Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 10 Novemba

Kalenda ya Kiorthodoksi · 28 Oktoba (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 10 Novemba 2027

Jumatano · Wiki ya 21 baada ya Pentekoste · Sauti ya 3

Sikukuu na watakatifu

Mfiadini Mkuu Paraskeva, aitwaye Pyatnitsa (karne ya 3)

Siku ya mfungo

Mfungo: pamoja na mafuta

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

Kol 1:18–23

18Na yeye ndiye kichwa cha mwili yaani kanisa, yeye ni mwanzo na mzaliwa wa kwanza kutoka miongoni mwa wafu, hivyo, ana nafasi ya kwanza miongoni mwa vitu vyote. 19Kwa kuwa Mungu alipendezwa kwamba utimilifu wake wote uishi ndani yake, 20na kupatanisha vitu vyote kwake kwa njia ya Mwanawe. Mungu alifanya amani kupitia damu ya msalaba wake. Mungu alipatanisha vitu vyote kwake mwenyewe, ikiwa ni vitu vya duniani au vitu vya mbinguni. 21Nanyi pia, kwa wakati mmoja mlikuwa wageni kwa Mungu na mlikuwa maadui wake katika akili na matendo maovu. 22Lakini sasa amewapatanisha ninyi kwa mwili wake kupitia kifo. Alifanya hivi ili kuwaleta ninyi watakatifu, wasio na lawama na bila dosari mbele yake, 23kama mkiendelea katika imani, mliyoimarishwa na kuwa thabiti, pasipo kuondoshwa mbali kutoka kwenye taraja la ujasiri la injili mliyoisikia. Hi ndiyo injili iliyotangazwa kwa kila mtu aliyeumbwa chini ya mbingu. Hii ndiyo injili ambayo kwayo mimi, Paulo, nimekuwa mtumishi.

Injili

Lk 11:9–13

9Nami pia nawaambieni, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata, pigeni hodi nanyi mtafunguliwa. 10Kwa kuwa kila mtu aombaye atapokea, na kila mtu atafutaye atapata, na kila mtu apigaye hodi, mlango utafunguliwa kwake. 11Ni baba yupi miongoni mwenu, mwanaye akimuomba samaki atampa nyoka badala yake.? 12Au akimuomba yai atampa nge badala yake?. 13Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajuwa kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, je si zaidi sana Baba yenu wa mbinguni kwamba atawapa Roho Mtakatifu hao wamuombao?”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 10 Novemba

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 28 Oktoba katika kalenda ya kanisa ni 10 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki