Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Wagalatia 5:22–23

Mstari wa Biblia · ULB

Wagalatia 5:22–23

22Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani,

23upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo.

Soma sura nzima: Wagalatia 5

Katika muktadha

19Sasa matendo ya mwili yanaonekana. Nayo ni uasherati, uchafu, ufisadi,

20ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, husuda, kuwaka hasira, ushindani, faraka, mgawanyiko wa madhehebu,

21wivu, ulevi, ulafi na mambo mengine kama haya. Nawaonya ninyi, kama nilivyowaonya mwanzoni, kwamba wale wanaofanya mambo kama hayo hawataurithi ufalme wa Mungu.

22Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani,

23upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo.

24Wale walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na shauku na tamaa zao mbaya.

25Kama tukiishi kwa Roho, pia tutembee kwa Roho.

26Tusiwe wa kujivuna, tusichokozane kila mmoja na mwenzake, wala tusioneane wivu.

Wagalatia 5

Kwa Kiingereza

Berean Standard BibleGalatians 5:22–23But the fruit of the Spirit is love, joy, peace, patience, kindness, goodness, faithfulness, gentleness, and self-control. Against such things there is no law.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Kol 3:12–17Kama wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, jivikeni utu wema, ukarimu, unyenyekevu, upole na uvumilivu. Chukulianeni ninyi kwa ninyi. Hurumianeni kila mtu na mwenzake. Kama mtu analalamiko dhidi ya mwingine, amsamehe kwa jinsi ilele ambayo Bwana alivyo wasamehe ninyi. Zaidi ya mambo haya yote, muwe na upendo, ambao ndio kigezo cha ukamilifu. Amani ya Kristo na iwaongoze mioyoni mwenu. Ilikuwa ni kwa ajili ya amani hii kwamba mliitiwa katika mwili mmoja. Iweni na shukrani. Na Neno la Kristo likae ndani yenu kwa utajiri. Kwa hekima yote, fundishaneni na kushauriana ninyi kwa ninyi kwa Zaburi, nyimbo, na nyimbo za rohoni. Imbeni kwa shukrani mioyo yenu kwa Mungu. Na chochote mfanyacho, katika maneno au katika matendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu. Mpeni shukrani Mungu baba kupitia Yeye.
1 Kor 13:4–7Upendo huvumilia na hufadhili. Upendo haujisifu au kujivuna. Hauna kiburi au ukorofi. Hautafuti mambo yake, hauoni uchungu haraka, wala hauhesabu mabaya. Haufurahii udhalimu. Badala yake, hufurahi katika kweli. Upendo huvumilia mambo yote; huamini mambo yote, una ujasiri katika mambo yote, na hustahimili mambo yote.
Yn 15:5Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi. Adumuye ndani yangu na mimi ndani yake, mtu huyu huzaa matunda mengi, kwa kuwa pasipo mimi hamuwezi kufanya jambo lolote.
Yak 3:17–18Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, kisha kupenda amani, upole na ukarimu, yenye kujaa rehema na matunda mema, bila kupendelea watu fulani, na kweli. Na tunda la haki hupandwa katika amani kwa wale ambao wanatenda mambo ya amani.
Yn 15:2Kila tawi ndani yangu ambalo halizai tunda, na husafisha kila tawi ambalo huzaa tunda huliondoa ili kwamba liweze kuzaa zaidi.
Efe 5:9Kwa kuwa matunda ya nuru yanajumuisha uzuri wote, haki na ukweli.
Zab 1:3Atakuwa kama mti uliopandwa karibu na mkondo wa maji ambao huzaa matunda yake kwa majira yake, ambao majani yake hayakauki; lolote afanyalo litafanikiwa.
Yn 15:16Hamkunichagua mimi, bali mimi niliwachagua ninyi na kuwaweka mwende mazae matunda, na tunda lenu lipate kukaa. Hii liko hivi ili kwamba chochote muombacho kwa Baba kwa jina langu, atawapeni.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki