Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Yakobo 1:5
Mstari wa Biblia · ULB
Yakobo 1:5
Lakini kama mtu kati yenu anahitaji hekima, aiombe kutoka kwa Mungu, ambaye hutoa kwa ukarimu na pasipo kukemea kwa wote wamwombao, na atawapa hekima.
Katika muktadha
2Hesabuni kuwa ni furaha zaidi, ndugu zangu, mnapopita katika matatizo mbali mbali,
3mkijua kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huwapa uvumilivu.
4Acheni uvumilivu uikamilishe kazi yake, kwamba muweze kukomaa kikamilifu, bila kupungukiwa katika lolote.
5Lakini kama mtu kati yenu anahitaji hekima, aiombe kutoka kwa Mungu, ambaye hutoa kwa ukarimu na pasipo kukemea kwa wote wamwombao, na atawapa hekima.
6Lakini omba kwa imani, bila shaka, kwa kuwa mwenye kutia shaka ni kama mawimbi katika bahari, huchukuliwa na upepo na kutupwa huku na huko.
7Kwa hakika mtu huyu asifikirie kwamba atapokelewa ombi lake kutoka kwa Bwana;
8mtu huyu ana nia mbili, si imara katika njia zake zote.
Kwa Kiingereza
Now if any of you lacks wisdom, he should ask God, who gives generously to all without finding fault, and it will be given to him.Marejeo mtambuka
Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.
kama utalilia ufahamu na kupaza sauti yako kwa ajili ya ufahamu, kama utautafuta kama fedha na kupekua ufahamu kama unatafuta hazina iliyojificha, ndipo utakapofahamu hofu ya Yehova na utapata maarifa ya Mungu. Kwa kuwa Yohova hutoa hekima, katika kinywa chake hutoka maarifa na ufahamu.Ikiwa mtadumu ndani yangu, na kama maneno yangu yakidumu ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtafanyiwa.Kisha mtaniita, na kwenda na kuniomba mimi, na nitawasikiliza. Kwa maana mtanitafuta na kunipata, kwa kuwa mtanitafuta kwa moyo wenu wote.Mtegemee Yehova kwa moyo wako wote na wala usitegemee ufahamu wako mwenyewe, katika njia zako zote mkiri Yeye na yeye atayanyosha mapito yako. Usiwe mwenye busara machoni pako mwenyewe; mche Yehova na jiepushe na uovu.Na huu ndio ujasiri tulionao mbele zake, kwamba kama tukiomba kitu chochote sawa sawa na mapenzi yake, hutusikia. Na kama tunajua kwamba hutusikia — chochote tumwombacho tunajua kwamba tunacho hicho tulichomwomba.Sasa nipe hekima na maarifa, ili niweze kuwaongoza watu hawa, maana ni nani anayeweza kuwaamua watu wako, ambao ni wengi sana kwa idadi?”Omba, nawe utapewa. Tafuta, nawe utapata. Bisha hodi, na wewe utafunguliwa. Kwa yeyote anayeomba, hupokea. Na kwa yeyote anayetafuta, hupata. Na kwa mtu ambaye anayebisha hodi, atafunguliwa. Au kuna mtu miongoni mwenu ambaye, ikiwa mtoto wake amemwomba kipande cha mkate atampa jiwe? Au ikiwa atamwomba samaki, na yeye atampa nyoka? Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, Je! Ni kiasi gani zaidi Baba aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wanao muomba yeye?Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, kisha kupenda amani, upole na ukarimu, yenye kujaa rehema na matunda mema, bila kupendelea watu fulani, na kweli.Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki