Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 10 Novemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 10 Novemba 2027

Jumatano · Juma la 32 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatano ya Juma la 32 la Mwaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe

Mt. Leo Mkuu, papa na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Haimo katika tafsiri hii

Wimbo wa katikati

Zab 82:3–4, 6–7

3Wateteeni maskini na yatima; dumisheni haki kwa aliyetaabishwa na fukara. 4Muokoeni maskini na muhitaji; watoeni mkononi mwa waovu. 6Mimi nilisema, “Ninyi ni miungu, na ninyi nyote wana wa Mungu aliye Juu. 7Hata hivyo mtakufa kama wanadamu na mtaanguka kama mmoja wa wakuu.”

Injili

Lk 17:11–19

11Ilitokea kwamba alivyokua akisafiri kwenda Yerusalemu, alipita mpakani mwa Samaria na Galilaya. 12Alipokua akiingia kwenye kijiji kimoja, huko alikutana na watu kumi waliokuwa na ukoma. Wakasimama mbali 13wakapaza sauti wakasema “Yesu, Bwana tuhurumie.” 14Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” nao walipokua wakienda wakatakasika. 15Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa sauti kuu akimsifu Mungu. 16Akapiga magoti miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikua msamaria. 17Yesu akajibu, akasema, “Je hawakutakasika wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa? 18Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumtukuza Mungu, isipokuwa huyu mgeni?” 19Akamwambia, “Inuka na uende zako imani yako imekuponya.”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 10 Novemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki