na rafiki zangu. 30Lakini alipokuja huyu mwana wako aliyetapanya mali yako yote pamoja na makahaba umemchinjia ndama alienona. 31Baba akamwambia, 'Mwanangu, wewe u pamoja nami siku zote na vyote nilivyo navyo ni vyako. 32Ila ilikua vyema kwetu kufanya sherehe na kufurahi, huyu ndugu yako alikua amekufa, na sasa yu hai; alikua amepotea naye ameonekana.”
Watakatifu wa siku
- Mtume Onesimo, mmoja wa Mitume 70 (karibu 109)
- Wafiadini wa Kikasisi Mikaeli na Yohana, mapadri (1930)
- Wafiadini wa Kikasisi Nikolao, Aleksi, Aleksi, mapadri, Simeoni, shemasi, Mtawa Mfiadini Petro na Mtawa Mfiadini Sofia (1938)
- Mtakatifu Mtawa Pafnuti na binti yake Eufrosini (karne ya 5)
- Mtakatifu Mtawa Eusebio, mkaa jangwani wa Shamu (karne ya 5)
- Mtakatifu Mtawa Pafnuti, mtawa wa faragha wa Mapango ya Kyiv (karne ya 13)
- Ikoni za Mama wa Mungu za Vilnius (ilihamishiwa Vilnius mwaka 1495) na ya Dalmatovo (1646)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 15 Februari katika kalenda ya kanisa ni 28 Februari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki