Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 17 Mei

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 17 Mei 2027

Jumatatu · Juma la 7 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatatu ya Juma la 7 la Mwaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe

Bikira Maria, Mama wa Kanisa · Kumbukumbu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mwa 3:9–15, 20

au: Mdo 1:12–14

9Yahwe Mungu akamuita mwanaume na kumwambia, “ uko wapi?” 10Mwanaume akasema, “nilikusikia bustanini, na nkaogopa, kwa sababu nilikuwa uchi. kwa hiyo nikajificha.” 11Mungu akasema, “Ni nani alikwambia kuwa ulikuwa uchi? Je umekula kutoka mti ambao nilikuagiza usile matunda yake?” 12Mwanaume akasema, “ Mwanamke uliyenipa kuwa na mimi, alinipatia tunda kutoka kwenye mti, na nikala.” 13Yahwe Mungu akamwambia mwanamke, “ Nini hiki ulichofanya?” mwanamke akasema, “nyoka alinidanganya, na nikala.” 14Yahwe Mungu akamwambia nyoka, “ kwa sababu umefanya jambo hili, umelaaniwa wewe mwenyewe miongoni mwa wanyama wote wa kufugwa na wanyama wote wa mwituni. Itakuwa kwa tumbo lako utakwenda, na mavumbi utakula kwa siku zote za maisha yako. 15Nitaweka uadui kati yako na mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake. Atakujeruhi kichwa chako na utamjeruhi kisigino chake.” 20Mwanaume akaita mke wake jina Hawa kwa sababu alikuwa mama wa wote wenye uhai.

Wimbo wa katikati

Zab 87:1–3, 5–7

1Zaburi ya wana wa Kora; wimbo. Mji aliouanzisha umesimama juu ya mlima mtakatifu; 2Yahwe anapenda zaidi malango ya Sayuni kuliko mahema yote ya Yakobo. 3Mambo matukufu yamesemwa kwako, mji wa Mungu. Selah 5Itasemwa juu ya Sayuni, “Kila mmoja wa hawa alizaliwa katika yeye; na yeye Aliye Juu atamuimarisha. 6Yahwe anaandika katika kitabau cha sensa ya mataifa, “Huyu alizaliwa humo.” Selah 7Hivyo waimbaji na wachezaji kwa pamoja waseme, “chemchem zangu zimo kwako.”

Injili

Yn 19:25–27

25Askari walifanya mambo haya. Mama yake Yesu, dada wa mama yake, Mariamu mke wa Kleopa na Mariamu Magdalena - wanawake hawa walikuwa wamesimama karibu na msalaba wa Yesu. 26Yesu alipomwona mama yake pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wakisimama karibu, akamwambia mama yake, “Mwanamke, tazama, ona mwanao huyu hapa!” 27Kisha akamwambia yule mwanfunzi, “Tazama, huyu hapa mama yako. “Tokea saa hiyo yule mwanafunzi akamchukua kwenda nyumbani kwake.

Watakatifu wa 17 Mei

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki