Mwanzo › Biblia inasema nini › Kumngoja Mungu
Imani
Biblia inasema nini kuhusu Kumngoja Mungu
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (14), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Isa 40:31
Lakini wale watakao mngojea Yahwe watapewa nguvu mpya; na watapaa kwa mbawa kama malaika; watakimbia wala hawatachoka; watatembea wala hawatazimia.Zab 27:14
Umngoje Yahwe; uwe imara, na moyo wako uwe jasiri! Umngoje Yahwe!Zab 37:7
Uwe kumya mbele za Yahwe na umsubiri yeye kwa uvumilivu. Usikasirike ikiwa kuna mtu anafanikiwa kwa kile afanyacho, au afanyapo njama za uovu.Omb 3:25
Yahweh ni mwema kwao wanao msubiri, kwa anaye mtafuta.Isa 30:18
Lakini Bwana anawasubiri ili awape neema yake, Hivyo basi yuko tayari kuwaonyesha huruma. Maana Yahwe na Mungu wa haki; Huwabarikiwe wale wanaomsubiri yeye.Zab 130:5
Ninamngoja Yahwe, nafsi yangu inasubiri, na katika neno lake ninatumainia.Mik 7:7
Lakini kama kwangu mimi, nitamtazama Yahwe. Nitamsubiri Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu ataniskia.Yak 5:7–8
Kwa hiyo vumilieni, ndugu, mpaka ujio wa Bwana, kama mkulima husubiri mavuno ya thamani toka katika nchi, akisubiri kwa uvumilivu kwa ajili yake, mpaka mvua za kwanza na zile za mwisho zikinyesha. Pia ninyi muwe wavumilivu; kazeni mioyo yenu, kwa sababu kuja kwake Bwana ni karibu.Zab 33:20
Sisi tunamngoja Yahwe, yeye ni msaada wetu na ngao yetu.Zab 62:5
Katika ukimya ninamsubiri Mungu pekee; kwa maana matumaini yangu yako kwake.Hab 2:3
Sababu maono haya bado ni kwa wakati ujao na hatimaye atazungumza bila kuanguka. Ingawa inachelewa, isubiri. Sababu kwa hakika itatakuja na haitachelewa.Zab 37:34
Umngoje Yahwe na uishike njia yake, naye atakuinua uimiliki nchi. Atakapo waondosha waovu wewe utaona.Isa 64:4
Tangu nyakati za kale hakuna hata mmoja aliyesikia au kujua, wala jicho kuona Mungu yeyote karibu yake, ni nani afanyae mambo haya kwake anayemsubiri yeye.Zab 38:15
Hakika ninakungoja wewe, Yahwe; wewe utanijibu, Bwana Mungu wangu.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0