Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 18 Machi

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 18 Machi 2027

Alhamisi · Juma la 5 la Kwaresima

Sikukuu na watakatifu

Alhamisi ya Juma la 5 la Kwaresima

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: zambarau

Mt. Sirili wa Yerusalemu, askofu na mwalimu wa Kanisa · Ukumbusho

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mwa 17:3–9

3Abram akainama uso wake hadi chini ardhini na Mungu akazungumza naye, akisema, 4“Mimi, tazama, agano langu liko nawe. Utakuwa baba wa mataifa mengi. 5Wala jina lako halitakuwa tena Abram, bali jina lako litakuwa Abraham - kwa kuwa ninakuchagua kuwa baba wa mataifa mengi. 6Nitakufanya uwe na uzao mwingi zaidi, na nitakufanya mataifa, na wafalme watatoka kwako. 7Nitaimarisha agao langu kati yangu mimi na wewe na uzao wako baada yako, katika vizazi vyao vyote kwa agano la milele, nitakuwa Mungu kwako na kwa wazao wako baada yako. 8Nitakupa wewe, na wazao wako baada yako, nchi ambayo ulikuwa unaishi, nchi yote ya Kanaani, kuwa miliki ya milele, na nitakuwa Mungu wao.” 9Kisha Mungu akamwambia Abraham, “nawe lazima ulishike agano langu, wewe pamoja na uzao wako baada yako kwa vizazi vyao.

Wimbo wa katikati

Zab 105:4–9

4Mtafuteni Yahwe na nguvu zake; utafuteni uwepo wake siku zote. 5Kumbukeni mambo ya ajabu aliyoyatenda, 6miujiza yake na amri zitokazo kinywani mwake, enyi kizazi cha Ibrahimu mtumishi wake, enyi watu wa Yakobo, wachaguliwa wake. 7Yeye ni Yahwe, Mungu wetu. Amri zake ziko juu ya nchi yote. 8Naye hulikumbuka agano lake milele, neno alilo amuru kwa ajili ya vizazi elfu. 9Hulikumbuka agano alilolifanya na Ibrahimu na kiapo alicho mwapia Isaka.

Injili

Yn 8:51–59

51Amini, amini, nawaambia, iwapo yeyote atalishika neno langu, hataona mauti kamwe.” 52Wayahudi wakamwambia, “Sasa tumejua kuwa una pepo. Abrahamu na mabii walikufa; lakini unasema, 'Ikiwa mtu atalishika neno langu, hataonja mauti'. 53Wewe si mkuu kuliko baba yetu Abrahamu aliyekufa, sivyo? Manabii pia walikufa. Wewe wajifanya kuwa nani?” 54Yesu akajibu, “Ikiwa nitajitukuza mwenyewe, utukufu wangu ni bure; ni Baba yangu anayenitukuza - yule mnayemsema kuwa ni Mungu wenu. 55Ninyi hamjamjua yeye, lakini mimi namjua yeye. Ikiwa nitasema, 'simjui,' nitakuwa kama nyinyi, muongo. Hata hivyo, ninamjua na maneno yake nimeyashika. 56Baba yenu Abrahamu alishangilia atakavyoiona siku yangu; aliiona na alifurahi.” 57Wayahudi wakamwambia,”Haujafikisha umri wa miaka hamsini bado, nawe umemuona Ibrahimu?” 58Yesu akawaambia, “Amini, amini, nawaambia, kabla Abrahamu hajazaliwa, MIMI NIKO.” 59Ndipo waliokota mawe wapate kumpiga, lakini Yesu alijificha na akatoka nje ya hekalu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 18 Machi

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki