Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 29 Machi
Kalenda ya Kiorthodoksi · 16 Machi (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 29 Machi 2027
Jumatatu · Wiki ya 3 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 2
Sikukuu na watakatifu
Mfiadini Sabino (287)
Kwaresima Kuu
Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Saa ya 6
13Yahwe wa majeshi ambaye mtakaye muheshimu kama mtakatifu; yeye ndie mtakayemuogopa na yeye ndiye mtakayemuhofia. 14mtakatifu; lakinia takuwa kama jiwe la kikwazo na mwamba wa kujikwaza kwa nyumba zote za Israeli. Na atakuwa mtego na mtego kwa watu wake Yerusalemu. 15Wengi watajikwaa juu yao na kuanguka na kuvunjika, na kutekwa na kukamata mateka. 16Ufunge huo ushuhuda, tia muhuri, na uwape wafuasi wangu, 17Nitamsubiri Yahwe, afichaye uso wake kutoka nyumba ya Yakobo; Nitamsubiri yeye. 18Ona, Mimi na watoto ambaye Yahwe amenipa mimi ni ishara na maajabu tu katika Israeli kutoka kwa Yahwe wa Majeshi yeye aishiye mlima wa Sayuni. 19Watakuambia wewe, ''tafuta habari kwa watu wenye pepo na wachawi'', walio kama ndege na kunong'ona dua. Lakini hawataacha kutafuta habari kwa Mungu wao? Je waenende kwa watu waliokufa badala ya walio hai? 20Kwa sheria na kwa ushuhuda! kama hawatayasema mambo hayo ni kwa sababu hakuna mwanga wa alfajiri. 21Nawatapita katikati ya nchi kwa shida kubwa na njaa. Walipokuwa na njaa, walipatwa na hasira na kumlaani mfalme wao na Mungu wao, na wakajeuza macho yao juu. 22Wataiangalia nchi na kuona dhiki, giza, na ukandamizaji wa viza. Watapelekwa kwenye nchi ya giza. 9:1Viza itaondolewa kwa yeyote ambaye yuko kwenye dhiki. Katika kipindi cha awali aliifedhehesha nchi ya Zebuluni na nchi ya Naftali, lakini kipindi cha baadae ataifanya itukuke, njia ya kuelekea baharini, mbele ya Yordani na mataifa ya Galilaya. 2Watu wanotembeakatika giza wameona wameona mwanga mkubwa; wale waishio katika nchi ya uvuli wa mauti, mwanga umewaka juu yao. 3Umeliongeza taifa; umeongeza furaha yao. Wamefurahia mbele yako kama furaha ya kipindi cha mavuno, kama watu wanavyofurahi kugawanya nyara. 4Maana nira ya mzigo wake, boriti katika mabega yake, fimbo ya mkandamizaji, umesambaratisha ndoto kama siku ya Midiamu. 5Kila buti likanyagalo gasia na vazi limekwisha kwenye damu itachomwa, mafuta kwa moto. 6Kwetu mtoto amezaliwa, kwetu mtoto ametoka; na mtawala atakuwa kwenye mabega yake; na jina lake ataitwa mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa Amani. 7Enzi yake na amani yake haitakuwa na mwisho, maana anatawala katika kiti cha enzi cha Daudi, na juu ya ufalme wake, ataanzisha hukumu ya haki, tangu sasa na hata milele. Bidii ya Yahwenwa majeshi itafanya haya.
Sala ya Jioni: somo
9Kulikuwa na matukio kumuhusu Nuhu. Nuhu alikuwa mtu mwenye haki, na asiye na lawama miongoni mwa watu wa kipindi chake. Nuhu alitembea na Mungu. 10Nuhu akafanyika baba wa wana watatu wa kiume: Shem, Ham na Yafeti. 11Nchi iliharibika mbele za Mungu, na ikajaa ghasia. 12Mungu akaiona nchi; tazama, ilikuwa imeharibika, kwa kuwa wote wenye mwili walikuwa wameharibu njia zao juu ya nchi. 13Mungu akamwambia Nuhu, “Nimeona kuwa sasa niwakati wa mwisho kwa wote wenye mwili, kwa kuwa inchi imejaa ghasia kutokana na wao. Hakika, nitawaharibu wao pamoja na nchi. 14Tengeneza safina ya mti wa mvinje kwa ajili yako. Tengeneza vyumba katika safina, na vifunike kwa lami ndani na nje. 15Hivi ndivyo utakavyofanya: urefu wa safina dhiraa miatatu, upana wake dhiraa hamsini, kwenda juu kwake dhiraa thelathini. 16Tengeneza paa la safina, na ulimalize kwa kipimo cha dhiraa kutoka juu ubavuni. Weka mlango katika ubavu wa safina na utengeneze dari ya chini, ya pili na ya tatu. 17Sikiliza, nimekaribia kuleta gharika ya maji juu ya nchi, kuharibu wenye mwili wote wakaao ndani ya nchi wenye pumzi ya uhai chini ya mbingu. Kila kitu kilichopo juu ya nchi kitakufa. 18Lakini nitalifanya thabiti agano langu na wewe. Utaingia ndani ya safina, wewe, na wana wako wa kiume, na mke wako, pamoja na wake za wanao. 19Kwa kila kiumbe hai chenye mwili, viwili vya kila aina utavileta ndani ya safina, ili visalie hai pamoja nawe, vya kike na vya kiume. 20Katika ndege kwa jinsi yake, na wanyama wakubwa kwa jinsi yake, kila kitambaacho ardhini kwa jinsi yake, viwili viwili vya kila aina vitakuja kwako ili viwe salama. 21Kusanya kila aina ya chakula kinacholiwa kwa ajili yako na ukitunze, ili kwamba viwe chakula chako na chao.” 22Kwa hiyo Nuhu akafanya hivi. kulingana na yote ambayo Mungu alimuagiza, ndivyo alifanya.
Sala ya Jioni: somo
1Je hekima haiti? Je ufahamu hapazi sauti yake? 2Juu ya kilima kando ya barabara, kwenye njia panda, hekima anasimama. 3Kando ya njia ya kuingilia mjini, karibu na milango ya mji, anaita kwa sauti. 4Watu, ninawaita ninyi na ninapaza sauti yangu kwa wana wa wanadamu. 5Ninyi wajinga, jifunzeni hekima, na ninyi mnaochukia maarifa, lazima mjipatieni moyo wa ufahamu. 6Sikiliza na mimi nitasema mambo mazuri na nifumbuapo midomo yangu nitaongea haki. 7Maana kinywa changu hunena uaminifu na midomo yangu huchukia uovu. 8Maneno ya kinywa changu yote ni haki; hakuna kilichogeuzwa wala kupotoshwa. 9Maneno yangu yote yamenyooka kwa yule mwenye kuelewa; maneno yangu ni haki kwa wale wanaotafuta maarifa. 10Chagua fundisho langu badala ya fedha na maarifa kuliko dhahabu safi. 11Maana mimi, hekima ni bora kuliko vito; hakuna unachokitamani kinaweza kulinganishwa na mimi. 12Mimi, hekima, naishi kwa utaratibu, na ninamiliki maarifa na busara. 13Hofu ya Mungu ni kuchukia uovu- nachukia majivuno na kiburi, njia ya uovu, na kauli iliyopotoka- hivyo ninavichukia. 14Ninaushauri mzuri na hekima sahihi; mimi ni busara; nguvu zipo kwangu. 15Kwa njia yangu wafalme hutawala- pia na waungwana, na wote ambao hutawala kwa haki. 16Kwa njia yangu wafalme hutawala na waungwana na wote wanaotawala kwa haki. 17Nawapenda wale wanaonipenda, na wale wanaonitafuta kwa bidii, wataniona. 18Kwangu kunautajiri na heshima, utajiri wa kudumu na haki. 19Tunda langu ni bora kuliko dhahabu, bora hata kuliko dhahabu safi. 20Ninazalisha kilicho bora kuliko fedha safi. Natembea katika njia ya haki, 21katika mapito ambayo huelekea kwenye haki, ili niwape urithi wale wanaonipenda na kuzijaza hazina zao.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini Papa (305-311)
- Mtume Aristobulo, Askofu wa Britania (karne ya 1)
- Mfiadini wa Kikasisi Aleksanda, Papa wa Roma (119)
- Mfiadini Yuliani wa Anazarbo (karne ya 4)
- Askofu Mtakatifu Serapioni, Askofu Mkuu wa Novgorod (1516)
- Wafiadini wa Kikasisi Trofimo na Thalo, mapadri wa Laodikia (karibu 300)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 16 Machi katika kalenda ya kanisa ni 29 Machi katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki