Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › 1 Yohana 4:18
Mstari wa Biblia · ULB
1 Yohana 4:18
Hakuna hofu ndani ya pendo. Lakini pendo kamili huitupa hofu nje, kwa sababu hofu huhusiana na hukumu. Lakini yeye aogopaye hajakamilishwa katika pendo.
Katika muktadha
15Kila anayekiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu anakaa ndani yake na yeye ndani ya Mungu.
16Na tunajua na kuamini upendo alio nao Mungu ndani yetu. Mungu ni pendo, na yeye anayekaa ndani ya upendo anakaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.
17Katika pendo hili limekwisha kamilishwa kati yetu, ili tuwe na ujasiri siku ya hukumu, kwa sababu kama yeye alivyo, na sisi ndivyo tulivyo katika ulimwenngu huu.
18Hakuna hofu ndani ya pendo. Lakini pendo kamili huitupa hofu nje, kwa sababu hofu huhusiana na hukumu. Lakini yeye aogopaye hajakamilishwa katika pendo.
19Tunapenda kwa sababu Mungu alitupenda kwanza.
20Ikiwa mmoja atasema, “Nampenda Mungu” lakini anamchukia ndugu yake, ni mwongo. Kwa sababu asiyempenda ndugu yake, anayemuona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamuona.
21Na hii ndiyo amri tuliyo nayo kutoka kwake: Yeyote ampendaye Mungu, anapaswa kumpenda ndugu yake pia.
Kwa Kiingereza
There is no fear in love, but perfect love drives out fear, because fear involves punishment. The one who fears has not been perfected in love.Marejeo mtambuka
Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.
Kwa kuwa Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na upendo na nidhamu.Kwa kuwa hamkupokea roho wa utumwa tena hata muogope. Badala yake, mlipokea roho ya kufanywa kuwa wana, ambayo kwayo tunalia, “Abba, Baba!”Hakuna hata mmoja aliyemuona Mungu. Kama tukipendana sisi kwa sisi, Mungu anakaa ndani yetu na pendo lake limekamilika ndani yetu.Aliapa kuthibitha kwamba ingewezekana kumtumikia Yeye bila hofu, baada ya kuokolewa kutoka katika mikononi ya adui zetu. katika utakatifu na haki mbele zake siku zetu zote.Kwa hiyo, tupokee ufalme ambao hautetemeshwi, tufurahi katika hali ya kumwabudu Mungu kwa kukubali pamoja na kunyenyekea katika kicho,Waamini kuwa kuna Mungu mmoja; uko sahihi. Lakini mapepo nayo yanaamini hivyo na kutetemeka.Mwili wangu hutetemeka kwa hofu yako, na ninaziogopa amri za haki yako.Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki