Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 7 Juni

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 7 Juni 2027

Jumatatu · Juma la 10 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatatu ya Juma la 10 la Mwaka

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani

Masomo ya siku

Somo la kwanza

2 Kor 1:1–7

1Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, na kwa waumini wote walioko katika mkoa wote wa Akaya. 2Neema na iwe kwenu na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo. 3Na asifiwe Mungu na Baba wa Bwana Yesu Kristo. Yeye ni Baba wa rehema na Mungu wa faraja yote. 4Mungu hutufariji sisi katika mateso yetu yote, ili kwamba tuweze kuwafariji wale walio katika mateso. Tunawafariji wengine kwa faraja ileile ambayo Mungu alitumia kutufariji sisi. 5Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo huongezeka kwa ajili yetu, vile vile faraja yetu huongezeka kupitia Kristo. 6Lakini kama tunataabishwa, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu. Na kama tunafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu. Faraja yenu inafanya kazi kikamilifu mnaposhiriki mateso kwa uvumilivu kama sisi pia tunavyoteseka. 7Na ujasiri wetu juu yenu ni thabiti. Tunajua kwamba kama vile ambavyo mnashiriki mateso, vile vile mnashiriki faraja.

Wimbo wa katikati

Zab 34:1–8

1Zaburi ya Daudi; wakati alipojifanya kuwa mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimtoa yeye nje. Nitamsifu Yahwe wakati wote, siku zote sifa zake zitakuwa mdomoni mwangu. 2Nitamsifu Yahwe! walio onewa wasikie na kufurahi. 3Msifuni Yahwe pamoja nami, kwa pamoja tuliinue jina lake. 4Nilimuomba Yahwe msaada naye akanijibu, akanipa ushindi juu ya hofu yangu yote. 5Wale wanao mtazama yeye wana furaha, na nyuso zao hazina aibu. 6Huyu mtu aliye onewa alilia na Yahwe akamsikia na kumuokoa kwenye matatizo yake yote. 7Malaika wa Yahwe huweka kambi wakiwazunguka wale wanao muogopa yeye na kuwaokoa. 8Onjeni muone Yahwe ni mzuri. Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe ni kimbilio lake.

Injili

Mt 5:1–12

1Yesu alipo uona umati, akaondoka na kuelekea Mlimani. Alipokuwa ameketi chini, wanafunzi wake wakaja kwake. 2Akafunua kinywa chake na akawafundisha, akisema, 3“Heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao. 4Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa. 5Heri wenye upole, maana watairithi nchi. 6Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa. 7Heri wenye rehema maana hao watapata Rehema. 8Heri wenye moyo safi maana watamwona Mungu. 9Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu. 10Heri wale wanaoteswa kwa ajili ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao. 11Heri ninyi ambao watu watawatukana na kuwatesa, au kusema kila aina ya ubaya dhidi yenu kwa uongo kwa ajili yangu. 12Furahini na kushangilia, maana thawabu yenu ni kubwa juu mbinguni. Kwa kuwa hivi ndivyo watu walivyo watesa manabii walioishi kabla yenu.

Watakatifu wa 7 Juni

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki