Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Sulemani

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Sulemani

Sulemani awabariki watu

1 Fal 8:12–21 · 2 Nya 6:1–11

1 Wafalme

1 Fal 8:12–21

12Kisha Sulemani akasema, “BWANA amsema kuwa anaweza kuishi hata kwenye giza nene,

13Lakinni nimekujengea makao ya kujivunia, mahali pako pa kuishi milele.”

14Kisha mfalme akageuka na kuwabariki mkusanyiko wa watu wa Israeli, wakati huo mkusanyiko wa Waisraeli walikuwa wamesimama.

15Akasema, “BWANA, Mungu wa Israeli, asifiwe, ambaye alisema na baba yangu Daudi, na ametimiza kwa mikono yake, akisema,

16'Tangu siku ile niliyowatoa watu wangu Israeli kutoka Misri, sikuchagua mji wowote toka kwa makabila yote ya Israeli ambako ningeijenga nyumba, kwa ajili ya jina langu kuwemo humo. Hata hivyo, nilimchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.

17Sasa ilikuwa kwenye moyo wa Daudi baba yangu kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli.

18Lakini BWANA alimwambia baba yangu Daudi, 'Ilikuwa ndani ya moyo wako kunijengea nyumba kwa jina langu, ulifanya vyema kwa hilo kuwa ndani ya moyo wako.

19Ingawa hutanijengea nyumba; badala yake mwanao, mmoja wa wanao atakayezaliwa toka viunoni mwako, atanijengea nyumba kwa jina langu,'

20BWANA amelibeba lile neno slilokuwa amesema, kwa kuwa nimeinuka mahali pa baba yangu Daudi, na nimeketi kwenye kiti cha enzi cha Israeli, kama BWANA alivyoahidi. Nimeijenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli.

21Nimetengeneza mahali kwa ajili ya sanduku ndani yake, ambamo ndani yake kuna agano la BWANA, ambalo alifanya na baba zetu alipowatoa toka nchi ya Misri,”

2 Mambo ya Nyakati

2 Nya 6:1–11

1Kisha Selemani akasema, “Yahwe alisema kwamba ataishi katika giza nene,

2lakini nimekujengea makao makuu, sehemu kwa ajili yako ya kuishi milele.”

3Kisha mfaalme akageuka nyuma na kuwabariki kusanyiko lote la Israeli, wakati kusanyiko lote la Israeli walikuwa wamesimama.

4Akasema, “Yahwe, Mungu wa Israeli, usifiwe, uliyesema na Daudi baba yangu, na ametimiza kwa mikono yake mwenyewe, akisema.

5'Tangu siku nilipowaleta watu wanagu nje ya nchi ya Misiri, sikuchaagua mji wowote nje ya makabaila yote ya Israeli ambamo nyumba ingejengwa, ili jina lanagu liwe humo. Wala sikuchagua mtu yeyote kuwa mfalme juu ya watu wangu Israeli.

6Aidha, nimechagua Yeruselemu, ili kwamba jina langu liwe humo, na nimemchagua Daudi kuwa juu ya watu wanagu Israeli. '

7Sasa ilikuwa ndani ya moyo wa Daudi baba yangu, kujenga nyumba kwa ajili ya jina la Yahwe, Mungu wa Israeli.

8Lakini Yahwe alisema kwa Daudi Baba yanagu. 'Kwmba ilikuwa ndani ya moyo wako kujenga nyumba kwa ajili ya jina langu, ulifanya vizuri kwa hili kuliweka moyono mwako.

9Aidha, hutaijenga ile nyumba, badala yake, mwanao, mmoja atakayetoka kwenye viuno vyako, ataijenga nyumba kwa ajili ya jina langu.'

10Yahwe ameyatimiza maneno aliyokuwa amesema, kwa maana nimeiinua sehemu ya Daudi baba yangu, na ninkaa juu ya kiti cha enzi cha Israeli, kama alivyoahidi Yahwe. Nimeijenga nyumba kwa ajii ya jina la Yahwe, Mungu wa Israeli.

11Nimeliweka humo sanduku, amabamo kuna agano la Yahwe, alilofanya na watu wa Israeli.”

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY