Mwanzo › Biblia inasema nini › Imani
Imani
Biblia inasema nini kuhusu Imani
Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.
Lk 18:27
Yesu akajibu, 'Mambo yasiyowezekana kwa mwanadamu kwa Mungu yanawezekana.”Rum 10:17
Hivyo imani huja kutokana na kusikia, na kusikia kwa neno la Kristo.Ebr 11:6
Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa kuwa ajaye kwa Mungu lazima aamini kwamba Mungu anaishi na kwamba huwapatia zawadi wale wamtafutao.Mt 21:22
Chochote mtakachoomba kwa sala, huku mkiamini, mtapokea.”Ebr 11:1
Sasa imani ni hakika aliyo nayo mtu wakati atarajiapo kitu fulani kwa ujasiri. Ni hakika ya kitu ambacho bado hakijaonekana.Mt 21:21
Yesu akajibu na kuwaambia, “Kweli nawaambieni, kama mkiwa na imani na bila wasiwasi, hamtafanya kile kilichofanyika kwa huo mtini tu, lakini mtauambia hata huo mlima, ' uchukuliwe na ukatupwe baharini, 'na itafanyika.Mk 11:22–24
Yesu aliwajibu, “Muwe na imani katika Mungu. Amini nawaambia kwamba kila auambiaye mlima huu, 'Ondoka, na ukajitupe mwenyewe baharini, 'na kama hana mashaka moyoni mwake lakini anaamini kwamba alichokisema kitatokea, hivyo ndivyo Mungu atakavyofanya. Kwa hiyo ninawaambia: kila kitu muombacho na kuuliza kwa ajili yake, aminini kwamba mmepokea, navyo vitakuwa vyenu.2 Kor 5:7
Kwa kuwa tunatembea kwa imani, sio kwa kuona. Kwa hiyo tunaujasiri.Mit 3:5–6
Mtegemee Yehova kwa moyo wako wote na wala usitegemee ufahamu wako mwenyewe, katika njia zako zote mkiri Yeye na yeye atayanyosha mapito yako.Lk 1:37
Maana hakuna lisilowezekana kwa Mungu.”Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.
Vyanzo
Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0
Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0