Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Kutoka Hezekia hadi Yosia

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Kutoka Hezekia hadi Yosia

Manase mfalme wa Yuda

2 Fal 21:1–18 · 2 Nya 33:1–20

2 Wafalme

2 Fal 21:1–18

1Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili wakati alipoanza kutawala; alitawala miaka hamsini na tano katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Hefziba.

2Alifanya maovu usoni kwa Yahwe, kama machukizo ya mataifa ambayo Yahwe aliyafukuza nje mbele ya wana wa Israeli.

3Kwa kupajenga tena mahala pa juu ambapo Hezekia baba yake alipaharibu, na akajenga madhabahu kwa ajili ya Baali, akafanya Ashera, kama Ahabu mfalme wa Israeli alivyofanya, akasujudu kwa nyota zote za mbinguni na kuwaabudu wao.

4Manase akajenga madhabahu za kipagani kwenye nyumba ya Yahwe, ingawaje Yahwe aliamuru, “Jina langu litakuwa Yerusalemu daima.”

5Akajenga madhabahu kwa ajili ya nyota zote za mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Yahwe.

6Akamuweka mtoto wake wa kiume kwenye moto; akatazama bao ushirikina na kujishuhulisha pamoja wale ambao wenye pepo wa utambuzi na wale wachawi. Akafanya maovu mengi usoni kwa Yahwe na kuchochea hasira kwa Mungu.

7Sanamu ya kuchongwa ya Ashera ambayo aliitnegeneza, akaiweka kwenye nyumba ya Yahwe. Nyumba hii ndiyo ambayo Yahwe alimwambia Daudi na Sulemani mwanawe; alisema: “Ni nyumba hii na katika Yerusalemu, ambayo nimeichagua kutoka makabila yote ya Isaraeli, ambako nitaliweka jina langu milele.

8Sintofanya miguu ya Israeli kushindwa tena nje ya nchi ambayo niliwapa babu zao, kama tu watakuwa makini kutii yale yote niliyowaamuru, na kufuata sheria zote ambazo mtumishi wangu Musa aliwaamuru.”

9Lakini watu hawakusikia, na Manase akawaongoza kufanya maovu zaidi kuliko yale ya mataifa ambayo Yahwe aliyaharibu mbele ya watu wa Israeli.

10Basi Yahwe akaongea na watumishi wake manabii, akisema,

11Kwasababu Manase mfalme wa Yuda amefanya haya machukizo, na kutenda maovu zaidi kuliko yote waliyoyatenda Waamori ambao walikuwa mbele yake walikubali, na pia aliwafanya Yuda kuasi kwa sanamu zake,

12kwa hiyo Yahwe, Mungu wa Israeli, akasema hivi: Tazama, nakaribia kuleta uovu juu ya Yerusalemu na Yuda ambayo kila mtu asikiapo kuhusu hilo, masikio yake yote yatang'aa.

13Nitanyoosha juu ya Yerusalemu kipimo kilichotumika dhidi ya Samaria, na kuangusha msatari utakaotumika dhidi ya nyumba ya Ahabu; Nitaifuta Yerusalemu safi, kama kufuta sahani, kuifuta na kuifunika juu chini.

14Nitawatupa masalia ya urithi wangu na kuwaweka mikononi mwa maadui zao. Watakuwa nyara na mateka kwa maadui zao wote,

15kwa sababu wamefanya yaliyo maovu usoni kwangu, na kunichochea hasira, tangu siku babu zao walipotoka Misri, hadi leo.”

16Aidha, Manase akazimwaga damu nyingi za wasio na hatia, hadi alipoijaza Yerusalemu kutoka upande huu kwenda mwingine kwa kifo. Hii ilikuwa ni kuongeza kwenye dhambi ambayo aliifanya Yuda kuasi, wakati walipofanya uovu mbele za Yahwe.

17Kama kwa mambo mengine yamhusuyo Manase, yote aliyoyafanya, na dhambi ambayo aliyoifanya, je haya hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafalme wa Yuda?

18Manase akalala pamoja na babu zake na alizikwa kwenye bustani ya nyumba yake, katika bustani ya Uza. Amoni mwanawe akawa mfalme katika sehemu yake.

2 Mambo ya Nyakati

2 Nya 33:1–20

1Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili alipoanza kutawala, alitawala miaka hamsini na tano katika Yerusalemu.

2Akafanya yalikuwa uovu katika macho ya Yahwe, kama yalivyo mambo ya machukizo ya mataifa ambao Yahwe alikuwa amewafukuza mbele ya watu wa Israeli.

3Kwa maana alizijenga tena sehemu za juu ambazo baba yake Hezekia alikuwa amezibomoa, na akajenga madhabahu kwa ajili ya mabaali, akatengeneza sanaamu za Maashera, na akaziinamia chini nyota zote za mbinguni na kuziabudu.

4Manase akajenga madhbahu za kipagani katika nyumba ya Yahwe, ingawa Yahwe alikuwa amemwamuru, “Ni katika Yerusalemu ambamo jina langu litawekwa milele”.

5Alijenga madhabahu kwa ajili ya nyota zote za mbinguni katika vile viwanja viwili vya nyumba ya Yahwe.

6Katika bonde la Beni Hinomu akawaweka wanaye katika moto. Akafanya misemo ya ubashiri, na uchawi, akassoma utabiri; akashauriana na wale waliozungumza na wafu na wale waliozungumza na na roho. Akafanaya maaovu mengi katika mcho ya Yahwe na alimfanya Mungu akasirike.

7Ile sanamu ya Maashera aliyokuwa amefanya, akaipeleka katika nyumba ya Mungu. Ni kuhusu nyumba hii ambayo Mungu alikuwa amesema kwa Daudi na Selemani mwanaye; alikuwa amesema, “Ni katika nyumba hii na katika Yerusalemu, ambao nimeuchangua kutoka makabila yote ya Israeli, kwamba nitaliweka jina langu milele.

8Sitawaondoa tena watu wa Israeli katina nchi hii ambayo niliitoa kwa babu zao, ikiwa tu watakuwa makini katika kuyashika yote niliyowaamuru, kuzishika sheria zangu, amri zangu, na sheria zangu nilizowapa kupitia Musa.”

9Manase akawaongoza Yuda na wakaaji wa Yerusalemu hata kufanya uovu zaidi kuliko hata watu wa mataifa ambao Yahwe alikuwa amewateketeza mbele za Israeli.

10Yahwe akasema kwa Manase, na kwa watu wake wote, lakini hawakumsikiliza.

11Kwa hiyo Yahwe akaleta juu yao maamri jeshsi wa jeshi la Ashuru, ambao walimchukua Manase katika minyonyoro, wakamfunga kwa pingu, na wakampeleka Babeli.

12Manase alipokuwa katika dhika, alimuomba Yahwe, Mungu wake, na akajinyenyekesha sana mbele za Mungu wa babu zake.

13Akaomba kwake; na Mungu akamsikiliza, na Mungu akasikia kuomba kwake na akamrudisha Yerusalemu, katika ufalme wake. Kisha Manase akafahamu kwamba Yahwe alikuwa Mungu.

14Baada ya hayo, manase akajenga ukuta wa nje ya mji wa Daudi, upande wa magharibi wa Gihoni, katika bonde, hadi kwenye lango la Samaki. Akauzungushia mlima wa Ofeli na akaupandisha ukuta hadi usawa mrefu sana. Akaweka maamri jeshi jasiri katika ngome zote za miji ya Yuda.

15Akaipeleka mbali miungu yote ya kigeni, akaondoa sanamu zote kwenye nyumba ya Yahwe, na madhabahu zote ambazo alikuwa amejenga juu ya mlima wa nyumba ya Yahwe na katika Yerusalemu, na kuvitupa nje ya mji.

16Akaijenga tena madhabahu ya Yahwe na juu yake akatoa sadaka za amani na sadaka za shukrani; akamwamuru Yuda amtumikie Yahwe, Mungu wa Israeli.

17Hata hivyo watu bado walitoa sadaka mahali pa sehemu za juu, lakini kwa Yahwe, Mungu wao pekee.

18Katika mambo mengine kuhusu Manase, maombi yake kwa Mungu wake, na maneno ya waonaji ambao walisema kwake katika jina la Yahwe, Mungu wa Israeli, tazama, yameandikwa miongoni mwa matendo ya wafalme wa Israeli.

19Katika matukio hayo kuna historia ya maombi yake, na jinsi Mungu alivyoguswa na maomabi hayo. Pia kuna kumbu kumbu ya dhambi zake zote na makosa yake, na sehemu ambako alikuwa amejenga sehemu za juu na kuzisimamisha Maashera na sanamu za kuchonga, kambla ya kujinyenyekesha mwenyewe — na imeandikwa kuhusu hayo katika tarehe ya waonaji.

20Kwa hiyo Manase akalala na babu zake, na wakamzika katika nyumba yake mwenyewe. Amoni, mwaye, akawa mfalme katika nafasi yake.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY