Mwanzo › Biblia inasema nini › Uaminifu wa Mungu
Imani
Biblia inasema nini kuhusu Uaminifu wa Mungu
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (12), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
1 Yoh 1:9
Lakini tukizitubu dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na haki kutusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.2 Tim 2:13
kama hatutakuwa waaminifu, yeye atabaki kuwa mwaminifu, maana hawezi kujikana mwenyewe.”Ebr 10:23
Basi na tushikilie kwa uthabiti katika ungamo la ujasiri wa tumaini letu, bila ya kugeuka, kwa sababu Mungu aliyeahidi ni mwaminifu.Omb 3:22–23
Upendo dhabiti wa Yahweh haukomi na huruma zake haziishi, ni mpya kila asubui; uaminifu wako ni mkubwa.Kum 7:9
Kwa hiyo tambua ya kuwa Yahwe Mungu wako-ni Mungu, Mungu mwaminifu, anayetunza maagano na uaminifu kwa vizazi elfu kwa wale wanaompenda na kuyashika maagizo yake,2 The 3:3
Lakini Bwana ni mwaminifu, ambaye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutoka kwa yule mwovu.1 Kor 10:13
Hakuna jaribu lililowapata ninyi lisilo kawaida ya wanadamu. Ila Mungu ni mwaminifu. Hatawaacha mjaribiwe kupita uwezo wenu. Pamoja na jaribu yeye atawapa mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.1 Kor 1:9
Mungu ni mwaminifu ambaye aliwaita ninyi katika ushirika wa mwana wake, Yesu Kristo Bwana wetu.Zab 91:4
Yeye atakufunika kwa mbawa zake, na chini ya mbawa zake utapata kimbilio. Uaminifu wake ni ngao na ulinzi.Zab 36:5
Uaminifu wa agano lako, Yahwe, unafika mbinguni; uaminifu wako unafika mawinguni.1 Pet 4:19
Kwa hiyo wote wanaoteseka kutokana na mapenzi ya Mungu wakabidhi nafsi zao kwa Muumba mwaminifu ili hali wakitenda mema.1 The 5:24
Yeye aliyewaita ni mwaminifu, naye ndiye mwenye kutenda.Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0