Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 30 Machi
Kalenda ya Kiorthodoksi · 17 Machi (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 30 Machi 2027
Jumanne · Wiki ya 3 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 2
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Aleksi, mtu wa Mungu (411)
Kwaresima Kuu
Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Saa ya 6
9Watu wote watajua, Hata Samaria na wakazi wote wa Samaria, wanaongea kwa kiburi na moyo wenye kiburi, 10Matofali yameanguka, lakini tutajenga tena kwa jiwe la patasi; mkuyu umekatwa chini, lakini tutaotesha mierezi katika eneo lao. 11Hivyo basi Yahwe atamwinua juu yao Rezini, adui zake, atawakoroga adui zake, 12Waaramea upande wa mashariki, na wafilisti upande wa magharibi. Nao watamla Israeli kwa mdomo uliowazi. katika mambo yote haya hasira yake haijapungua; badala yake ameunyosha mkono wake nje. 13Lakini hawatageuka kwa yule anayewapiga wao, wala kumtafuta Yahwe wa majeshi. 14Hivyo basi yao atakata kichwa nakiwiwili cha Israeli, kuti na nyasi, katika siku moja. 15Viongozi na watu wenye vyeo na manabii wanaofundisha kuwa uongo ni mkia. 16Wale wanaowaongoza watu hawa wanawaongoza vibaya, na wale wanaongozwa wameangamia. 17Hivyo basi Bwana atafurahia juu ya vijana wadogo wala hatakuwa na huruma kwa yatima na wajane, maana kila mmoja hana Mungu na ni watenda dhambi, na kila mdomo unazungumza matendo mabaya. Mambo yote haya, hasira yake haijapungua; badala yake mkono wake umenyooka hata sasa. 18Matendo mabaya yataungua kama moto, moto hulao mbigili na miiba; itachoma hata vichaka vya mwitu, na safu ya moshi mkubwa upaa. 19Japo hasira ya Yahwe wa majeshi imeunguza, na watu ni kama mafuta kwenye moto. Hakuna mtu aliyemuacha ndugu yake. 20Watanyakuwa chakula katika mkono kulia lakini bado watasikia njaa; watakula chakula kwa mkono wa kushoto lakini hawataridhika. Kila mmoja atakula nyama ya mkono wake mwenyewe. 21Manase; kwa pamoja watavamia Yuda. Mambo yote haya, hasira yake haitapungua; badala yake, amenyoosha mkono wake hata sasa. 10:1Ole wao watimizao sheria zisizo za haki na waandikao sheria zisizo na haki. 2Wanawanyima wahitaji haki yao, wanawaibia watu wangu walio masikini haki zao, wajane mateka wao, na kuwafanya waliofiwa na baba zao mawindo yao! 3Hutafanya nini siku ya hukumu pale siku ya uaribifu itakapokuja kutoka mbali, utakimbilia msaada kwa nani? na utauacha utajiri wako wapi? 4Hakuna kitakachobaki, utaota miongoni mwa wafungwa au kuanguka miongoni mwa wauwaji. Katika mambo yote haya, hasira yake haijapungua; badala yake mkono wake ameunjoosha hata sasa.
Sala ya Jioni: somo
1Yahwe akamwambia Nuhu, “Njoo, wewe na nyumba yako wote, katika safina, kwa kuwa nimeona kuwa wewe ni mwenye haki mbele yangu katika kizazi hiki. 2Kwa kila mnyama aliye safi utakuja nao saba wa kiume na saba wa kike. Na kwa wanyama wasio safi, lete wawili wawili, wakiume na wakike. 3Pia na kwa ndege wa angani, lete saba wa kiume na saba wa kike, ili kuhifadhi kizazi chao juu ya uso wa nchi yote. 4Kwa kuwa ndani ya siku saba nitasababisha mvua kunyesha juu ya nchi muda wa siku arobaini mchana na usiku. Nitaharibu kila kiumbe hai nilichokiumba juu ya uso wa ardhi.” 5Nuhu alifanya yote ambayo Yahwe alimuagiza.
Sala ya Jioni: somo
32Na sasa, wanangu, nisikilizeni, maana wale wazishikao njia zangu watakuwa na furaha. 33Sikilizeni fundisho langu na mpate hekima; wala msilipuuze. 34Anisikilizaye atakuwa na furaha- kila siku akitazama katika malango yangu, akinisubiri pembeni mwa milango ya masikani yangu. 35Maana yeyote anionaye mimi, anapata uzima, naye atapata kibali kwa Yehova. 36Na yeyote asiyeniona mimi, hujiumiza mwenyewe, wote wanaonichukia hupenda mauti. 9:1Hekima amejenga nyumba yake; amechonga nguzo saba kutoka katika miamba. 2Ameandaa wanyama wake kwa chakula cha usiku; ameichanganya divai yake; na kuandaa meza yake. 3Amewatuma watumishi wake kupeleka mialiko na kutoka mahali pa juu sana kwenye mji anaita: 4“Wale wasiofunzwa waje hapa!” anawaambia wale wasionaufahamu. 5Njoo, ule chakula, na unywe divai nimeshaichanganya. 6Acheni njia zenu za kijinga, na mkaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu. 7Yeyote amrekebishaye mwenye dhihaka hukaribisha matusi na yeyote anayemshutumu mtu mbaya atapata madhara. 8Usimshutumu mwenye dhihaka, ama atakuchukia; mshutumu mtu mwenye busara, naye atakupenda. 9Mpe mafundisho mtu mwenye busara, naye atakuwa na busara zaidi; mfundishe mtu mwenye haki, naye ataongeza elimu. 10Hofu ya Mungu ni chanzo cha hekima na maarifa ya Mtakatifu ni ufahamu. 11Maana kwa njia yangu siku zako zitazidishwa na uzima wako utaongezewa miaka.
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Makario, abati wa Kalyazin, mtenda miujiza (1483)
- Mfiadini wa Kikasisi Aleksanda, padri (1919)
- Mfiadini wa Kikasisi Vikta, padri (1942)
- Mfiadini Marino
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 17 Machi katika kalenda ya kanisa ni 30 Machi katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki