19Amoni alikuwa na miaka kumi na mbili alipoanza kutawala; alitawala miaka miwili katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Meshlemethi; alikuwa binti wa Haruzi wa Yotba.
20Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe, kama manase baba yake alivyofanya.
21Amoni alifuata njia zote ambazo baba yake alizotembelea na kuabudu sanamu ambazo baba yake aliziabudu, na kuzisujudia.
22Akajitenga na Yahwe, Mungu wa baba zake, na hakutembea katika njia ya Yahwe.
23Watumishi wa Amoni wakafanya njama dhidi yake na kumuua mfalme kwenye nyumba yake mwenyewe.
24Lakini watu wa nchi wakawaua watu wote waliofanya njama dhidi ya mfalme Amoni, na wakamfanya Yosia mtoto wake kuwa mfalme katika sehemu yake.
25Kama ilivyo kwa mambo mengine yamhusuyo Amoni yale aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
26Watu wakamzika kwenye kaburi lake katika bustani ya Uza, na Yosia mwanawe akawa mfalme katika sehemu yake.