Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 11 Novemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 11 Novemba 2027
Alhamisi · Juma la 32 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Alhamisi ya Juma la 32 la Mwaka
Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Mt. Martino wa Tours, askofu · Kumbukumbu
Masomo ya siku
Somo la kwanza
Haimo katika tafsiri hii
Wimbo wa katikati
89Yahwe, neno lako linasimama milele; neno lako limefanywa imara mbinguni. 90Uaminifu wako wadumu kwa ajili ya vizazi vyote; umeiimarisha nchi, nayo inadumu. 91Vitu yote yaliendelea mpaka leo hii, kama vile ulivyosema katika amri zako za haki, maana vitu vyote ni watumishi wako. 130Ufafanuzi wa maneno yako huleta nuru; na kumpa ufahamu mjinga. 135Uso wako umwangazie mtumishi wako, na unifundishe sheria zako. 175Naomba niishi na nikusifu wewe, na amri zako za haki zinisaidie.
Injili
20Alipoulizwa na mafarisayo ufalme wa Mungu utakuja lini, Yesu akawajibu akisema, “Ufalme wa Mungu sio kitu ambacho kinaweza kuonekana. 21Wala watu hawatasema, 'Angalia hapa!' au, 'Angalia kule!' kwa maana ufalme wa Mungu umo ndani yenu.” 22Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona moja ya siku ya Mwana wa Adamu, lakini hamtaiona. 23Watawaambia, 'Angalia, kule! Angalia, hapa!' Lakini msiende kuangalia, wala kuwafuafata, 24kama umeme wa radi umulikao katika anga kuanzia upande mmoja hadi mwingine. Hivyo hata Mwana wa Adamu atakuwa ivyo katika siku yake. 25Lakini kwanza itampasa kuteseka katika mambo mengi na kukataliwa na kizazi hiki.
Watakatifu wa siku
- Mt. Martino wa Tours, askofu
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki