Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 16 Machi

Kalenda ya Kiorthodoksi · 3 Machi (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 16 Machi 2027

Jumanne · Wiki ya 1 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 8

Sikukuu na watakatifu

Wafiadini Eutropio, Kleoniko na Basilisko (karibu 308)

Kwaresima Kuu

Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Saa ya 6

Isa 1:19–2:3

19Kama utakubali na kutii, utakula mema ya nchi, 20lakini ukikataa na kugeuka, upanga utakuangamiza, maama Yahwe amesema. 21Ni kwa jinsi gani mji ulioaminika umekuwa kahaba! ulikuwa ni mij wenye usawa na haki, lakini sasa mji umejaa mauwaji. 22Fedha zenu zimechafuka, na mvinyo wenu umechanganjwa na maji. 23Viongozi wenu wamemgeuka Mungu wamekuwa marafiki wa wezi; yeyote anayopenda rushwa na kuikimbilia. Hawawajali yatima, wala wajane wanaokuja kuwanyenyekea mbele yao. 24Hivyo basi hili ndilo tamko la Bwana, Yahwe wa majeshi, Shujaa wa Israeli: Ole wao! nitachukua hatua kwa wale walio kinyume na mimi na niwaadhibu wale wanaonipinga; 25Nitaugeuza mkono wangu juu yako, nitatakasa chuma kilicho chakaa na kuondoa kutu yote. 26Nitailinda hukumu yako kama ilivyokuwa mwanzo, na washauri wako kama ilivyokuwa hapo mwanzo; baada ya hapo mtaitwa mji wa haki, mji wa imani.'' 27Sayuni itakombolewa kwa haki, na wanaotubu kwa haki. 28Waasi na wenye dhambi wataangamizwa pamoja, na wale wataenda kinyume na Yahwe watauliwa. 29Kwakukuwa utaona aibu juu ya miti ya mialoni uliyoitamani, na utakuwa na hofu juu ya bustani uliyoichagua. 30Kwa kukuwa utakuwa kama mualoni ambao majani yake yamenyauka, na kama bustani isiyokuwa na maji. 31Mtu mwenye nguvu atakuwa kama kitu kikavu, na kazi yake itakuwa kama cheche; zitawaka moto kwa pamoja, na hakuna hata mmoja ataweza kuuzima''. 2:1Vitu ambavyo Isaya mtoto Amozi alivijua katika maono, kuhusu Yuda na Yerusalemu. 2Na itakuwa katika siku za mwisho, ule mlima wa nyumba ya Yahwe itaanzishwa kama mlima mrefu zaidi, na utanyanyuliwa juu ya vilima, na mataifa yote yatakusanyika pale. 3Watu wengi watakuja na kusema, ''Njooni, twendeni juu ya mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo, kwa hiyo anaweza kutufundisha baadhi ya njia zake na tunaweza kutembea katika njia zake.'' Nje ya Sayuni itaenda sheria na neno la Yahwe litatoka Yerualemu.

Sala ya Jioni: somo

Mwa 1:14–23

14Mungu akasema, “kuwe na mianga katika anga kutenganisha mchana na usiku. Na ziwe kama ishara, kwa majira, kwa siku na miaka. 15Ziwe mianga katika anga ili kutoa mwanga juu ya nchi.” Ikawa hivyo. 16Mungu akafanya mianga mikuu miwili, mwanga mkuu zaidi kutawala mchana, na mwanga mdogo kutawala usiku. Akafanya nyota pia. 17Mungu akazipanga katika anga kutoa mwanga juu nchi, 18kutawala mchana na usiku, na kugawanya mwanga kutoka kwenye giza. Mungu akaona kuwa ni vyema. 19Ikawa jioni na asubuhi, siku ya nne. 20Mungu akasema, “maji yajae idadi kubwa ya viumbe hai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.” 21Mungu akaumba viumbe wakubwa wa baharini, pamoja na kila kiumbe hai cha aina yake, viumbe waendao na wanaojaa kila mahali majini, na kila ndege mwenye mabawa kwa aina yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. 22Mungu akavibariki, akisema, “zaeni na muongezeke, na mjae majini katika bahari. Ndege waongezeke juu nchi.” 23Ikawa jioni na asubuhi, siku ya tano.

Sala ya Jioni: somo

Mit 1:20–33

20Hekima inalia kwa sauti mtaani, inapaza sauti katika viwanja; 21katika mitaa inalia kwa sauti kuu, kwenye maingilio ya milango ya mji inasema “ 22Mpaka lini enyi wajinga mtapenda kuwa wajinga? Mpaka lini enyi wenye dhihaka mtapenda dhihaka, na hadi lini enyi wapumbavu, mtachukia maarifa? 23Zingatia karipio langu; nitatoa mawazo yangu kwa ajili yenu; nitawafahamisha maneno yangu. 24Nimeita, nanyi mkakataa kusikiliza; nimeunyosha mkono wangu, wala hakuna aliyezingatia. 25Lakini mumedharau mafundisho yangu yote na wala hamkuzingatia maelekezo yangu. 26Nitacheka katika taabu yenu, nitawadhihaki wakati wa kupatwa taabu- 27hofu ya kutisha itawapata kama tufani na maafa yatawakumba kama upepo wa kisulisuli, taabu na uchungu vitawapata. 28Halafu wataniita, nami sitawajibu; wataniita katika hali ya kukata tamaa lakini hawataniona. 29Kwa sababu wamechukia maarifa na hawakuchagua kuwa na hofu ya Yehova, 30hawakufuata mafundisho yangu na wakayadharau masahihisho yangu yote. 31Watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa kwa matunda ya hila zao wenyewe. 32kwa maana wajinga hufa wanaporudi nyuma, na kutojali kwa wapumbavu kutawaangamiza. 33Bali kila anisikilizaye ataishi kwa usalama na atapumzika salama pasipo hofu ya maafa.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 16 Machi

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 3 Machi katika kalenda ya kanisa ni 16 Machi katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki