Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 28 Februari
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 28 Februari 2027
Jumapili · Juma la 3 la Kwaresima
Sikukuu na watakatifu
Dominika ya 3 ya Kwaresima
Dominika · Rangi ya liturujia: zambarau
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Mungu alisema maneno yote haya: 2Ndimi Bwana Mungu wenu, niliyewatoa katika ardhi Misri, nje ya nyumba ya utumwa. 3Msiwe na miungu mingine ila mimi tu. 4Msijitengenezee sanamu za kuchonga kufananisha na kitu chochote kilichopo juu ya mbingu, chini ya ardhi, au ndani ya maji. 5Msipinde na kuabudu sanamu, mimi Yahweh Mungu wenu, ni Mungu mwenye wivu. Nitaadhibu uovu wa mabubu kwa kuleta adhabu juu ya kizazi, cha tatu hadi kizazi cha nne kwa wale wanao nichukia. 6Ila nitaweka agano la uaminifu kwa maelfu watakao nipenda na kushika amri zangu. 7Usilitaje bure jina la Yahweh Mungu wako, sitkuwa na hatia kwa yeyote atakaye taja jina langu bure. 8Ikumbuke siku ya Sabato, na kunitengea. 9lazima ufanye kazi zako zote kwa siku sita. 10Ila siku ya saba ni Sabato kwaajili ya Yahweh Mungu wako. Siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, au mwana wako, au binti yako, au mtumishi wako wakiume, au mtumishi wako mwanamke, au ng'ombe zako, au mgeni aliye ndani ya malango yako. 11Kwa siku sita Yahweh aliumba mbingu na nchi, bahari, na vitu vyote vilivyomo, na siku ya saba alipumzika. Kwa hiyo Yahweh aliibariki siku ya Sabato na kuitenga. 12Waheshimu baba na mama yako, ili uweze kuishi miaka mingi duniani Yahweh Mungu wako ametoa. 13Usiue. 14Usifanye uasherati (usizini). 15Usiibe kwa mtu yoyote. 16Usishuhudie uongo dhidi ya jirani yako. 17Usitaman nyumba ya jirani yako; usitamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wakiume, mtumishi wake mwanamke, ng'ombe wake, punda wake, au chochote cha jirani yako.
Wimbo wa katikati
7Sheria ya Yahwe ni kamilifu, huokoa roho; ushuhuda wa Yahwe ni wa kuaminika, ukifanya hekima nyepesi. 8Maelekezo ya Yahwe ni ya hakika, yakiufanya moyo kuwa na furaha; amri ya Yahwe ni safi, ikileta mwanga kwenye macho yetu. 9Hofu ya Yahwe ni safi, inadumu milele; amri za haki ya Yahwe ni za kweli na zote ni za hakika! 10Nazo zina thamani kuliko dhahabu, nazo ni tamu kuliko asali na matone ya asali kutoka sega la asali (sega la nyuki).
Somo la pili
22Kwa Wayahudi huuliza ishara za miujiza na kwa Wayunani hutafuta hekima. 23Lakini tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa, aliye kikwazo kwa Wayahudi na ni ujinga kwa Wayunani. 24Lakini kwa wale ambao waliitwa na Mungu, Wayahudi na Wayunani, tunamhubiri Kristo kama nguvu na hekima ya Mungu. 25Kwa kuwa ujinga wa Mungu una hekima kuliko ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.
Injili
13Basi Pasaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia, hivyo Yesu akaenda Yerusalemu. 14Akawakuta wauzaji wa ng'ombe, kondoo, na njiwa ndani ya Hekalu. Pia na wabadilisha fedha walikuwa wameketi ndani ya Hekalu. 15Yesu akatengeneza mjeledi wenye vifundo, akawatoa wote walikuwemo katika hekalu, ikijumuisha ng'ombe na kondoo. Akamwaga fedha za wabadili fedha na kuzipindua meza zao. 16Kwa wauzaji wa njiwa akawambia, “Toeni vitu hivi mbali na mahali hapa, acheni kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa mahali pa soko.” 17Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa ilikuwa imeandikwa, “Wivu wa nyumba yako utanila.” 18Wakuu wa Kiyahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara ipi utakayoionyesha kwa sababu unayafanya mambo haya?” 19Yesu akawajibu, libomoeni Hekalu hili nami nitalijenga baada ya siku tatu.” 20Kisha wakuu wa Wayahudi wakasema, “Iligharimu miaka arobaini na sita kujenga hekalu hili nawe unasema utalijenga kwa siku tatu?” 21Ingawa, yeye aliongea hekalu akimaanisha mwili wake. 22Hivyo baadaye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka kuwa alisema hivyo, wakaamini maandiko na kauli hii ambayo Yesu alikuwa amekwisha kuisema. 23Basi alipokuwa Yerusalemu wakati wa Pasaka, wakati wa sikukuu watu wengi waliamini jina lake, walipoona ishara ya miujiza aliyoifanya. 24Lakini Yesu hakuwa na imani nao kwa sababu aliwajua wanadamu wote. 25Hakuhitaji mtu yeyote kumwambia kuhusu walivyo wanadamu kwa sababu alijua kilichokuwamo ndani yao.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki