Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 19 Septemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 6 Septemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 19 Septemba 2027
Jumapili · Sauti ya 4
Sikukuu na watakatifu
Jumapili ya 13 baada ya Pentekoste
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Injili ya 2 ya Sala ya Alfajiri
1Wakati sabato ilipokwisha, Mariamu Magdalena na Mariamu mama yake na Yakobo, na Salome, walinunua manukato mazuri, ili waweze kuja na kuupaka mafuta mwili wa Yesu kwa ajili ya maziko. 2Asubuhi na mapema siku ya kwanza ya juma, walienda kwenye kaburi wakati jua lilipochomoza. 3Wakisemezana wao kwa wao, “Nani ataliviringisha jiwe kwa ajili yetu ili tuingie kaburini?” 4Wakati walipotazama, walimuona mtu amekwisha kulivingirisha jiwe, ambalo lilikuwa kubwa sana. 5Wakaingia kwenye kaburi na wakamwona kijana amevaa joho jeupe, ameketi upande wa kulia, na wakashangazwa. 6Akawaambia, “Msiogope. Mnamtafuta Yesu, wa Nazareti, aliyesulibiwa. Amefufuka! Hayupo hapa. Tazama mahali pale walipokuwa wamemweka. 7Nendeni, mkawaambie wanafunzi wake na Petro ya kuwa amewatangulia kuelekea Galilaya. Huko mtamwona, kama alivyokua amewaambia.” 8Wakaondoka na kukimbia kutoka kwenye kaburi; walitetemeka na walishangazwa. Hawakusema chochote kwa mtu yeyote sababu waliogopa sana.
Waraka
13Muwe macho, simameni imara, mtende kama wanaume, muwe na nguvu. 14Basi yote myafanyayo yafanyike katika upendo. 15Mnaijua kaya ya Stefana. Mnajua kwamba walikuwa waamini wa kwanza huko Akaya, na kwamba walijiweka wenyewe kwenye huduma ya waumini. Na sasa nawasihi, kaka na dada zangu, 16kuweni wanyenyekevu kwa watu kama hao, na kwa kila mtu anayesaidia katika kazi na watenda kazi pamoja nasi. 17Na ninafurahi kwa ujio wa Stefana, Fotunato, na Akiko. Wamesimama mahali ambapo ninyi mgepaswa kuwa. 18Kwa kuwa wameifurahisha roho yangu na yenu. Kwa hiyo sasa, watambueni watu kama hawa. 19Makanisa ya Asia wametuma salamu kwenu. Akila na Priska wanawasalimu katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko nyumbani kwao. 20Kaka na dada zangu wote wanawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu. 21Mimi, Paulo, naandika hivi kwa mkono wangu. 22Kama yeyote hampendi Bwana, basi laana iwe juu yake. Bwana wetu, njoo! 23Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi. 24Upendo wangu uwe pamoja nanyi katika Kristo Yesu.
Injili
33Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu, mtu mwenye eneo kubwa la ardh. Alipanda mizabibu, akaiwekea uzio, akatengeneza na chombo cha kukamlia divai, akajenga na mnara wa walinzi, na akalikodisha kwa watunza zabibu. Kisha akaenda katika nchi nyingine. 34Wakati wa mavuno ya mizabibu ulipokaribia, aliwatuma baadhi ya watumishi kwa wakulima wa mizabibu kuchukua mizabibu yake. 35Lakini wakulima wa zabibu wakawachukua watumishi wake, wakampiga mmoja, wakamwua mwingine, na wakampiga mmoja kwa mawe. 36Kwa mara nyingine, Mmiliki aliwatuma watumishi wengine, wengi zaidi ya wale wa kwanza, lakini wakulima wa mizabibu waliwatendea vilevile. 37Baada ya hapo bwana yule akamtuma kwao mwana wake, akisema, 'Watamheshimu mwanangu.'' 38Lakini wakulima wa mizabibu walipomwona kijana yule, wakaambizana, 'Huyu ni mrithi, Njooni, tumuue na tumiliki urithi.' 39'Hivyo wakamchukua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu na kumwua. 40Je mmliki wa shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanya nini wakulima wa mizabibu?” 41Wakamwambia, “Atawaharibu hao watu waovu katika njia ya ukali zaidi, na kisha atalikodisha shamba la mizabibu kwa wakulima wengine wa mizabibu, watu ambao watalipa kwa ajili ya mizabibu itakapoiva.” 42Yesu akawaambia, “Hamkusoma katika maandiko, 'Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi. Hili lilitoka kwa Bwana, na inashangaza machoni petu?'
Watakatifu wa siku
- Kumbukumbu ya muujiza wa Malaika Mkuu Mikaeli huko Khonai (Kolosai) (karne ya 4)
- Wafiadini Eudoksio, Zenoni na Makario, na pamoja nao askari 1104 (311-312)
- Mfiadini wa Kikasisi Demetrio, padri (1918)
- Wafiadini wa Kikasisi Konstantino, Yohana na Vsevolod, mapadri (1937)
- Mfiadini Romilo na pamoja naye askari 11000 (karibu 107-115)
- Mtakatifu Mtawa Arkipo (karne ya 4)
- Wafiadini Kiriako, Fausto, padri, Abibo, shemasi, na pamoja nao wafiadini 11 (karibu 250)
- Mfiadini wa Kikasisi Kirilo, Askofu wa Gortina (karne ya 3-4)
- Mtakatifu Mtawa Daudi (karne ya 6)
- Ikoni za Mama wa Mungu za Udugu wa Kyiv (1654) na za Arapet
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 6 Septemba katika kalenda ya kanisa ni 19 Septemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki