Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Katika Yerusalemu

Injili kando kwa kando · Katika Yerusalemu

Mfano wa wakulima waovu

Mt 21:33–46 · Mk 12:1–12 · Lk 20:9–19

Mathayo

Mt 21:33–46

33Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu, mtu mwenye eneo kubwa la ardh. Alipanda mizabibu, akaiwekea uzio, akatengeneza na chombo cha kukamlia divai, akajenga na mnara wa walinzi, na akalikodisha kwa watunza zabibu. Kisha akaenda katika nchi nyingine.

34Wakati wa mavuno ya mizabibu ulipokaribia, aliwatuma baadhi ya watumishi kwa wakulima wa mizabibu kuchukua mizabibu yake.

35Lakini wakulima wa zabibu wakawachukua watumishi wake, wakampiga mmoja, wakamwua mwingine, na wakampiga mmoja kwa mawe.

36Kwa mara nyingine, Mmiliki aliwatuma watumishi wengine, wengi zaidi ya wale wa kwanza, lakini wakulima wa mizabibu waliwatendea vilevile.

37Baada ya hapo bwana yule akamtuma kwao mwana wake, akisema, 'Watamheshimu mwanangu.''

38Lakini wakulima wa mizabibu walipomwona kijana yule, wakaambizana, 'Huyu ni mrithi, Njooni, tumuue na tumiliki urithi.'

39'Hivyo wakamchukua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu na kumwua.

40Je mmliki wa shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanya nini wakulima wa mizabibu?”

41Wakamwambia, “Atawaharibu hao watu waovu katika njia ya ukali zaidi, na kisha atalikodisha shamba la mizabibu kwa wakulima wengine wa mizabibu, watu ambao watalipa kwa ajili ya mizabibu itakapoiva.”

42Yesu akawaambia, “Hamkusoma katika maandiko, 'Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi. Hili lilitoka kwa Bwana, na inashangaza machoni petu?'

43Hivyo nawaambieni, Ufalme wa Mungu utatwaliwa kutoka kwenu na kupewa taifa linalojali matunda yake.

44Yeyote atakayeanguka juu ya jiwe hilo atavunjwa vipandevipande. Lakini kwa yeyote litakayemwangukia, litamsaga.”

45Wakuu wa makuhani na mafarisayo waliposikia mifano yake, wakaona kuwa anawazungumzia wao.

46Lakini kila walipotaka kunyosha mikono juu yake, waliogopa makutano, kwa sababu watu walimtazama kama nabii.

Marko

Mk 12:1–12

1Kisha Yesu alianza kuwafundisha kwa mifano. Akasema, “Mtu alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia uzio, na akachimba shimo la kusindika mvinyo. Akajenga mnara na kisha akalipangisha shamba la mizabibu kwa wakulima wa mizabibu. Kisha alisafiri safari ya mbali.

2Wakati ulipofika, alimtuma mtumishi kwa wakulima wa mizabibu kupokea kutoka kwao baadhi ya matunda ya shamba la mizabibu.

3Lakini walimkamata, wakampiga, na wakamfukuza bila chochote.

4Akamtuma kwao mtumishi mwingine, wakamjeruhi kichwani na kumtendea mambo ya aibu.

5Bado alimtuma mwingine, na huyu mmoja walimwua. Waliwatendea wengine wengi mambo kama hayo hayo, wakiwapiga na wengine kuwaua.

6Alikuwa bado na mtu mmoja zaidi wa kumtuma, mwana mpendwa. Naye alikuwa wa mwisho aliyetumwa kwao. Akisema, “Watamheshimu mwanangu”.

7Lakini wapangaji walisemezana wao kwa wao, “Huyu ndiye mrithi. Njoni, hebu na tumwue, na urithi utakuwa wetu.”

8Walimvamia, wakamuua na kumtupa nje ya shamba la mizabibu.

9Kwa hiyo, Je! Atafanya nini mmiliki wa shamba la mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wakulima wa mizabibu na atalikabidhi shamba la mizabibu kwa wengine.

10Hamjapata kusoma andiko hili? “Jiwe ambalo wajenzi walilikataa, limekuwa jiwe la pembeni.

11Hili lilitoka kwa Bwana, na ni la ajabu machoni petu.”

12Walitafuta kumkamata Yesu, Lakini waliwaogopa makutano, kwani walijua kuwa alikuwa amenena mfano huo dhidi yao. Hivyo walimwacha na wakaenda zao.

Luka

Lk 20:9–19

9Aliwaambia watu mfano huu, “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima wa mizabibu, na akaenda nchi nyingine kwa muda mrefu.

10Kwa muda uliopangwa, alimtuma mtumishi kwa wakulima mizabibu, kwamba wampe sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wakulima wa mzabibu wakampiga, wakamrudisha mikono- mitupu.

11Kisha akamtuma tena mtumishi mwingine na nao wakampiga, kumtendea vibaya, na wakamrudisha mikono- mitupu.

12Alimtuma tena wa tatu na nao wakamjeruhi na kumtupa nje.

13Hivyo bwana wa shamba akasema, 'Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpendwa. Labda watamheshimu. '

14Lakini wakulima wa mzabibu walipomwona, walijadili wao kwa wao wakisema, 'Huyu ndiye mrithi. Tumuue, ili urithi wake uwe wetu. '

15Wakamtoa nje ya shamba la mizabibu na kumuua. Je bwana shamba atawafanya nini?

16Atakuja kuwaangamiza wakulima wa mzabibu, na atawapa shamba hilo wengine”. 'Nao waliposikia hayo, wakasema, 'Mungu amekataa'

17Lakini Yesu akawatazama, akasema, “Je andiko hili lina maana gani? 'Jiwe walilolikataa wajenzi, limekuwa jiwe la pembeni'?

18Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo, atavunjika vipande vipande. Lakini yule ambaye litamwangukia, litamponda. '

19Hivyo waandishi na wakuu wa makuhani walitafuta njia ya kumkamata wakati huohuo, walijua kwamba alikuwa amesema mfano huu dhidi yao. Lakini waliwaogopa watu.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY