Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 26 Februari
Kalenda ya Kiorthodoksi · 13 Februari (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 26 Februari 2027
Ijumaa · Wiki ya Mtoza Ushuru na Farisayo · Sauti ya 5
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Martiniani (karne ya 5)
Wiki isiyo na mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
7Wapenzi, siwaandikii ninyi amri mpya, bali amri ya zamani ambayo mmekwisha kuwa nayo tangu mwanzo. Amri ya zamani ni neno ambalo mlilolisikia. 8Hata hivyo ninawaandikia ninyi amri mpya, ambayo ni kweli katika Kristo na kwenu, kwa sababu giza linapita, na nuru ya kweli iko tayari inaangaza 9Yeye asemeye yuko kwenye nuru na amchukia ndugu yake yuko katika giza hata sasa. 10Yeye ampendaye ndugu yake anaishi katika nuru na hakuna jambo lolote liwezalo kumkwaza. 11Lakini yeye amchukiaye ndugu yake yuko gizani na anatembea gizani; Yeye hajui wapi aendako, kwa sababu giza limeyapofusha macho yake. 12Nawaandikia ninyi, watoto wapendwa, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu kwa ajili ya jina lake. 13Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mnamjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nimewaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mnamjua Baba. 14Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mnamjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mko imara, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, na mmemshinda yule mwovu. 15Msiipende dunia wala mambo ambayo yaliyo katika dunia. Iwapo yule ataipenda dunia, upendo wa kumpenda Baba haumo ndani yake. 16Kwani kila kitu kilichomo katika dunia- tamaa ya mwili, tamaa ya macho, na kiburi cha uzima- havitokani na Baba lakini vinatokana na dunia. 17Dunia na tamaa zake zinapita. Bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu huyo adumu milele.
Injili
3Wakati Yesu alipokuwa Bethania nyumbani kwa Simoni mkoma, na alipokuwa akielekea mezani, mwanamke mmoja alikuja kwake akiwa na chupa ya marashi ya nardo safi yenye gharama kubwa sana, aliivunja chupa na kuimimina juu ya kichwa chake. 4Lakini kulikuwa na baadhi yao waliokasirika. Waliambiana wao kwa wao wakisema, “Ni nini sababu ya upotevu huu? 5Manukato haya yangeweza kuuzwa kwa zaidi ya dinari mia tatu, na wakapewa maskini.” Nao walimkemea. 6Lakini Yesu alisema, “Mwacheni peke yake. Kwa nini mnamsumbua? Amefanya jambo zuri kwangu. 7Siku zote maskini mnao, na wakati wowote mnapotamani mnaweza kufanya mazuri kwao, lakini hamtakuwa nami wakati wote. 8Amefanya kile anachoweza: ameupaka mwili wangu mafuta kwa ajili ya maziko. 9Kweli nawaambia, kila mahali injili inapohubiriwa katika ulimwengu wote, kile alichofanya mwanamke huyu kitazungumzwa kwa ukumbusho wake.
Watakatifu wa siku
- Wafiadini wa Kikasisi Basili na Gabrieli, mapadri (1919)
- Mfiadini wa Kikasisi Silvesta, Askofu Mkuu wa Omsk (1920)
- Wafiadini wa Kikasisi Zosima, Nikolao, Basili, Yohana, Leontio, Vladimir, Parthenio, Yohana, Yohana, Mikaeli, mapadri, na Eugenio, shemasi, Mfiadini Paulo, Watawa Wafiadini Ana, Vera na Irina (1938)
- Watakatifu Watawa Zoe na Fotinia (Svetlana) (karne ya 5)
- Mtakatifu Mtawa Eulogio, Askofu Mkuu wa Aleksandria (607-608)
- Mtakatifu Mtawa Shio wa Mgvime (karne ya 6)
- Mtakatifu Mtawa Stefano, aliyeitwa Simeoni katika utawa, mfalme wa Serbia, anayetoa manemane (1200)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 13 Februari katika kalenda ya kanisa ni 26 Februari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki