Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 21 Agosti

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 21 Agosti 2027

Jumamosi · Juma la 20 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi ya Juma la 20 la Mwaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe

Mt. Pio X, papa · Kumbukumbu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Rut 2:1–3, 8–11; 4:13–17

1Basi Elimeleki mme wa Naomi, alikuwa na jamaa aitwaye Boazi, aliye kuwa tajiri, na mtu maarufu. 2Ruth, Mmoabu, alimwambia Naomi, “Ngoja niende nikakusanye mabaki ya chakula katika shamba. Nitamfuata yeyote ambaye nitapata kibali machoni pake.” Hivyo naomi akamwambia, “Nenda, mwanangu.” 3Ruth alienda kuvuna kwenye shamba akiwafuata kwa nyuma wavunaji. Na kumbe ile sehemu ya shamba ilikuwa ni mali ya Boazi, aliyekuwa na mahusiano na Elimeleki. 8Kisha Boazi akamwambia Ruth, “Unanisikiliza, mwanangu? Usiende kuvuna kwenye shamba lingine; usiondoke shambani kwangu. Badala yake, baki hapa na wasichana wangu wa kazi. 9Yaelekeze tu macho yako kwenye shamba ambamo wanaume wanavuna na ufuatie nyuma ya wanawake wengine. Je, sikuwaelekeza wanaume wasikuguse? Na upatapo kiu, unaweza kwenda kunywa maji kwenye mtungi ambao wanaume wamejaza.” 10Ndipo akapiga magoti mbele ya Boazi, na kugusisha kichwa chake chini. Akamwambia, “Kwa nini nimepata kibali machoni pako, hata unijali mimi mgeni?” 11Boazi akajibu na kumwabia, “Nimekwisha ambiwa, yote uliyo yafanya tangu mme wako afariki. Umewaacha baba yako, mama, na nchi uliyozaliwa kumfuata mama mkwe wako na kuja kwa watu usiowajua. 4:13Hivyo Boazi alimchukua Ruth, na akawa mke wake. Boazi alilala naye, na Yahweh alimruhusu kupata mimba, na alizaa mtoto wa kiume. 14Wanamke huyu akamwambia Naomi, “Yahweh abarikiwe, ambaye hajakuacha bila ndugu wa karibu, yaani mtoto huyu. Jina lake na liwe maarufu katika Israeli. 15Na awe kwako mrutubishaji wa maisha na mwenye ruzuku uzeeni mwako, kwa kuwa mtoto wako mkwe, ambaye anakupenda, ambaye ni bora kwako kuliko watoto wa kiume saba, amemzaa. 16Kisha naomi akamchukua mtoto, akamlaza kifuani pake, na kumhudumia. 17Na majirani wa yule mwanamke, wakampa jina, wakisema, “Mtoto amezaliwa kwa Naomi.” Wakawita Obedi. Ambaye alikuja kuwa baba yake na Jese, ambaye alikuja kuwa baba yake na Daudi.

Wimbo wa katikati

Zab 128:1–5

1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. Amebarikiwa kila mtu amchaye Yahwe, atembeaye katika njia zake. 2Kazi ya mikono yako, wewe utaifurahia; utabarikiwa na kufanikiwa. 3Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao katika nyumba yako; wanao watakuwa kama miche ya mimea ya mizeituni wakaapo kuzunguka meza yako. 4Ndiyo, hakika, mtu anaye muheshimu Yahwe atabarikiwa. 5Mungu na akubariki toka Sayuni; na uweze kuona mafanikio ya Yerusalemu siku zote za maisha yako.

Injili

Mt 23:1–12

1Baadaye aliongea na umati wa watu na wanafunzi wake. Akasema, 2“Waandishi na Mafarisayo wanakalia kiti cha Musa. 3Kwa hiyo chochote wanacho waamuru kufanya, fanyeni huku mkiwachunguza. Lakini msije mkaiga matendo yao, kwa sababu wao hutamka mambo wasiyoyafanya. 4Kweli, wao hufunga mizigo mizito ambayo ni vigumu kuibeba, na kisha huwabebesha watu mabegani mwao. Lakini wao wenyewe hawasogezi hata kidole kuibeba. 5Matendo yao yote, huyafanya ili watazamwe na watu. Kwa sababu wao hupanua masanduku yao na huongeza ukubwa wa mapindo ya mavazi yao. 6Wao hupendelea kukaa maeneo ya kifahari katika sherehe na katika viti vya heshima ndani ya masinagogi, 7na kusalimiwa kwa heshima maeneo ya sokoni, na kuitwa “Walimu” na watu. 8Lakini ninyi hampaswi kuitwa “Walimu,” Kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja, na ninyi wote ni ndugu. 9Msimuite mtu yeyote hapa duniani kuwa baba yenu, kwa kuwa mnaye Baba mmoja tu, naye yuko mbinguni. 10Wala msije kuitwa 'walimu,' kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja tu, yaani Kristo. 11Bali aliye mkubwa miongoni mwenu atakuwa mtumishi wenu. 12Yeyote ajiinuae atashushwa. Na yeyote anaye jishusha atainuliwa.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 21 Agosti

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki