Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Sulemani

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Sulemani

Maombi ya Sulemani ya kuweka wakfu hekalu

1 Fal 8:22–53 · 2 Nya 6:12–42

1 Wafalme

1 Fal 8:22–53

22Sulemani alisimama mbele ya madhabahu ya BWANA, mbela ya mkusanyiko wote wa Waisraeli, naye akanyosha mikono yake kuelekea mbinguni.

23Akasema, “BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe juu mbinguni au chini duniani, ambaye hutunza agano lake kwa uaminifu kwa watumishi wako ambao hutembea mbele yako kwa mioyo yao yote;

24wewe ambaye umetunza ahadi yako na mtumishi wako Daudi baba yangu ile uliyomwahidi. Naam, ulisema kwa kinywa chako na sasa umeitimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo.

25Sasa basi, BWANA, Mungu wa Israeli, timiza kile ulichomwahidi mtumishi wako Daudi baba yangu, pale uliposema, 'Hautashindwa kunipa mtu mbele ya macho yangu ambaye ataketi katika kiti cha enzi cha Israeli, kama tu uzao wako watakuwa waangalifu kutembea mbele yangu, kama vile wewe ulivyotembea mbele yangu.'

26Sasa basi, Mungu wa Israeli, Ninaomba kwamba ile ahadi uliyofanya kwa mtumishi wako Daudi baba yangu, itimie.

27Je, ni kweli kwamba Mungu ataishi duniani? Tazama, Ulimwengu wote na mbingu hazikutoshi - sembuse nyumba hii niliyoijenga!

28Kwa hiyo Mungu naomba uyajali maombi haya ya mtumishi wako na maombi yake, BWANA, Mungu wangu; sikiliza kilio na maombi ambayo mtumishi wako anakuomba leo.

29Naomba ulitazame hekalu hili mchana na usiku, mahali ambapo ulisema, 'Jina langu na uwepo wangu utakuwa' - ili niweze kuwa nasikiliza maombi ambayo mtumishi wako ataomba mahali hapa.

30Kwa hiyo sikia maombi ya mtumishi wako na ya watu wako Israeli tunapokuwa tunaomba mahali hapa. Ndiyo, sikia kutokea mahali ambapo unaishi, kutoka katika mbingu za mbingu; na unaposikia tafadhali samehe.

31Kama mtu atamtendea uovu jirani yake na anapewa sharti la kiapo, na kama atakuja na kuapa mbele ya madhabahu yako katika nyumba hii,

32basi usikie kutoka mbinguni ukatende na kuwahukumu watumishi wako, ukamhukumu mwovu, ili kuwaletea tabia zake kichwani mwake, na kumtunza mwenye haki kuwa hana hatia, na kumpa thawabu yake ya haki.

33Watu wako Israeli watakapopigwa na adui kwa sabau ya kutenda dhambi dhidi yako, na kama watakurudia, na kulikiri jina lako, na kukusihi, na kuomba msamaha kwako katika hekalu hili-

34tafadhali nakuomba usikie kutoka mbinguni na usamehe dhambi za watu wako Israeli; uwarudishe katika nchi ambayo uliwapa mababu zao.

35Kama mbingu zitafungwa na mvua hazinyeshi kwa sababu watu wamekutenda dhambi wewe - na kama wataomba mahali hapa, na kulikiri jina lako, na kugeuka toka dhambi zao na kama umewapiga -

36basi sikia tokea mbinguni na usamehe dhambi za watumishi wako na za watu wako Israeli, utakapowafundisha njia njema inayowapasa; basi uinyeshee mvua nchi yako, ambayo uliwapa watu wako kuwa urithi.

37Na kama kuna njaa katika nchi, au kama kuna magonjwa, au ukungu, nzige au funza; au kama adui atavamia malango ya mji katika nchi yao, kama kuna tauni au magonjwa yeyote -

38na kama kuna mtu au wata wa Israeli wataomba - kila mmoja akaijua hiyo tauni katika moyo wake wakati akinyosha mikono yake katika hekalu hili.

39Basi usikie kutoka mbinguni, mahali unapoishi, utende na kusamehe, na umpe kila mtu thawabu anayostahili kwa kile anachofanya; wewe unajua moyo wake, kwa sababu ni wewe pekee yako ujuaye mioyo ya watu.

40Fanya hivi ili kwamba wawe na hofu kwako katika siku zote za maisha yao wanayoishi katika nchi uliyowapa mababu zetu.

41Na nyongeza yake, kuhusiana na mgeni ambaye si mtu wako wa Israeli: atakapokuja kutokea nchi ya mbali kwa sababu ya jina lako -

42kwa sababu watasikia jina lako lilivyo kuu, mkono wako wenye nguvu, na mkono wako ulioinuliwa - atakapokuja na kuomba mahali hapa pa hekalu,

43tafadhali usikie kutokea katika mbingu, mahali unapoishi, na umfanyie huyo mgeni akuombacho. Fanya hivi ili makundi ya wtu wote duniani wakujue jina lako na kukuhofia, kama wanavyofanya watu Israeli. Fanya hivyo ili wajue kwamba nyumba hii niliyoijenga inaitwa kwa jina lako.

44Na kama watu wko wataenda vitani dhidi ya adui, kwa njia yeyote unayoweza kuwatuma, na kama watakuomba wewe, BWANA, kuelekea mji huu uliuchagua, na kuekea nyumba ambayo nimeijenga kwa jina lako.

45Basi sikia tokea mbinguni maombi yao, dua zao, na uwasaidie wanachohitaji.

46Na kama watafanya dhambi dhidi yako, kwa kuwa hakuna hata mtu mmoja asiyefanya dhambi, na kama una hasira dhidi yao na kuwapeleka kwa maadui, ili kwamba maadui wawachukue mateka katika nchi yao, mbali au karibu.

47Na kama watatambua kuwa wako katika nchi ya utumwa, na kama watatubu na kuomba neema kwako kutokea katika nchi ya watekaji. Na kama watasema, 'tumetenda kwa ukaidi na tumefanya dhambi. Tumetenda kwa uovu.'

48Na kama watarudi kwako kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote katika chi ya maadui ambao wanawakamata, na kama watakuomba wewe kuelekea nchi yao, ambayo uliwapa mababu zao, na kuelekea katika mji uliouchagua, nakuelekea kaika nyumba ambayo nimeijenga kwa jina lako.

49Basi usikie maombi yao, na dua zao tokea mbinguni, mahali unapoishi, na ukaitetee haki yao.

50Wasamehe watu wako waliotenda dhambi dhidi yako, na dhambi zao zote ambazo kwazo wamekukosea wewe dhidi ya amri zako. Uwahurumie mbele ya maadui zao ambao waliwachukua mateka, ili kwamba maadui zao pia wawahurumie watu wako.

51Hawa ni watu wako uliowachagau, ambao uliwaokoa toka nchi ya Misri kama kwamba walikuwa katikati ya tanuru amabamo vyuma huyeyushwa.

52Naomba kwamba macho yako yatazame dua za mtumishi wako na kwa dua za watu wako Issraeli, ili uwasike kila wanapokulilia.

53Kwa kuwa uliwatenga toka kwa watu wengine wa duniani ili wawe wako nakupokea ahadi zako, kama vile ulivyomwambia Musa mtumishi wako, wakati ulipowatoa babazetu toka Misri, BWANA.”

2 Mambo ya Nyakati

2 Nya 6:12–42

12Selemani akasimama mbele ya madhabahu ya Yahwe mbele za kusanyiko lote la Israeli, na akanyosha mikono yake.

13Kwa mana alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba, lenye urefu wa mikono mitano, upana wa mikono mitano, urefu wake kwenda juu mikono mitatu. Alikuwa ameliweka katika ya uwanja. Akasimama juu yake na kupiga magoti mbele ya kusanyiko la Israeli, kisha akanyosha mikono yake kuzielekea mbingu.

14Akasema, “Yahwe, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe katika mbingu, au juu ya dunia, ambaye anatunza agano na upendo imara na watumishi wako ambao hutembea mbele zako kwa moyo wao wote;

15wewe uliyetimtimizia Daudi baba yanagu, uliyokuwa umemwahidi. Ndiyo, ulisema kwa kinywa chako na umetimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo.

16Sasa, Yahwe, Mungu wa Israeli, tunza ahadi uliyoahidi kwa mtumishi wako Daudi baba yangu, uliposema, 'Hautashindwa kupata mtu mbele yangu wa kukaa juu ya kiti cha enzi cha Israeli, ikiwa tu uzao wako ni waangalifu kutembea katika sheria yangu, kama wewe ulivyotembea mbele zangu.

17Sasa, Mungu wa Israeli, ninaomba kwamba ahadi uliyofanya kwa mtumishi wako Daudi itakuwa kweli.

18Lakini kweli Mungu ataishi na wanadamu juu ya dunia? Angalia, dunia yoye na mbugu yenyewe haviwezi kukubeba -sembuse na hekalu hili nililojenga!

19Nakusihi yaheshimu maombi haya ya mtumishi wako na ombi lake. Yahwe Mungu wangu; sikia kilio na amaombi ambayo mtumishi wako anaomba mbele zako.

20Fumbua macho yako kuelekea hekaalu hili usiku na mchana, sehemu aambaayo uliahidi kuliweka jina lako. Nakuomba usikie maombi atakayoomba mtumishi wako kuelekea sehemu hii.

21Hivyo sikia maombi ya mtumishi na ya watu wako Israeli tunapoomba kuelekea sehemu hii. Ndiyo, sikia kutoka mahali unapoishi, kutoka mbinguni; na unaposikia, samehe.

22Kama mtu atamtenda dhambi jirani yake na ikampasa kuapa kiapo, na ikiwa atakuja na kuapa kiapo mbele ya madhabahu yako katika nyumba hii,

23basi sikia kutoka mbinguni na kutend na ukawahukumu watumishi wako, ukamlipizie mwovu, ili kuyaleta matendo yake juu ya kichwa chake. Ukamtangaze mwenye haki kuwa hana hatia, ili kumlipa thawabu kwa ajili ya uaminifu wake.

24Watu wako watakaposhindwa na adui kwa sababu wamekutenda dhambi, kama watageuka nyuma kwako, wakilikili jina lako, wakisali na kuomba msamaha mbele zako hekaluni—

25basi tafadhali sikia mbinguni na usamehe dhambi za watu wako Isaraeli; uwarudishe katika nchi uliyoitoa kwa ajili yao na baba zao.

26Wakati mbingu zimefungwa na hakuna mvua kwa sababu watu wamekutenda dhambi—ikiwa wataomba kuelekea sehemu hii, wakilikili jina lako, na kuziacha dhambi zao utakapokuwa umewaadhibu—

27basi sikia mbinguni na usamehe dhambi za watumishi wako na watu wako Israeli, utakapowaelekeza kwenye njia njema iwapasayo kutembea. Tuma mvua juu ya nchi yako, ambayo umewapa watu wako kama urithi.

28Kama kuna njaa katika nchi, au kama kuna ugonjwa, tauni au ukungu, nzige au viwavijeshi, au kama adui wake wameyavamia malango ya mji katika nchi yao, au kwamba kuna pigo lolote au ugonjwa—

29na ikiwa sala na maombi yamefanywa na mtu au watu wako wote Israel—kila mmoja akilijua pigo na huzuni katika moyo wake akinyosha mikono yake kuelekea hekalu hili.

30Basi sikiliza mbinguni, sehemu ambayo unaishi; samehe, na umlipe kila mtu kwa njia zake zote; uhaujua moyo wake, kwa sababu wewe na ni wewe pekee unaijua mioyo ya wanadamu.

31Fanya hivyo ili kwamba wakuogope wewe, ili waweze kutembea katika katika njia zako siku zote ambazo wataishi katika nchi uliyowapa baba zetu.

32Kwa mgeni ambaye siyo sehemu ya watu wako Israeli, lakini ambaye- kwa sababu ya ukuu wa jina lako, mkono wako wenye nguvu, na mkono wako ulionyoshwa- akija na kuomba kuelekea sehemu nyumba hii,

33basi sikiliza mbinguni, sehemu ambayo unaishi, na fanya yote ambayo mgeni atakuomba, ili kwamba watu wote wa dunia walijue jina lako na kukuogopa wewe, kama wafanyavyo watu wako Israeli, na kwamba waweze kujua kwamba nyumba hii niliyoijenga inaitwa kwa jina lako.

34Ikiwa kwamba watu wako wakaenda nje kupigana dhidi ya adui zao, kwa njia yoyote amabayo unaweza kuwatuma, na ikiwa kwamba wakaomba kwako kuelekea mji huu ambao umeuchagua, na kuelekea nyumba ambayo nimeijenga kwa ajili ya jina lako.

35Basi sikiliza maombi yao mbinguni, ombi lao, na uwasaidie.

36Kama wametenda dhambi dhidi yako—kwa kuwa hakuna asiye tenda dhambi—na ikiwa una hasira nao na kuwakabidhi kwa adui zao, ili kwamba adui wakawabeba na kuwachukua kama mateka kwa ajili ya nchi zao, iwe mbali au karibu.

37Kisha wakatambua kuwa wako katika nchi ambako wamewekwa utumwani, na ikiwa watatubu na kutafuta msaada kwako katika utumwa wao. ikiwa watasema, 'Tumetenda kinyume na kutenda dhambi. Tumetenda kwa uovu,'

38ikiwa watarudi kwako kwa mioyo yao yote na kwa nia yao yote katika nchi ya utumwa wao, ambako walichuliwa kama mateka, na ikiwa wataomba kukabili nchi yao, uliyowapa babu zao, na kukabili mji ambao uliuchagua na kukabili nyumba ambayo niliijenga kwa ajili ya jina lako.

39Basi sika kutoka mbinguni, mahali unapoishi, sikia kuomba kwao na maombi na wayaombayo, na uwasaidie shida zao. Wasamehe watu wako, ambao wamekutenda dhambi.

40Sasa, Mungu wangu, ninakusihi, uyafungue macho yako, na masikio yako yasiskie maombi yatakayofanywa katika sehemu hii.

41Sasa basi, amka, Yahwe Mungu, kwenye mahali pako pa kupumzikia, Wewe na sanduku la nguvu zako. Makuhani wako, Yahwe Mungu, wavikwe wokovu, na watakatifu wako wafurahi katika wema.

42Yahwe Mungu, usiugeuze nyuma uso wa masihi wako. Yakumbuke matendo yako katika agano lako la ufalme kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY