Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 19 Machi

Kalenda ya Kiorthodoksi · 6 Machi (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 19 Machi 2027

Ijumaa · Wiki ya 1 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 8

Sikukuu na watakatifu

Wafiadini 42 wa Amorio: Konstantino, Aetio, Theofilo, Theodoro, Melisseno, Kalisto, Basoe na wengine pamoja nao (karibu 845)

Kwaresima Kuu

Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Saa ya 6

Isa 3:1–14

1Ona, Bwana, Yahwe wa majeshi, anakaribia kuwachukua kutoka Yerusalema na Yudawasaidizi na wafanyakazi: wasambazaji wote wa mikate, wasambazaji wote wa maji; 2mtu mwenye nguvu, shuja, hakimu, nabii, dalili za msomaji, na mzee; 3naodha wa hamsini, raia husika, mshauri, fundi mtarajiwa, na mchawi stadi. 4Nitamuweka kijana tu kama kiongozi wenu, kijana atawaongoza wao. 5Watu watanyanyasika, kila mmoja mmoja na kila mmoja na jirani yake; watoto watawatusi wazee, na mivutano itawapa changamoto waheshimiwa. 6Mwanaume atamshikilia ndugu yake katika nyumba ya baba yake na kusema, 'Unayo kanzu; uwe kiongozi wetu, na uharibifu huu uwe mikononi mwako. 7'Siku hiyo atapaza sauti na kusema, 'hautakuwa mganga; sina mkate wala mavazi. Hatanifanya kuwa kiongozi wa watu. 8Kwa maana Yerusalemu kuna mashaka, na Yuda imeanguka, kwa sababu mazungumzo yao na matendo yao yako kinyume na Yahwe, wanayapinga macho ya utukufu wake. 9Angalia nyuso zao zinashudia kinyume nao; na watasema dhambi zao kama Sodoma; hawatazificha, Ole wao! Maana wanakamilisha janga lao wenyewe. 10Mwambie mtu mwenye haki kwamba itakuwa vizuri, maana watakula matunda ya matendo yao. 11Ole kwa wakosaji! itakuwa vibaya kwa yeye, maana malipo ya mikono yake yatafanyika kwake pia. 12Watu wangu-watoto wangu wanawakandamiza, na wanawake wanawaongoza wao. Watu wangu, wale wanaowaongoza wanawaongoza vibaya na kuchanganya muelekeo wa nja yenu. 13Yahwe simama juu ya mashitaka; yeye amesimama kuwashaki watu. 14Yahwe atakuja na hukumu juu ya wazee na watu wao na viongozi wao: ''Umeharibu shamba; nyara kutoka kwa masikni ziko kwenye nyumba zako.

Sala ya Jioni: somo

Mwa 2:20–3:20

20Mtu huyu akawapatia majina wanyama wote, ndege wote wa angani, na kila mnyama wa mwitu. Lakini kwa mtu mwenyewe hapakuwa na msaidizi wa kumfaa yeye. 21Yahwe Mungu akaleta usingizi mzito kwa mtu huyu, kwa hiyo mtu huyu akalala. Yahwe Mungu akatwaa moja ya mbavu za mtu huyu na akapafunika pale alipo chukua ubavu. 22Kwa ubavu ambao Yahwe Mungu alichukua toka kwa mtu huyu, akafanya mwanamke na akamleta kwa mtu huyu. 23Mwanaume akasema, “kwa sasa, huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu. ataitwa 'mwanamke,' kwa sababu ametwaliwa katika mwanaume. 24Kwa hiyo mwanaume atawaacha baba yake na mama yake, ataungamanika na mke wake, na watakuwa mwili mmoja. 25Wote wawili walikuwa uchi, mwanaume na mke wake, lakini hawakuona aibu. 3:1Sasa nyoka alikuwa mwerevu kuliko myama mwingine yeyote wa kondeni ambaye Yahwe Mungu alikuwa amemuumba. Akamwambia mwanamke, “Je ni kweli Mungu amesema, 'Msile matunda kutoka kwenye mti wowote bustanini'?” 2Mwanamke akamwambia nyoka, “Twaweza kula tunda kutoka kwenye miti ya bustani, 3lakini kuhusu tunda la mti ambao uko katikati ya bustani, Mungu alisema, 'msile, wala msiuguse, vinginevyo mtakufa.'” 4Nyoka akamwambia mwanamke, “hakika hamtakufa. 5Kwasababu Mungu anajua kwamba siku mkila macho yenu yatafumbuliwa, na mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” 6Na mwanamke alipoona kuwa mti ni mzuri kwa chakula, na kuwa unapendeza macho, na kwamba mti ulitamanika kwa kumfanya mtu awe mwerevu, alichukua sehemu ya tunda na akala. Na sehemu yake pia akampatia mumewe aliyekuwa naye, naye akala. 7Macho ya wote wawili yalifumbuliwa, na wakajua kuwa wako uchi. Wakashona majani ya miti pamoja na wakatengeneza vya kujifunika wao wenyewe. 8Wakasikia sauti ya Yahwe Mungu akitembea bustanini majira ya kupoa kwa jua, kwa hiyo mwanaume na mke wake wakajificha wao wenyewe kwenye miti ya bustani kuepuka uwepo wa Yahwe Mungu. 9Yahwe Mungu akamuita mwanaume na kumwambia, “ uko wapi?” 10Mwanaume akasema, “nilikusikia bustanini, na nkaogopa, kwa sababu nilikuwa uchi. kwa hiyo nikajificha.” 11Mungu akasema, “Ni nani alikwambia kuwa ulikuwa uchi? Je umekula kutoka mti ambao nilikuagiza usile matunda yake?” 12Mwanaume akasema, “ Mwanamke uliyenipa kuwa na mimi, alinipatia tunda kutoka kwenye mti, na nikala.” 13Yahwe Mungu akamwambia mwanamke, “ Nini hiki ulichofanya?” mwanamke akasema, “nyoka alinidanganya, na nikala.” 14Yahwe Mungu akamwambia nyoka, “ kwa sababu umefanya jambo hili, umelaaniwa wewe mwenyewe miongoni mwa wanyama wote wa kufugwa na wanyama wote wa mwituni. Itakuwa kwa tumbo lako utakwenda, na mavumbi utakula kwa siku zote za maisha yako. 15Nitaweka uadui kati yako na mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake. Atakujeruhi kichwa chako na utamjeruhi kisigino chake.” 16Kwa mwanamke akasema, nitaongeza uchungu wakati wa kuzaa watoto; itakuwa katika maumivu utazaa watoto. Tamaa yako itakua kwa mume wako, lakini atakutawala.” 17Kwa Adam akasema, “kwa sababu umesikiliza sauti ya mke wako, na umekula kutoka katika mti, ambao nilikuagiza, nikisema, “ usile matunda yake', ardhi imelaaniwa kwa sababu yako; kupitia kazi yenye maumivu utakula matunda ya ardhi kwa siku zote za maisha yako. 18Ardhi itazaa miiba na mbigili kwa ajili yako, na utakula mimea ya shambani. 19Kwa jasho la uso wako utakula mkate, mpaka utakapo irudia ardhi, ambayo kwayo ulitwaliwa. kwa kuwa wewe ni mavumbi na kwenye mavumbi utarudi.” 20Mwanaume akaita mke wake jina Hawa kwa sababu alikuwa mama wa wote wenye uhai.

Sala ya Jioni: somo

Mit 3:19–34

19Kwa hekima Yehova aliweka msingi wa dunia, kwa ufahamu aliziimarisha mbingu. 20Kwa maarifa yake vina vilipasuka na mawingu kudondosha umande wake. 21Mwanangu, zingatia hukumu ya kweli na ufahamu, na wala usiache kuvitazama. 22Vitakuwa uzima wa nafsi yako na urembo wa hisani wa kuvaa shingoni mwako. 23Ndipo utatembea katika njia yako kwa usalama na mguu wako hautajikwaa; 24ulalapo hutaogopa; utakapolala, usingizi wako utakuwa mtamu. 25Usitishwe na hofu ya ghafula au uharibifu uliosababishwa na waovu unapotokea, 26kwa maana Yehova utakuwa upande wako na ataulinda mguu wako usinaswe kwenye mtego. 27Usizuie mema kwa wale wanaoyastahili, wakati utendaji upo ndani ya mamlaka yako. 28Jirani yako usimwambie, “Nenda, na uje tena, na kesho nitakupa,” wakati pesa unazo. 29Usiweke mpango wa kumdhuru jirani yako- anayeishi jirani nawe na yeye anakuamini. 30Usishindane na mtu pasipo sababu, ikiwa hajafanya chochote kukudhuru. 31Usimhusudu mtu jeuri au kuchagua njia zake zozote. 32Maana mtu mjanja ni chukizo kwa Yehova, bali humleta mtu mwaminifu kwenye tumaini lake. 33Laana ya Yehova ipo katika nyumba ya watu waovu, bali huibariki maskani ya watu wenye haki. 34Yeye huwadhihaki wenye dhihaka, bali huwapa hisani watu wanyenyekevu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 19 Machi

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 6 Machi katika kalenda ya kanisa ni 19 Machi katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki