Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 6 Juni
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 6 Juni 2027
Jumapili · Juma la 10 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Dominika ya 10 ya Mwaka
Dominika · Rangi ya liturujia: kijani
Masomo ya siku
Somo la kwanza
9Yahwe Mungu akamuita mwanaume na kumwambia, “ uko wapi?” 10Mwanaume akasema, “nilikusikia bustanini, na nkaogopa, kwa sababu nilikuwa uchi. kwa hiyo nikajificha.” 11Mungu akasema, “Ni nani alikwambia kuwa ulikuwa uchi? Je umekula kutoka mti ambao nilikuagiza usile matunda yake?” 12Mwanaume akasema, “ Mwanamke uliyenipa kuwa na mimi, alinipatia tunda kutoka kwenye mti, na nikala.” 13Yahwe Mungu akamwambia mwanamke, “ Nini hiki ulichofanya?” mwanamke akasema, “nyoka alinidanganya, na nikala.” 14Yahwe Mungu akamwambia nyoka, “ kwa sababu umefanya jambo hili, umelaaniwa wewe mwenyewe miongoni mwa wanyama wote wa kufugwa na wanyama wote wa mwituni. Itakuwa kwa tumbo lako utakwenda, na mavumbi utakula kwa siku zote za maisha yako. 15Nitaweka uadui kati yako na mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake. Atakujeruhi kichwa chako na utamjeruhi kisigino chake.”
Wimbo wa katikati
1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. Toka ndani yangu ninakulilia, Yahwe. 2Bwana, usikie sauti yangu; masikio yako na yasikie kwa makini kuomba kwangu kwa ajili ya huruma. 3Kama wewe, Yahwe, ungehesabu maovu, Bwana, ni nani angesimama? 4Lakini kwako kuna msamaha, ili uweze kuheshimiwa. 5Ninamngoja Yahwe, nafsi yangu inasubiri, na katika neno lake ninatumainia. 6Nafsi yangu inamngoja Bwana kuliko mlinzi aingojavyo asubuhi. 7Israeli, umtumainie yahwe. Yahwe ni wenye huruma, na yuko tayari kusamehe. 8Ni yeye ambaye ataikomboa istaeli dhidi ya dhambi zake zote.
Somo la pili
13Lakini tuna roho ileile ya imani kulingana na kile kilicho andikwa: “Niliamini, na hivyo nilinena.” Sisi pia tunaamini, na hivyo pia tunanena. 14Tunajua kuwa yule aliye mfufua Bwana Yesu pia atatufufua sisi pamoja naye. Tunajua kuwa atatuleta sisi pamoja nanyi katika uwepo wake. 15Kila kitu ni kwa ajili yenu ili kwamba, kwa kadri neema inavyo enea kwa watu wengi, shukurani zizidi kuongezeka kwa utukufu wa Mungu. 16Hivyo hatukati tamaa. Japokuwa kwa nje tunachakaa, kwa ndani tunafanywa upya siku hadi siku. 17Kwa kipindi hiki kifupi, mateso haya mepesi yanatuandaa sisi kwa ajili ya umilele mzito wa utukufu uzidio vipimo vyote. 18Kwa kuwa hatutazami kwa ajili ya vitu ambavyo vinaonekana, bali kwa ajili ya vitu visivyoonekana. Vitu tunavyoweza kuviona ni vya muda tu, bali vitu ambayo havionekani ni vya milele. 5:1Tunajua kwamba kama maskani ya ulimwenguni ambayo tunaishi humo yanaharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu. Ni nyumba isiyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu, bali ni nyumba ya milele, katika mbingu.
Injili
20Kisha alienda nyumbani, na umati wa watu wakaja pamoja tena, hata wasiweze kula hata mkate. 21Familia yake waliposikia habari hiyo, walienda kumkamata, kwani walisema, “ Amerukwa na akili”. 22Waandishi waliokuja kutoka Yerusalemu walisema, “ Amepagawa na Beelzebuli,” na, “ Kwa mtawala wa mapepo anatoa mapepo”. 23Yesu aliwaita kwake na kusema nao kwa mifano, “ Jinsi gani Shetani aweza kumtoa Shetani? 24Kama ufalme ukigawanyika wenyewe, ufalme huo hauwezi kusimama. 25Kama nyumba ikigawanyika yenyewe, nyumba hiyo haiwezi kusimama. 26Kama Shetani atainuka kinyume chake mwenyewe na kugawanyika, hawezi kusimama, na atakuwa amefika mwisho wake. 27Lakini hakuna hata mmoja awezaye kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuiba vitu vyake bila kumfunga mwenye nguvu kwanza, na kisha kukusanya kilichomo nyumbani. 28Kweli nawambieni, dhambi zote za wana wa watu zitasamehewa, pamoja na kufuru ambazo wanatamka, 29lakini yeyote atakaye mkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, bali ana hatia ya dhambi ya milele”. 30Yesu alilisema hili kwa sababu walikuwa wakisema, “Ana roho chafu”. 31Kisha mama yake na ndugu zake walikuja na kusimama nje. Wakamtuma mtu, kumwita. 32Na umati wa watu uliokuwa umekaa karibu naye wakamwambia, “mama yako na ndugu zako wako nje, na wanakutafuta wewe”. 33Aliwajibu, “Ni nani mama yangu na ndugu zangu?” 34Aliwaangalia waliokuwa wamekaa wamemzunguka, na akasema, “Tazama, hawa ni mama zangu na ndugu zangu! 35Yeyote afanyaye mapenzi ya Mungu, mtu huyo ni ndugu yangu, na dada yangu, na mama yangu”.
Watakatifu wa siku
- Mt. Norberti, askofu
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki