Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 20 Septemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 7 Septemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 20 Septemba 2027
Jumatatu · Wiki ya 14 baada ya Pentekoste · Sauti ya 4
Sikukuu na watakatifu
Kabla ya Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Mama Mtakatifu Sana wa Mungu
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
10Kwa hiyo ninatosheka kwa ajili ya Kristo, katika udhaifu, katika matukano, katika shida, katika mateso, katika hali ya masikitiko. Kwa kuwa wakati nikiwa dhaifu, kisha nina nguvu. 11Mimi nimekuwa mpumbavu! ninyi mlinilazimisha kwa hili, kwa kuwa ningekuwa nimesifiwa na ninyi. Kwa kuwa sikuwa duni kabisa kwa hao waitwao mitume—bora, hata kama mimi si kitu. 12Ishara za kweli za mtume zilifanyika katikati yenu kwa uvumilivu, ishara na maajabu na matendo makuu. 13Kwa namna gani mlikuwa wa muhimu wa chini kuliko makanisa yaliyobaki, isipokuwa kwamba sikuwa mzigo kwenu? Mnisamehe kwa kosa hili! 14Tazama! mimi niko tayari kuja kwenu kwa mara ya tatu. Sitakuwa mzigo kwenu, kwa kuwa sitaki kitu kilicho chenu. Nawataka ninyi. Kwa kuwa watoto hawapaswi kuweka akiba kwa ajili ya wazazi. Badala yake, wazazi wanapaswa kuweka akiba kwa ajili ya watoto. 15Nitafurahi zaidi kutumia na kutumiwa kwa ajili ya nafsi zenu. Kama ninawapenda zaidi, natakiwa kupendwa kidogo? 16Lakini kama ilivyo, sikuwalemea mzigo ninyi. Lakini kwa kuwa mimi ni mwerevu sana, mimi ni yule aliyewashika ninyi kwa nimekuwa ambaye aliyewapata kwa udanganyifu. 17Je, nilichukua kwa kujifanyia faida kwa yeyote niliyemtuma kwenu? 18Nilimsihi Tito kuja kwenu, na nilituma ndugu mwingine pamoja naye. Je, Tito aliwafanyia faida ninyi? Je, hatukutembea katika njia ile ile? Je, hatukutembea katika nyayo zile zile? 19Mnadhani kwa muda huu wote tumekuwa tukijitetea sisi wenyewe kwenu? Mbele za Mungu, na katika Kristo, tumekuwa tukisema kila kitu kwa ajili ya kuwaimarisha ninyi.
Waraka (ya Jumanne)
20Kwa kuwa nina hofu kwamba nitakapokuja naweza nisiwapate ninyi kama ninavyotamani. Nina hofu kwamba mnaweza msinipate mimi kama mnavyotamani. Nahofia kwamba kunaweza kuwa na majadiliano, wivu, milipuko ya hasira, tamaa ya ubinafsi, umbeya, kiburi, na ugomvi. 21Nina hofu kwamba nitakaporudi tena, Mungu wangu anaweza kuninyenyekeza mbele yenu. Nina hofu kwamba ninaweza kuhuzunishwa na wengi ambao wamefanya dhambi kabla ya sasa, na ambao hawakutubu uchafu, na uasherati na mambo ya tamaa wanayoyatenda. 13:1Hii ni mara ya tatu kwamba nakuja kwenu. “Kila shitaka lazima lijengwe na uthibitisho wa mashahidi wawili au watatu.” 2Nimekwishashasema kwa hao waliotenda dhambi kabla na kwa wengine wote wakati nilipokuwa huko mara ya pili, na ninasema tena: Nitakapokuja tena, sitawavumilia.
Injili
10Yesu alipokuwa peke yake, wale waliokuwa karibu naye na wale kumi na wawili walimuuliza kuhusu mifano. 11Akasema kwao, “Kwenu mmepewa siri za ufalme wa Mungu. Lakini kwa walio nje kila kitu ni mifano, 12ili wakitazama, ndiyo hutazama, lakini hawaoni, na kwa hiyo wanaposikia ndiyo husikia, lakini hawaelewi, amasivyo wangegeuka na Mungu angeliwasamehe.” 13Na akasema kwao, “Je hamuelewi mfano huu? Mtawezaje kuelewa mifano mingine?. 14Mpanzi alipanda neno. 15Baadhi ni wale walioanguka pembeni mwa njia, mahali neno lilipopandwa. Na walipolisikia, mara Shetani akaja na kulichukua neno ambalo lilipandwa ndani yao. 16Na baadhi ni wale waliopandwa juu ya mwamba, ambao, wanapolisikia neno, kwa haraka wanalipokea kwa furaha. 17Na hawana mizizi yoyote ndani yao, lakini huvumilia kwa muda mfupi. Halafu tabu na masumbufu vinapokuja kwa sababu ya neno, mara hujikwaa. 18Na wengine ni wale waliopandwa katika miiba. Wanalisikia neno, 19lakini masumbufu ya dunia, udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine, huwaingia na kulisonga neno, na linashindwa kuzaa matunda. 20Kisha kuna wale ambao wamepandwa kwenye udongo mzuri. Wanalisikia neno na kulipokea na huzaa matunda: baadhi thelathini, na baadhi sitini, na baadhi mia moja.” 21Yesu akawaambia, “ Je huwa unaleta taa ndani ya nyumba na kuiweka chini ya kikapu, au chini ya kitanda? Huileta ndani na kuiweka juu ya kiango. 22Kwa kuwa hakuna chochote kilichojificha ambacho hakitajulikana, na hakuna siri ambayo haitawekwa wazi. 23Akiwapo mwenye masikio ya kusikia, na asikie!”
Injili (ya Jumanne)
24Akawaambia, “ Iweni makini kwa kile mnachokisikia, kwa kuwa kipimo mpimacho, ndicho mtakachopimiwa, na itaongezwa kwenu. 25Kwa sababu yeye aliyenacho, atapokea zaidi, na yule asiyenacho, kutoka kwake vitachukuliwa hata vile alivyonavyo.” 26Na akasema, “Ufalme wa Mungu umefananishwa na mtu aliyepanda mbegu katika udongo. 27Alipolala usiku na kuamka asubuhi, na mbegu zikachipuka na kukua, ingawa hajui ilivyotokea. 28Dunia hutoa mbegu yenyewe; kwanza majani, halafu maua, halafu mbegu zilizo komaa. 29Na wakati mbegu itakapokua imeiva mara hupeleka mundu, kwa sababu mavuno yamewadia.” 30Na akasema, “tuufananishe ufalme wa Mungu na kitu gani, au tutumie mfano gani kuuelezea?. 31Ni kama mbegu ya haradali, ambapo ilipopandwa ni ndogo sana kuliko mbegu zote duniani. 32Hata, wakati imepandwa, inakuana kuwa kubwa zaidi ya mimea yote ya bustani, na inafanya matawi makubwa, hata ndege wa mbinguni huweza kufanya viota vyao kwenye kivuli chake.” 33Kwa mifano mingi alifundisha na alisema neno kwao, kwa kadiri walivyoweza kuelewa, 34na hakusema nao bila mifano. Lakini wakati alipokuwa peke yake, akawaelezea kila kitu wanafunzi wake.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini Sozonti (karibu 304)
- Askofu Mtakatifu Yohana, Askofu Mkuu wa Novgorod (1186)
- Mtawa Mfiadini Makario wa Kaniv, arkimandriti wa Ovruch, wa Pereyaslav (1678)
- Mtakatifu Mtawa Makario wa Optina (1860)
- Wafiadini wa Kikasisi Petro na Mikaeli, mapadri, na Aleksanda, shemasi (1918)
- Wafiadini wa Kikasisi Eugenio, Mitropoliti wa Nizhny Novgorod, na pamoja naye Stefano, padri, na Watawa Wafiadini Eugenio, Nikolao na Pakomio (1937)
- Wafiadini wa Kikasisi Gregori na Basili, mapadri, Mtawa Mfiadini Leo (1937)
- Mitume Euodo (66) na Onesiforo (baada ya 67), wa Mitume 70
- Mfiadini Eupsikio (karne ya 2)
- Mtakatifu Mtawa Luka (baada ya 975)
- Watakatifu Watawa Aleksanda Peresvet na Andrea Oslyabya (1380)
- Mtakatifu Mtawa Serapioni wa Spaso-Eleazarov, wa Pskov (1480)
- Mkutano wa Wafiadini Wapya na Waungamaji wa Kazakhstan
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 7 Septemba katika kalenda ya kanisa ni 20 Septemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki