Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Biblia

Imani

Biblia inasema nini kuhusu Biblia

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (15), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

2 Tim 3:16Kila andiko limetiwa pumzi na Mungu. Linafaa kwa mafundisho yenye faida, kwa kushawishi, kwa kurekebisha makosa, na kwa kufundishia katika haki.
Ebr 4:12Kwa maana neno la Mungu li hai na lina nguvu na linaukali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili. Na huchoma hata kufikia kugawanya nafsi na roho, na viungo kutika uboho. Na lenye kuweza kufahamu fikira za moyo nia yake.
Rum 15:4Kwa chochote kilichotangulia kuandikwa, kiliandikwa kwa kutuelekeza, kwa kusudi kwamba kupitia uvumilivu na kupitia kutiwa moyo na maandiko tungekuwa na ujasiri.
Zab 119:105Neno lako ni taa ya mguu miguu yangu na mwanga wa njia yangu.
Mt 4:4Lakini Yesu alimjibu na kumwambia, “Imeandikwa, 'Mtu hataishi kwa mkate peke yake, bali kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu.'''
Yos 1:8Siku zote uuongee juu ya kitabu hiki cha sheria. Utakitafakari mchana na usiku ili kwamba uweze kutii yote yaliyoandikwa humo. Kisha utastawi na kufanikiwa.
Zab 119:11Moyoni mwangu nimeliweka neno lako ili nisije nikakutenda dhambi.
Zab 119:18Ufungue macho yangu ili niweze kuona mambo ya ajabu katika sheria yako.
1 Pet 2:2Kama watoto wachanga, mtamani maziwa safi ya kiroho, ili kwamba mweze kukua ndani ya wokovu,
Mit 30:5Kila neno la Mungu limejaribiwa, yeye ni ngao kwa wale wanaokimbilia kwake.
Yn 17:17Uwaweke wakfu kwako mwenyewe katika Kweli; neno lako ndiyo kweli.
Ayu 23:12Sijaiacha amri ya midomo yake; nimeyatii maneno ya kinywa chake.
Isa 55:11hivyo neno langu litakuwa linalotoka kwenye mdomo wangu: halitanirudia tena mimi bure, Lakini itatimiza lilie nililokusudia, na litatimiza lile nililolituma.
Mk 13:31Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Rum 10:17Hivyo imani huja kutokana na kusikia, na kusikia kwa neno la Kristo.

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0