Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › 1 Wakorintho 3:16–17

Mstari wa Biblia · ULB

1 Wakorintho 3:16–17

16Hamjui kuwa ninyi ni hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

17Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu yule. Kwa kuwa hekalu la Mungu ni takatifu, na hivyo na ninyi.

Soma sura nzima: 1 Wakorintho 3

Katika muktadha

13kazi yake itafunuliwa, kwa mwanga wa mchana utaidhihirisha. Kwa kuwa itadhihirishwa na moto. Moto utajaribu ubora wa kazi wa kila mmoja alichofanya.

14Kama chochote mtu alichojenga kitabaki, yeye atapokea zawadi.

15Lakini kama kazi ya mtu ikiteketea kwa moto, atapata hasara. Lakini yeye mwenyewe ataokolewa, kama vile kuepuka katika moto.

16Hamjui kuwa ninyi ni hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

17Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu yule. Kwa kuwa hekalu la Mungu ni takatifu, na hivyo na ninyi.

18Mtu asijidanganye mwenyewe, kama yeyote miongoni mwenu anadhani ana hekima katika nyakati hizi, awe kama “mjinga” ndipo atakuwa na hekima.

19Kwa kuwa hekima ya dunia hii ni ujinga mbele za Mungu, Kwa kuwa imeandikwa, “Huwanasa wenye hekima kwa hila zao”

20Na tena “Bwana anajua mawazo ya wenye busara ni ubatili.”

1 Wakorintho 3

Kwa Kiingereza

Berean Standard Bible1 Corinthians 3:16–17Do you not know that you yourselves are God’s temple, and that God’s Spirit dwells in you? If anyone destroys God’s temple, God will destroy him; for God’s temple is holy, and you are that temple.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

1 Kor 6:19Hamjui kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu, akaaye ndani yenu, yule ambaye mlipewa kutoka kwa Mungu? Hamjui kwamba si ninyi wenyewe?
Eze 36:27Nitaiweka Roho yangu ndani yenu na kuwawezesha kutembea katika sheria zangu na kuziweka hukumu zangu, hivyo mtazitenda.
2 Kor 6:16Na kuna makubaliano gani yapo kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi ni hekalu la Mungu aliye hai, kama ambavyo Mungu alisema: “Nitakaa kati yao na kutembea kati yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”
Rum 8:11Ikiwa Roho wa yule aliyemfufua Yesu kutoka wafu huishi ndani yenu, yeye yule aliyemfufua Kristo kutoka katika wafu ataipa pia miili yenu ya mauti uhai kwa njia ya Roho wake, aishie ndani yenu.
Efe 2:21–22Katika yeye jengo lote limeungamanishwa pamoja na kukua kama hekalu ndani ya Bwana. Ni ndani yake ninyi nanyi mnajengwa pamoja kama mahali pa kuishi pa Mungu katika Roho.
Rum 8:9Hata hivyo, hampo katika mwili bali katika Roho, kama ni kweli kwamba Roho wa Mungu huishi ndani yenu. Lakini kama mtu hana Roho wa Kristo, yeye si wake.
Yn 14:17Roho wa kweli. Ulimwengu hauwezi kumpokea yeye kwa sababu haumuoni, au kumjwa yeye. hata hivyo ninyi, mnamjua yeye, kwani anakaa pamoja nayi na atakuwa ndani yenu.
1 Pet 2:5Ninyi pia ni kama mawe yaliyo hai yanayojengwa juu kuwa nyumba ya kiroho, ili kuwa ukuhani mtakatifu ambao hutoa dhabihu za kiroho zinazokubaliwa kwa Mungu kupitia Yesu Kristo.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki