Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Mathayo 5:44
Mstari wa Biblia · ULB
Mathayo 5:44
Lakini nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanao waudhi,
Katika muktadha
41Na yeyote akulazimishaye kwenda naye maili moja, nenda naye maili mbili.
42Kwa yeyote akuombaye mpatie, na usimwepuke yeyote anayehitaji kukukopa.
43Mmesikia imenenwa, 'Umpende jirani yako, na umchukie adui yako.'
44Lakini nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanao waudhi,
45Ili kwamba muwe watoto wa baba yenu aliye mbinguni. Kwa kuwa anafanya jua liwaangazie wabaya na wema, na anawanyeshea mvua waovu na wema.
46Kama mkiwapenda wanaowapenda ninyi, mwapata thawabu gani? Kwani watoza ushuru hawafanyi hivyo?
47Na kama mkiwasalimia ndugu zenu tu mwapata nini zaidi ya wengine? Je!, Watu wa mataifa hawafanyi vivyo hivyo?
Kwa Kiingereza
But I tell you, love your enemies and pray for those who persecute you,Marejeo mtambuka
Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.
Watakieni baraka wote wanaowatesa ninyi; muwabariki na wala msiwalaani.Msilipe ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi. Kinyume chake, mwendelee kubariki, kwa sababu hii mliitwa, ili kwamba muweze kurithi baraka.Lakini nasema kwenu ninyi mnaonisikiliza, wapendeni adui zenu na kufanya mema kwa wanao wachukieni. Wabarikini wale wanao walaani ninyi na waombeeni wale wanaowaonea.“Lakini ikiwa adui yako ana njaa, mlishe. Akiwa na kiu, mnyweshe. Kwa maana ukifanya hivyo, utampalia makaa ya moto juu ya kichwa chake.” Usishindwe na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema.Kama adui yako ana njaa, mpe chakula ale na kama ana kiu, mpe maji ya kunywa, maana utamwekea mkaa juu ya kichwa chake na Yehova atakupa thawabu.Yesu alisema, “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. “Nao wakapiga kura, kugawa mavazi yake.Wakati yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano, alipoteseka, hakutisha bali alijitoa mwenyewe kwake Yeye ahukumuye kwa haki.Akapiga magoti na kuita kwa sauti kubwa, “Bwana, usiwahesabie dhambi hii. “Aliposema haya, akakata roho.Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki