Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Wakolosai 3:21
Mstari wa Biblia · ULB
Wakolosai 3:21
Akina baba msiwachokoze watoto wenu, ili kwamba wasije wakakata tamaa.
Katika muktadha
18Wake, wanyenyekeeni waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.
19Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali dhidi yao.
20Watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, maana ndivyo impendezavyo Bwana.
21Akina baba msiwachokoze watoto wenu, ili kwamba wasije wakakata tamaa.
22Watumwa, watiini mabwana zenu katika mwili kwa mambo yote, sio kwa huduma ya macho kama watu wa kufurahisha tu, bali kwa moyo wa kweli. Mwogopeni Mungu.
23Chochote mfanyacho, fanyeni kutoka nafsini mwenu kama kwa Bwana na si kama kwa wanadamu.
24Mnajua ya kwamba mtapokea tuzo ya umilkaji kutoka kwa Bwana. Ni Kristo Bwana mnayemtumikia.
Kwa Kiingereza
Fathers, do not provoke your children, so they will not become discouraged.Marejeo mtambuka
Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.
Wanangu, sikilizeni, fundisho la baba, na zingatieni ili mjue maana ya ufahamu. Mimi ninawapa mafundisho mazuri; msiyaache mafundisho yangu. Mimi nilikuwa mwana kwa baba yangu, mpole na mtoto pekee kwa mama yangu, baba alinifundisha akiniambia, “Moyo wako uzingatie sana maneno yangu; shika amri zangu nawe uishi.Na ninyi akina baba, msiwakwaze watoto na kuwasababishia hasira, badala yake, waleeni katika maonyo na maagizo ya Bwana.Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki