Bible Explorer

Mwanzo › Biblia inasema nini › Ahadi za Mungu

Imani

Biblia inasema nini kuhusu Ahadi za Mungu

Aya ambazo wasomaji hurejea mara nyingi zaidi kwa mada hii (10), zimenukuliwa kikamilifu kutoka Swahili Unlocked Literal Bible.

2 Pet 3:9Si kwamba Bwana anafanya pole pole kutimiza ahadi, kama inavyofikiriwa kuwa, Lakini yeye ni mvumilivu kwa ajili yenu, yeye hatamani hata mmoja aangamie, Lakini hutamani kutoa muda ili wote wapate kutubu.
2 Pet 1:4Kwa njia hii alitutumainishia ahadi kuu za thamani. Alifanya hili ili kutufanya warith wa asili ya Mungu, kwa kadiri tunavyoendelea kuuacha uovu wa dunia hii.
1 Kor 10:13Hakuna jaribu lililowapata ninyi lisilo kawaida ya wanadamu. Ila Mungu ni mwaminifu. Hatawaacha mjaribiwe kupita uwezo wenu. Pamoja na jaribu yeye atawapa mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
Flp 4:19Kwa ajili hiyo, Mungu wangu atawajazeni mahitaji yenu kwa utajiri wa utukufu wake katikaYesu Kristo.
2 Kor 1:20Kwa kuwa ahadi zote za Mungu ni “Ndiyo” katika yeye. Hivyo pia kupitia yeye tunasema “Amina” kwa utukufu wa Mungu.
1 Yoh 1:9Lakini tukizitubu dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na haki kutusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.
Ebr 10:23Basi na tushikilie kwa uthabiti katika ungamo la ujasiri wa tumaini letu, bila ya kugeuka, kwa sababu Mungu aliyeahidi ni mwaminifu.
Rum 6:23Kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti, bali zawadi ya bure ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Ebr 6:13Kwa maana Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa nafsi yake, kwa kuwa asingeliapa kwa mwingine yeyote aliye mkubwa kuliko yeye.
Kum 31:6Uwe hodari na mwenye ujasiri mwema, usiogope, na usiwaogope; kwa maana Yahwe Mungu wako, ni yeye aendaye kabla yako; hatakuangusha wala kukuacha.”

Hii ni mistari ambayo wasomaji huirudia mara nyingi kwa mada hii — si fundisho juu yake. Soma kila mmoja katika sura yake.

Vyanzo

Aya za kila mada na mpangilio wake: data za mada za OpenBible.info, kwa kura za wasomaji: OpenBible.info · CC BY 4.0

Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0