Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Wakolosai 2:8

Mstari wa Biblia · ULB

Wakolosai 2:8

Angalieni ya kwamba mtu yeyote asiwanase kwa falsafa na maneno matupu ya udanganyifu kulingana na mapokeo ya wanadamu, kulingana na kanuni za kidunia, na sio kulingana na Kristo.

Soma sura nzima: Wakolosai 2

Katika muktadha

5Na ingawa sipo pamoja nanyi katika mwili, lakini nipo nanyi katika roho. Ninafurahi kuona utaratibu wenu mzuri na nguvu ya imani yenu katika Kristo.

6Kama mlivyompokea Kristo Bwana, tembeeni katika yeye.

7Mwimarishwe katika yeye, mjengwe katika yeye, mwimarishwe katika imani kama tu mlivyofundishwa, na kufungwa katika shukrani nyingi.

8Angalieni ya kwamba mtu yeyote asiwanase kwa falsafa na maneno matupu ya udanganyifu kulingana na mapokeo ya wanadamu, kulingana na kanuni za kidunia, na sio kulingana na Kristo.

9Kwa kuwa katika yeye ukamilifu wote wa Mungu unaishi katika mwili.

10Nanyi mmejazwa katika yeye. Yeye ni kichwa cha kila uweza na mamlaka.

11Katika yeye pia mlitahiriwa kwa tohara isiyofanywa na wanadamu katika kuondolewa mwili wa nyama, lakini ni katika tohara ya Kristo.

Wakolosai 2

Kwa Kiingereza

Berean Standard BibleColossians 2:8See to it that no one takes you captive through philosophy and empty deception, which are based on human tradition and the spiritual forces of the world rather than on Christ.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

1 Tim 6:20Timotheo, linda kile ulichopewa. Jiepushe na majadiliano ya kipumbavu na mabishano yenye kujipinga ambayo kwa kwa uongo huitwamaarifa.
Efe 5:6Mtu yote asikudanganye kwa maneno matupu, kwa sababu ya mambo haya hasira ya Mungu inakuja juu ya wana wasiotii.
Mt 7:15Jihadhari na manabii wa uongo, wanaokuja wamevaa ngozi ya kondoo, lakini kweli ni mbweha wakali.
Gal 4:9Lakini sasa kwamba mnamjua Mungu, au kwamba mnajulikana na Mungu, kwa nini mnarudi tena kwenye kanuni dhaifu za kwanza na zisizo za thamani? Je mnataka kuwa watumwa tena?
1 Kor 3:18–19Mtu asijidanganye mwenyewe, kama yeyote miongoni mwenu anadhani ana hekima katika nyakati hizi, awe kama “mjinga” ndipo atakuwa na hekima. Kwa kuwa hekima ya dunia hii ni ujinga mbele za Mungu, Kwa kuwa imeandikwa, “Huwanasa wenye hekima kwa hila zao”
Rum 1:21–22Hii ni kwa sababu, ingawa walijua kuhusu Mungu, hawakumtukuza yeye kama Mungu, wala hawakumpa shukrani. Badala yake, wamekuwa wapumbavu katika mawazo yao, na mioyo yao yenye ujinga ilitiwa giza. Walijiita kuwa ni werevu, lakini wakawa wajinga.
Kol 2:20Ikiwa mlikufa pamoja na Kristo kwa tabia za dunia, mbona mnaishi kama mnawajibika kwa dunia:
2 Tim 3:13Watu waovu na wadanganyifu watazidi kuwa waovu zaidi. Watawapotosha wengine. Wao wenyewe wamepotoshwa.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki