Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Waefeso 6:4
Mstari wa Biblia · ULB
Waefeso 6:4
Na ninyi akina baba, msiwakwaze watoto na kuwasababishia hasira, badala yake, waleeni katika maonyo na maagizo ya Bwana.
Katika muktadha
1Watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana hii ni haki.
2“Mheshimu baba yako na mama yako” (Maana hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi),
3“ili iwe heri kwenu na muweze kuishi maisha marefu juu ya nchi.”
4Na ninyi akina baba, msiwakwaze watoto na kuwasababishia hasira, badala yake, waleeni katika maonyo na maagizo ya Bwana.
5Enyi watumwa, iweni watiifu kwa mabwana zenu wa hapa duniani kwa heshima kubwa na kutetemeka kwa hofu itokayo mioyoni mwenu. muwe watiifu kwao kama vile mnavyomtii Kristo.
6Utii wenu usiwe tu pale mabwana zenu wanapowatazama ili kuwafurahisha. Badala yake, iweni watiifu kama watumwa wa Kristo. Fanyeni Mapenzi ya Mungu kutoka mioyoni mwenu,
7watumikieni kwa mioyo yenu yote, kwa kuwa mnamtumikia Bwana na wala si wanadamu,
Kwa Kiingereza
Fathers, do not provoke your children to wrath; instead, bring them up in the discipline and instruction of the Lord.Marejeo mtambuka
Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.
Akina baba msiwachokoze watoto wenu, ili kwamba wasije wakakata tamaa.Mfundishe mtoto njia inayompasa na wakati akiwa mzee hatayaacha mafundisho hayo.Fimbo na maonyo huleta hekima, bali mtoto huru mbali na makaripio humwaibisha mama yake.Mrudi mwanao wakati kuna matumaini na usiwe na shauku ya kumweka katika mauti.na mtayafundisha kwa bidii kwa watoto wenu, mtayazungumza wakati mkaapo katika nyumba zenu, wakati mlalapo, na wakati mwinukapo.Unatambua ya kuwa tangu utotoni mwako uliyajua maandiko matakatifu. Haya yanaweza kukuhekimisha kwa ajili ya wokovu kwa njia ya imani katika kristo Yesu.Mwadibishe mwanao naye atakupa pumziko; ataleta furaha katika maisha yako.Usizuie kuadilisha mtoto, maana ukimchapa kwa fimbo, hatakufa. Ni wewe unayepaswa kumchapa kwa fimbo na kuikoa nafsi yake kuzimu.Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki