Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Wafilipi 4:6–7

Mstari wa Biblia · ULB

Wafilipi 4:6–7

6Msijisumbue kwa jambo lolote. Badala yake, fanyeni mambo yenu yote kwa njia ya kusali, kuomba na kushukuru. Na mahitaji yenu yajulikane kwa Mungu.

7Basi amani ya Bwana iliyo kuu kuliko ufahamu wote, italinda mioyo na mawazo yenu kwa msaad Kristo Yesu.

Soma sura nzima: Wafilipi 4

Katika muktadha

3Kwa kweli, niwasihi pia ninyi watenda kazi wenzangu, muwasaidie hawa wanawake kwa kuwa walitumika pamoja na mimi katika kueneza injili ya Bwana tukiwa na Kelementi pamoja na watumishi wengine wa Bwana, ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.

4katika Bwana siku zote. tena nitasema, furahini.

5Upole wenu na ujulikane kwa watu wote. Bwana yuko karibu.

6Msijisumbue kwa jambo lolote. Badala yake, fanyeni mambo yenu yote kwa njia ya kusali, kuomba na kushukuru. Na mahitaji yenu yajulikane kwa Mungu.

7Basi amani ya Bwana iliyo kuu kuliko ufahamu wote, italinda mioyo na mawazo yenu kwa msaad Kristo Yesu.

8Hatimaye, ndugu zangu; yatakafarini sana mambo yote yenye ukweli, heshima, haki, usafi, upendo, na yale yenye taarifa njema, yenye busara, pamoja na yale yanayohitaji kusifiwa.

9Yatekelezeni mambo yale mliojifunza, mliyopokea mliyoyasikia na yale mliyoyaona kwangu naye Baba yetu wa amani atakuwa nanyi.

10Ninayo furaha kubwa sana juu yenu katika Bwana kwa kuwa ninyi mmeonyesha tena nia ya kujihusisha kwenu juu ya mahitaji yangu. Kwa kweli, hapo awali mlitamani kunijali kwa mahitaji yangu japo hamkupata fursa ya kunisaidia.

Wafilipi 4

Kwa Kiingereza

Berean Standard BiblePhilippians 4:6–7Be anxious for nothing, but in everything, by prayer and petition, with thanksgiving, present your requests to God. And the peace of God, which surpasses all understanding, will guard your hearts and your minds in Christ Jesus.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Mit 3:5–6Mtegemee Yehova kwa moyo wako wote na wala usitegemee ufahamu wako mwenyewe, katika njia zako zote mkiri Yeye na yeye atayanyosha mapito yako.
1 Pet 5:7Mwekeeni fadhaa zenu juu yake, kwa sababu anawajali.
Zab 55:22Umtwike mizigo yako Yahwe, naye atakusaidia; yeye hataruhusu mtu mwenye haki kuyumbayumba.
1 The 5:17–18Ombeni bila kukoma. Mshukuruni Mungu kwa kila jambo, kwa sababu hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu katika Yesu Kristo.
Mt 7:7–8Omba, nawe utapewa. Tafuta, nawe utapata. Bisha hodi, na wewe utafunguliwa. Kwa yeyote anayeomba, hupokea. Na kwa yeyote anayetafuta, hupata. Na kwa mtu ambaye anayebisha hodi, atafunguliwa.
Zab 34:5–7Wale wanao mtazama yeye wana furaha, na nyuso zao hazina aibu. Huyu mtu aliye onewa alilia na Yahwe akamsikia na kumuokoa kwenye matatizo yake yote. Malaika wa Yahwe huweka kambi wakiwazunguka wale wanao muogopa yeye na kuwaokoa.
Mt 6:8Kwa hiyo, usiwe kama wao, kwa kuwa Baba yako anatambua mahitaji yako hata kabla hujaomba kwake.
Yn 14:27Amani nawapa amani yangu ninyi. Siwapi hii kama ulimwengu utoavyo. Msiifanye mioyo yenu kuwa na mahangaiko, na woga.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki