Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › 1 Wakorintho 13:4–7

Mstari wa Biblia · ULB

1 Wakorintho 13:4–7

4Upendo huvumilia na hufadhili. Upendo haujisifu au kujivuna. Hauna kiburi

5au ukorofi. Hautafuti mambo yake, hauoni uchungu haraka, wala hauhesabu mabaya.

6Haufurahii udhalimu. Badala yake, hufurahi katika kweli.

7Upendo huvumilia mambo yote; huamini mambo yote, una ujasiri katika mambo yote, na hustahimili mambo yote.

Soma sura nzima: 1 Wakorintho 13

Katika muktadha

1Tuseme kwamba ninanena kwa lugha za wanadamu na za malaika. Lakini kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo au upatu uvumao.

2Na kwamba nina karama ya unabii na ufahamu wa kweli zilizofichika na maarifa, na kwamba ninayo imani ya kuhamisha milima. Lakini ikiwa sina upendo, mimi si kitu.

3Na tuseme kwamba ninatoa milki yangu yote na kuwalisha masikini, na kwamba ninautoa mwili wangu ili nichomwe moto. Lakini kama sina upendo, hainifaidii kitu.

4Upendo huvumilia na hufadhili. Upendo haujisifu au kujivuna. Hauna kiburi

5au ukorofi. Hautafuti mambo yake, hauoni uchungu haraka, wala hauhesabu mabaya.

6Haufurahii udhalimu. Badala yake, hufurahi katika kweli.

7Upendo huvumilia mambo yote; huamini mambo yote, una ujasiri katika mambo yote, na hustahimili mambo yote.

8Upendo haukomi. Ikiwa kuna unabii, wote utapita. Ikiwa kuna lugha, zitakoma. Ikiwa kuna maarifa, yatapita.

9Kwa kuwa tunajua kwa sehemu na tunafanya unabii kwa sehemu.

10Lakini ijapo ile iliyo kamili, ile isiyo kamili itapita.

1 Wakorintho 13

Kwa Kiingereza

Berean Standard Bible1 Corinthians 13:4–7Love is patient, love is kind. It does not envy, it does not boast, it is not proud. It is not rude, it is not self-seeking, it is not easily angered, it keeps no account of wrongs. Love takes no pleasure in evil, but rejoices in the truth. It bears all things, believes all things, hopes all things, endures all things.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

1 Pet 4:8Kabla ya mambo yote, eweni na bidii katika upendo kwa kila mmoja, kwa kuwa upendo hautafuti kufunua dhambi za wengine.
Efe 4:32Mwe na huruma. Msameheane ninyi kwa ninyi, kama vile Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Gal 5:21–22wivu, ulevi, ulafi na mambo mengine kama haya. Nawaonya ninyi, kama nilivyowaonya mwanzoni, kwamba wale wanaofanya mambo kama hayo hawataurithi ufalme wa Mungu. Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani,
Mit 10:12Chuki huchochea mafarakano, bali upendo hufunika juu ya makwazo yote.
Kol 3:12Kama wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, jivikeni utu wema, ukarimu, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
Rum 12:9Pendo lisiwe na unafiki. Chukieni uovu; mshikilie yaliyo mema.
1 Pet 2:24Yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu katika mwili wake kwenye mti, ili kwamba tusiwe na sehemu tena katika dhambi, na kwamba tuishi kwa ajili ya haki. Kwa kupigwa kwake ninyi mmepona.
1 Yoh 4:11Wapendwa, ikiwa Mungu alitupenda sisi, vile vile tunapaswa kupendana sisi kwa sisi.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki