Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 20 Agosti
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 20 Agosti 2027
Ijumaa · Juma la 20 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Ijumaa ya Juma la 20 la Mwaka
Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Mt. Bernardo wa Clairvaux, abati na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu
Kufunga na toba
Siku ya toba
Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Ilitokea katika siku za utawala wa majaji kuwa kulikuwa na njaa katika nchi, na mtu mmoja wa Bethelehemu ya Yuda alikwenda katika nchi ya Moabu pamoja na mke wake na watoto wake walili wa kiume. 3Ndipo Elimeleki, mume wa Naomi, alikufa, na Naomi aliachwa na watoto wake wa kiume wawili. 4Watoto hawa walioa wanawake wa Moabu; jina la mmoja lilikuwa Oripa, na jina la mwingine lilikuwa Ruth. waliishi huko kwa takribani miaka kumi. 5Kisha wote Mahiloni na Kileoni walikufa, na kumuacha Naomi bila mme wake na bila watoto wake wawili. 6Ndipo Naomi aliamua kuondoka Moabu pamoja na wake wa watoto wake na kurudi Yuda kwa sababu alikuwa amesikia katika mkoa wa Moabu kuwa Yahweh amewasaidia watu wake katika uhitaji na amewapa chakula. 14Ndipo wake wa watoto wake wakapaza sauti zao na kulia tena. Oripa alimuaga kwa kumbusu, lakini Ruth aliendelea kubaki naye. 15Naomi alisema, “sikiliza, mwenzako amerudi kwa watu wake na miungu yake. Ruri pamoja naye.” 16lakini Ruth alisema, “Usiniache niondoke mbali nawe, kwa kuwa uendako, nitakwenda, utakapoishi, nitaishi; watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu. 22Kwa hivyo Naomi na Ruth Mmoabu, mke wa mtoto wake, walirudi kutoka nchi ya Moabu. walirudi Bethrehemu mwazo wa mavuno ya shairi.
Wimbo wa katikati
5Amebarikiwa yule ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, ambaye tumaini lake liko katika Yahwe Mungu wake. 6Yahwe aliumba mbingu na nchi, bahari, na vyote vilivyomo; huitazama kweli milele. 7Yeye hutekeleza hukumu kwa ajili ya walioonewa na huwapa chakula wenye njaa. Yahwe huwafungua waliofungwa; 8Yahwe huyafungua macho ya kipofu; Yahwe huwainua walioinama; Yahwe huwapenda watu wenye haki. 9Yahwe huwalinda wageni katika nchi; huwainua yatima na wajane, bali huipinga njia ya wasio haki. 10Yahwe atatawala milele, Mungu wako, Sayuni, kwa vizazi vyote. Msifuni Yahwe.
Injili
34Lakini Mafarisayo waliposikia kuwa Yesu amewanyamazisha Masadukayo, walijikusanya wao wenyewe kwa pamoja. 35Mmoja wao, akiwa mwana sheria, alimwuliza swali kwa kumjaribu. 36“Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote katika sheria?” 37Yesu akamjibu, “Lazima umpende Bwana kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 38Hii ndiyo amri iliyo kuu na ya kwanza. 39Na ya pili inafanana na hiyo- Ni lazima kumpenda jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe. 40Sheria zote na Manabii hutegemea amri hizi mbili.”
Watakatifu wa siku
- Mt. Bernardo wa Clairvaux, abati na mwalimu wa Kanisa
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki