Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 22 Agosti

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 22 Agosti 2027

Jumapili · Juma la 21 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Dominika ya 21 ya Mwaka

Dominika · Rangi ya liturujia: kijani

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Yos 24:1–2, 15–18

1Kisha Yoshua aliyakusanya pamoja makabila yote ya Israeli huko Shekemu na aliwaita wazee wa Israeli, viongozi, waamuzi na maafisa wao, nao wakajihudhurisha mbele za Mungu. 2Yoshua akawaambia watu wote, “Hiki ndicho Yahweh, Mungu wa Israeli anachokisema, 'Mababu zenu kwa miaka mingi iliyopita waliishi ng'ambo ya mto Frati - Tera, baba wa Ibrahimu na baba wa Nahori - nao waliabudu miungu mingine. 15Na kama inaonekana kuwa ni vibaya machoni penu kumwabudu Yahweh, chagueni ninyi katika siku hii ya leo ni nani mtakayemtumikia, kama ni miungu ambayo baba zenu waliiabudu ng'ambo ya Frati, au miungu ya Waamori, ambao ninyi mnakaa ndani ya nchi yao. Lakini kwangu mimi na nyumba yangu, tutumwabudu Yahweh.” 16Watu walijibu na kusema, “Hatutaweza kumwacha Yahweh na kuitumikia miungu mingine, 17kwa kuwa ni Yahweh Mungu wetu ambaye alitutoa sisi na baba zetu kutoka katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa, na ambaye alifanya hizo ishara kubwa mbele yetu, na ambaye alituhifadhi sisi katika njia zote ambazo sisi tuliziendea, na miongoni mwa mataifa yote ambayo tulipita kati kati yake, 18Na Yahweh aliwaondoa mbele yetu watu wote, na Waamori walioishi katika nchi hii. Hivyo, tutamwabudu Yahweh pia, kwa kuwa ni Mungu wetu”

Wimbo wa katikati

Zab 34:1–2, 15–22

1Zaburi ya Daudi; wakati alipojifanya kuwa mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimtoa yeye nje. Nitamsifu Yahwe wakati wote, siku zote sifa zake zitakuwa mdomoni mwangu. 2Nitamsifu Yahwe! walio onewa wasikie na kufurahi. 15Macho ya Yahwe yako kwenye haki na masikio yake huelekea kulia kwao. 16Uso wa Yahwe uko kinyume na wale watendao uovu, kuikatilia mbali kumbukumbu yao duniani. 17Wenye haki hulia na Yahwe husikia na kuwaokoa kwenye matatizo yao yote. 18Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni. 19Mateso ya wenye haki ni mengi, bali Yahwe huwaokoa nayo yote. 20Yeye huitunza mifupa yake yote, hakuna hata mmoja wao utavunjika. 21Uovu utawauwa waovu. Wale wachukiao haki watahukumiwa. 22Yahwe huokoa maisha ya watumishi wake. Hakuna atakaye hukumiwa hata mmoja atafutaye usalama katika yeye.

Somo la pili

Efe 5:21–32

21Jitoeni wenyewe kila mmoja kwa mwingine kwa heshima ya Kristo. 22Wake, jitoeni kwa waume zenu, kama kwa Bwana. 23Kwa sababu mume ni kichwa cha mke, kama Kristo alivyo kichwa cha kanisa. Ni mwokozi wa mwili. 24Lakini kama kanisa lilivyo chini ya Kristo, vilevile wake lazima wafanye hivyo kwa waume zao katika kila jambo. 25Waume, wapendeni wake zenu kama vile Kristo alivyolipenda kanisa na akajitoa mwenyewe kwa ajili yake. 26Alifanya hivyo ili liwe takatifu. Alilitakasa kwa kuliosha na maji katika neno. 27Alifanya hivi ili kwamba aweze kujiwasilishia mwenyewe kanisa tukufu, pasipo na doa wala waa au kitu kifananacho na haya, badala yake ni takatifu lisilo na kosa. 28Kwa njia ile ile, waume wanatakiwa kuwapenda wake zao kama miili yao. Yule ampendae mke wake anajipenda mwenyewe. 29Hakuna hata mmoja anayechukia mwili wake. Badala yake, huurutubisha na kuupenda, kama Kristo pia alivyolipenda kanisa. 30Kwa kuwa sisi ni washiriki wa mwili wake. 31“Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja”. 32huu ulikuwa umefichika. Lakini ninasema kuhusu Kristo na kanisa.

Injili

Yn 6:60–69

60Ndipo wengi wa wanafunzi wake waliposikia haya, wakasema, “Hili nifundisho gumu ni nani awezaye kulipokea?” 61Yesu kwa sababu alijua ya kuwa wanafunzi wake walikuwa wakilinung'unikia jambo hili, akawambia je jambo hili linawakwaza? 62Basi itakuaje mtakapomwona mwana wa Adamu akishuka kutoka alikokuwa kabla? 63Ni Roho ndiye atoaye uzima. Mwili haufaidii kitu chochote. Maneno niliyoyasema kwenu ni roho na ni uzima. 64Bado kuna watu kati yenu wasioamini.” kwa sababu Yesu alijua tangu mwanzo yule ambaye asiyeweza kuamini na yeye ambaye angemsaliti. 65Akawambia, ni kwa sababu hii niliwambia kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amepewa na Baba.” 66Baada ya haya wanafunzi wake wengi walirudi nyuma na hawakuambatana naye tena. 67Yesu akawambia wale kumi na wawili, “Je na ninyi mnataka kuondoka?” 68Simoni Petro akamjibu, “Bwana twende kwa nani kwani wewe unayo maneno ya uzima wa milele, 69na tumeamini na kujua kuwa wewe ni Mtakatifu wa Mungu.”

Watakatifu wa 22 Agosti

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki