Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 26 Februari
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 26 Februari 2027
Ijumaa · Juma la 2 la Kwaresima
Sikukuu na watakatifu
Ijumaa ya Juma la 2 la Kwaresima
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: zambarau
Kufunga na toba
Kujinyima nyama
Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.
Masomo ya siku
Somo la kwanza
3Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote kwa sababu alikuwa mwana wa uzee wake. Akamshonea vazi zuri. 4Ndugu zake wakaona kwamba baba yao alimpenda sana kuliko ndugu zake wote. Wakamchukia na hawakuongea naye vema. 12Ndugu zake wakaenda kulichunga kundi la baba yao huko Shekemu. 13Israeli akamwambia Yusufu, 'Je ndugu zako hawalichungi kundi huko Shekemu? Njoo, nami nitakutuma kwao.” Yusufu akamwambia, “nipo tayari.” 17Yule mtu akasema, “Waliondoka mahali hapa, kwa maana niliwasikia wakisema, 'Haya twende Dothani.” Yusufu akawafuata ndugu zake na kuwaona huko Dothani. 18Wakamwona kutokea mbali, na kabla hajawakaribia, wakapanga njama ya kumwua. 19Ndugu zake wakaambiana wao kwa wao, “Tazama, mwotaji anakaribia. 20Njoni sasa, na tumwue na kumtupa katika mojawapo ya mashimo haya. Nasi tutasema, 'Mnyama mkali amemrarua.' Nasi tutaona ndoto zake zitakuwaje.” 21Rubeni alilisikia hilo na kumwokoa kutoka katika mikono yao. Alisema, “Tusiuondoe uhai wake.” 22Rubeni aliwambia, “Msimwage damu. Mtupeni katika shimo hili lililopo nyikani, lakini msiweke mikono yenu juu yake” - ili kwamba aweze kumwokoa katika mikono yao na kumrudisha kwa baba yake. 23Ikawa Yusufu alipowafikia ndugu zake, walimvua vazi lake zuri. 24Wakamchukua na kumtupa shimoni. Shimo lilikuwa tupu bila maji. 25Wakakaa chini kula mkate. Walipoinua macho yao na kuangalia, na, tazama, msafara wa Waishmaeli ulikuwa ukija kutoka Gileadi, pamoja na ngamia wao waliochukua viungo, malhamu na manemane. Walikuwa wakisafiri kuvichukua kuelekea Misri. 26Yuda akawambia ndugu zake, “Ni faida gani kama tutamwua ndugu yetu na kufunika damu yake? 27Haya, na tumwuze kwa Waishmaeli na wala tusiweke mikono yetu juu yake. Kwani yeye ni ndugu yetu, nyama yetu.” Ndugu zake wakamsikiliza. 28Wafanyabiashara wa Kimidiani wakapita. Ndugu zake wakamwinua na kumtoa Yusufu shimoni. Wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande ishirini vya fedha. Waishmaeli wakamchukua Yusufu mpaka Misri.
Wimbo wa katikati
16Aliita njaa katika nchi; akaondoa upatikanaji wa mkate wote. 17Akatuma mtu mbele yao; Yusufu aliuzwa kama mtumishi. 18Miguu yake ilifungwa kwa pingu; alivishwa mnyororo wa chuma shingoni mwake, 19mpaka wakati wa maneno yake ulipotimia, nalo neno la Yahwe lilimjaribu. 20Mfalme alituma watumishi kumfungua; mtawala wa watu alimuweka huru. 21Alimuweka kuwa msimamizi wa nyumba yake kama mtawala wa mali zake zote
Injili
33Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu, mtu mwenye eneo kubwa la ardh. Alipanda mizabibu, akaiwekea uzio, akatengeneza na chombo cha kukamlia divai, akajenga na mnara wa walinzi, na akalikodisha kwa watunza zabibu. Kisha akaenda katika nchi nyingine. 34Wakati wa mavuno ya mizabibu ulipokaribia, aliwatuma baadhi ya watumishi kwa wakulima wa mizabibu kuchukua mizabibu yake. 35Lakini wakulima wa zabibu wakawachukua watumishi wake, wakampiga mmoja, wakamwua mwingine, na wakampiga mmoja kwa mawe. 36Kwa mara nyingine, Mmiliki aliwatuma watumishi wengine, wengi zaidi ya wale wa kwanza, lakini wakulima wa mizabibu waliwatendea vilevile. 37Baada ya hapo bwana yule akamtuma kwao mwana wake, akisema, 'Watamheshimu mwanangu.'' 38Lakini wakulima wa mizabibu walipomwona kijana yule, wakaambizana, 'Huyu ni mrithi, Njooni, tumuue na tumiliki urithi.' 39'Hivyo wakamchukua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu na kumwua. 40Je mmliki wa shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanya nini wakulima wa mizabibu?” 41Wakamwambia, “Atawaharibu hao watu waovu katika njia ya ukali zaidi, na kisha atalikodisha shamba la mizabibu kwa wakulima wengine wa mizabibu, watu ambao watalipa kwa ajili ya mizabibu itakapoiva.” 42Yesu akawaambia, “Hamkusoma katika maandiko, 'Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi. Hili lilitoka kwa Bwana, na inashangaza machoni petu?' 43Hivyo nawaambieni, Ufalme wa Mungu utatwaliwa kutoka kwenu na kupewa taifa linalojali matunda yake. 45Wakuu wa makuhani na mafarisayo waliposikia mifano yake, wakaona kuwa anawazungumzia wao. 46Lakini kila walipotaka kunyosha mikono juu yake, waliogopa makutano, kwa sababu watu walimtazama kama nabii.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki