Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 18 Machi
Kalenda ya Kiorthodoksi · 5 Machi (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 18 Machi 2027
Alhamisi · Wiki ya 1 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 8
Sikukuu na watakatifu
Mfiadini Kononi wa Isauria (karne ya 1)
Kwaresima Kuu
Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Saa ya 6
11Mtu anaye tazama kwa kujivuna atashushw chini, na kiburi cha watu kitashushwa chini, na Yahwe mwenyewe atainuliwa siku hiyo. 12Maana kutakuwa na siku ya Yahwe wa majeshi juu ya yeyote anayejigamba na kujiinua juu, na dhidi ya yeyote mwenye kiburi na atashushwa chini- 13na dhidi ya mierezi ya Lebanoni iliyo juu na kupandishwa juu, na dhidi ya mialoni ya Bashani. 14Siku hiyo ya Yahwe wa majeshi itakuwa dhidi ya milima yote mirefu, na dhidi ya vilima vyote vilivyonyanyuliwa juu, 15na dhidi ya minara mirefu, na dhidi ya kila ukutaunaojitokeza, 16na dhidi ya merikebu zote za Tarshishi, na dhidi ya vyombo vizuri vya meli. 17Kiburi cha mwanaume kitashushwa chini, na kiburi cha wanaume kitaanguka; Yahwe mwenyewe atainuliwa siku hiyo. 18Sanamu zote zitaondolewa. 19Wanaume wataingia kwenye mapango ya miamba na mashimo ya aridhi, kwa hofu ya Yahwe, na kwa utukufu wa enzi yake, atakapo nyanyuka na kuitisha nchi. 20Siku hiyo watu watatupa sanamu zao za fedha na dhahabu ambazo wametengeneza wenyewe kwa ajili ya kuabudia - watazitupa mbali kwa fuko na popo. 21Watu wataingia kwenye miamba kupitia mwanya itakuwa miamba chakavu, kwa hofu ya Yahwe na utukufu wa enzi yake,
Sala ya Jioni: somo
4Haya yalikuwa ni matukio yahusuyo mbingu na nchi, wakati vilipoumbwa, katika siku ambayo Yahwe Mungu aliumba nchi na mbingu. 5Hapakuwa na msitu wa shambani uliokuwa katika nchi, na hapakuwa na mmea wa shambani uliokuwa umechipuka, kwa kuwa Yahwe Mungu alikuwa hajasababisha mvua kunyesha juu ya nchi, na hapakuwa na mtu wa kulima ardhi. 6Lakini ukungu uliinuka juu kutoka kwenye nchi na kuutia maji uso wote wa ardhi. 7Yahwe Mungu aliumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, na akampulizia puani pumzi ya uhai, na mtu akawa kiumbe hai. 8Yahwe Mungu aliotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, na pale akamuweka mtu ambaye alimuumba. 9Kutoka ardhini Yahwe Mungu alifanya kila mti uote ambao unapendeza na ni mzuri kwa chakula. Hii ni pamoja na mti wa uzima ambao ulikuwa katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya. 10Mto ukatoka nje ya Edeni kuitia maji bustani. Na kutoka pale ukagawanyika na kuwa mito minne. 11Jina la ule wa kwanza ni Pishoni. Huu ni ule ambao unatiririka kupitia nchi yote ya Havila, ambapo kuna dhahabu. 12Dhahabu ya inchi ile ni nzuri. pia kuna bedola na jiwe shohamu. 13Jina la mto wa pili ni Gihoni. Huu unatiririka kupitia nchi yote ya kushi. 14Jina la mto wa tatu ni Hidekeli, ambao unatiririka mashariki mwa Ashuru. Mto wa nne ni Frati. 15Yahwe Mungu alimtwaa mtu na kumweka ndani ya bustani ya Edeni kuilima na kuitunza. 16Yahwe Mungu alimuagiza mtu akisema, “kutoka kwenye kila mti bustanini waweza kula kwa uhuru. 17Lakini kutoka kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa kuwa siku utakayo kula kutoka katika mti huo, utakufa hakika.” 18Kisha Yahwe Mungu akasema, “siyo jambo jema kwamba mtu huyu lazima awe pekeyake. Nitamfanyia msaidizi anaye mfaa.” 19Kutoka ardhini Yahwe Mungu akafanya kila mnyama wa kondeni na kila ndege wa angani. Kisha akawaleta kwa mtu huyu aone angewapatia majina gani. Jina ambalo mtu huyu alimwita kila kiumbe hai, hili ndilo lilikuwa jina lake.
Sala ya Jioni: somo
1Mwanangu, usizisahau amri zangu na uyatunze mafundisho yangu katika moyo wako, 2maana ziatakuongezea siku zako na miaka ya maisha yako na amani. 3Usiache utiifu wa agano na uaminifu viondoke kwako, vifunge katika shingo yako, viandike katika vibao vya moyo wako. 4Ndipo utapata kibali na heshima mbele Mungu na wanadamu. 5Mtegemee Yehova kwa moyo wako wote na wala usitegemee ufahamu wako mwenyewe, 6katika njia zako zote mkiri Yeye na yeye atayanyosha mapito yako. 7Usiwe mwenye busara machoni pako mwenyewe; mche Yehova na jiepushe na uovu. 8Itakuponya mwili wako na kukuburudisha mwili wako. 9Mheshimu Yehova kwa utajiri wako na kwa malimbuko ya mazao kwa kila unachozalisha, 10na ndipo ghala zako zitajaa na mapipa makubwa yatafurika kwa divai mpya. 11Mwanangu, usidharau kuadibishwa na Yohova na wala usichukie karipio lake, 12maana Yehova huwaadibisha wale wapendao, kama baba anavyoshughulika kwa mtoto wake ampendezaye. 13Yeye apataye hekima anafuraha, naye hupata ufahamu. 14Kwani katika hekima unapata manufaa kuliko ukibadilisha kwa fedha na faida yake inafaa zaidi kuliko dhahabu. 15Hekima inathamani zaidi kuliko kito, na hakuna unachokitamani kinaweza kulinganishwa na hekima. 16Yeye anasiku nyingi katika mkono wake wa kuume; na mkono wake wa kushoto ni utajiri na heshima. 17Njia zake ni njia za ukarimu na mapito yake ni amani. 18Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomshikilia, wale wanaomshikilia wanafuraha.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini wa Kikasisi Nikolao, padri (1919)
- Mfiadini wa Kikasisi Yohana, padri, na Watawa Wafiadini Mardari na Theofani (1938)
- Mfiadini Onesio (karne ya 1)
- Mfiadini Kononi, mtunza bustani (karne ya 3)
- Mtakatifu Mtawa Marko, mfungaji (karne ya 5)
- Mtakatifu Mtawa Hesikio, mfungaji (karibu 790)
- Kupatikana kwa masalia ya Wana wa Mfalme Waaminifu Theodoro wa Smolensk na wanawe Daudi na Konstantino, watenda miujiza wa Yaroslavl (1463)
- Mtawa Mfiadini Adriani wa Poshekhonye, wa Yaroslavl (1550)
- Mfiadini Iraida
- Mfiadini Eulogio wa Palestina
- Mfiadini Eulampio
- Ikoni ya Mama wa Mungu iitwayo “Malezi”
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 5 Machi katika kalenda ya kanisa ni 18 Machi katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki