Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 17 Machi

Kalenda ya Kiorthodoksi · 4 Machi (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 17 Machi 2027

Jumatano · Wiki ya 1 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 8

Sikukuu na watakatifu

Mtakatifu Mtawa Gerasimo wa Yordani (451)

Kwaresima Kuu

Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Saa ya 6

Isa 2:3–11

3Watu wengi watakuja na kusema, ''Njooni, twendeni juu ya mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo, kwa hiyo anaweza kutufundisha baadhi ya njia zake na tunaweza kutembea katika njia zake.'' Nje ya Sayuni itaenda sheria na neno la Yahwe litatoka Yerualemu. 4Atahukumu kati ya mataifa na atatoa maamuzi kwa watu wote; watayapiga nyungo mapanga yao kuwa majembe, na mikiku yao kama ya kukatia ndoano; taifa halitanyanyua upanga juu ya taifa lingine, na wala hawata jiandaa kwa vita tena. 5Nyumba ya Yakobo, njooni, na tutembee katika mwanga wa Yahwe. 6Kwa maana mmewatekeleza watu wenu, nyumba ya Yakobo, wamejazwa na desturi kutoka mashariki na dalili kutokea kama mfilisti, na watasalimiana kwa mikono na wana wa wageni. 7Nchi yao imejaa fedha na dhahabu, na hakuna mipaka katika utajiri wao; nchi yao pia imejaa farasi, wala hakuna mipika ya magari. 8Nchi yao pia imejaa sanamu; wanaabu utengenezaji wa mikono yao wenyewe, vitu aambavyo vidole vyao vimetengeneza. 9Watu watainama chini, na kila mmoja atanguka chini; hivyo basi msiwanyanyue juu. 10Nendeni maeneo yenye miamba na mjifiche kwenye aridhi kwa hofu ya Yahwe na kwa utukufu wa enzi yake. 11Mtu anaye tazama kwa kujivuna atashushw chini, na kiburi cha watu kitashushwa chini, na Yahwe mwenyewe atainuliwa siku hiyo.

Sala ya Jioni: somo

Mwa 1:24–2:3

24Mungu akasema, “ nchi na itoe viumbe hai, kila kiumbe kwa aina yake, mnyama wa kufugwa, vitu vitambaavyo, na wanyama wa nchi, kila kitu kwa jinsi yake.” Ikawa hivyo. 25Mungu akafanya wanyama wa nchi kwa aina yake, wanyama wa kufugwa kwa aina yake, na kila kitambaaho juu ya ardhi kwa aina yake. Akaona kuwani vyema. 26Mung akasema, “na tumfanye mtu katika mfano wetu, wa kufanana na sisi. Wawe na mamlaka juu ya samaki wa bahari, juu ya ndege wa angani, juu ya wanyama wa kufuga, juu ya nchi yote, na juu ya kila kitu kitambaacho kinacho tambaa juu ya nchi.” 27Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake. Katika mfano wake alimuumba. Mwanaume na mwanamke aliwaumba. 28Mungu akawabariki na akawaambia, “zaeni na kuongezeka. Jazeni nchi, na muitawale. Muwe na mamlaka juu ya samaki wa baharini, juu ya ndege wa angani, na juu ya kila kiumbe hai kiendacho juu ya nchi,” 29Mungu akasema, “tazama, nimewapeni kila mmea uzaao mbegu ambao uko juu ya nchi, na kila mti wenye tunda ambalo lina mbegu ndani yake. Vitakuwa ni chakula kwenu. 30Kwa kila mnyama wa nchi, kwa kila ndege wa angani, na kila kitambaacho juu ya nchi, na kila kiumbe ambacho kina pumzi ya uhai ni metoa kila mmea kwa ajili ya chakula.” ikawa hivyo. 31Mungu akaona kila kitu alichokiumba. Tazama, kikawa chema sana. Ikawa jioni na asubuhi siku ya sita. 2:1Kisha mbingu na nchi zilimalizika, na viumbe hai vyote vilivyo jaza mbingu na nchi. 2Siku ya saba Mungu alifikia mwisho wa kazi yake ambayo aliifanya, na kwa hiyo alipumzika siku ya saba kutoka kwenye kazi yake yote. 3Mungu akaibarikia siku ya saba na akaitakasa, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kwenye kazi yake yote ambayo aliifanya katika uumbaji.

Sala ya Jioni: somo

Mit 2:1–22

1Mwanangu, kama ukiyapokea maneno yangu na kuzitunza amri zangu, 2usikilize hekima na utaelekeza moyo wako katika ufahamu. 3kama utalilia ufahamu na kupaza sauti yako kwa ajili ya ufahamu, 4kama utautafuta kama fedha na kupekua ufahamu kama unatafuta hazina iliyojificha, 5ndipo utakapofahamu hofu ya Yehova na utapata maarifa ya Mungu. 6Kwa kuwa Yohova hutoa hekima, katika kinywa chake hutoka maarifa na ufahamu. 7Yeye huhifadhi sauti ya hekima kwa wale wampendezao, yeye ni ngao kwa wale waendao katika uadilifu, 8huongoza katika njia za haki na atalinda njia ya waaminifu kwake. 9Ndipo utakapoelewa wema, haki, usawa na kila njia njema. 10Maana hekima itaingia moyoni mwako na maarifa yataipendeza nafsi yako. 11Busara itakulinda, ufahamu utakuongoza. 12Vitakuokoa kutoka katika njia ya uovu, kutoka kwa wale waongeao mambo potovu. 13Ambao huziacha njia za wema na kutembea katika njia za giza. 14Hufurahia wanapotenda maovu na hupendezwa katika upotovu. 15Hufuata njia za udanganyifu na kwa kutumia ghilba huficha mapito yao. 16Busara na hekima zitakuokoa kutoka kwa mwanamke malaya, kutoka kwa mwanamke anayetafuta visa na mwenye maneno ya kubembeleza. 17Yeye humwacha mwenzi wa ujana wake na kusahau agano la Mungu wake. 18Maana nyumba yake huinama na kufa na mapito yake yatakupeleka kwa wale walioko kaburini. 19Wote waiendeao njia yake hawatarudi tena na wala hawataziona njia za uzima. 20kwa hiyo utatembea katika njia ya watu wema na kufuata njia za wale watendao mema. 21Kwa wale watendao mema watafanya makazi yao katika nchi, na wale wenye uadilifu watadumu katika nchi. 22Lakini waovu wataondolewa katika nchi na wale wasioamini wataondolewa katika nchi.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 17 Machi

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 4 Machi katika kalenda ya kanisa ni 17 Machi katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki