Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 20 Juni

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 20 Juni 2027

Jumapili · Juma la 12 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Dominika ya 12 ya Mwaka

Dominika · Rangi ya liturujia: kijani

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Ayu 38:1, 8–11

1Ndipo Yahweh alimwita Ayubu kutoka katika dhoruba kali na kumwambia, 8Ni nani huifunga bahari kwa milango wakati inapofurika, kana kwamba inatoka katika tumbo, 9wakati nilipoyafanya mawingu kuwa ni mavazi yake, na giza nene kuwa mkanda wake wa kujifungia? 10Hapo ilikuwa wakati nilipoweka bahari mpaka wangu, na nilipoweka makomeo yake na milango, 11na wakati nilipoiambia, 'Unaweza kuja hapa kutoka mbali, lakini si zaidi; na hapa ndipo nitauweka mpaka kwa fahari ya mawimbi yako.'

Wimbo wa katikati

Zab 107:23–26, 28–31

23Baadhi husafiri baharini katika meli na kufanya biashara juu ya bahari. 24Hawa huona matendo ya Yahwe na maajabu yake baharini. 25Kwa maana aliamuru na alivumisha upepo wa dhoruba ambao uliyainua juu mawimbi ya baharini. 26Walipanda juu mawinguni na kushuka vilindini. Nafsi zao ziliyeyuka katika dhiki. 28Kisha walimlilia Yahwe katika shida yao, naye akawatoa katika dhiki yao. 29Aliituliza dhoruba, na mawimbi yakatulia. 30Ndipo walifurahia kwa sababu bahari ilikuwa shwali, na aliwaleta kwenye bandari waliyoitamani. 31Oh, ili watu wamsifu Yahwe kwa ajili ya uaminifu wa agano lake na kwa mambo ya ajabu aliyowatendea wanadamu!

Somo la pili

2 Kor 5:14–17

14Kwa kuwa upendo wa Kristo watushurutisha, kwa sababu tuna uhakika na hili: kuwa mtu mmoja alikufa kwa ajili ya wote, na kwa hiyo wote wamekufa. 15Na Kristo alikufa kwa ajili ya wote, ili kwamba wale wanaoishi wasiishi tena kwa ajili yao wenyewe. Badala yake, lazima waishi kwa ajili yake yeye ambaye alikufa na alifufuliwa. 16Kwa sababu hii, kuanzia sasa na kuendelea hatumuhukumu mtu kulingana na viwango vya wanadamu, ingawa hapo kwanza tulimtazama Kristo katika namna hii. Lakini sasa hatumuhukumu yeyote kwa namna hii tena. 17Kwa hiyo, ikiwa mtu yeyote yuko ndani ya Kristo, yeye ni kiumbe kipya. Mambo ya kale yamepita. Tazama, yamekuwa mapya.

Injili

Mk 4:35–41

35Katika siku hiyo, wakati wa jioni ulipowadia, akasema kwao, “Twendeni upande wa pili”. 36Hivyo wakauacha umati, wakamchukua Yesu, wakati huo tayari alikuwa ndani ya mtumbwi. Mitumbwi mingine ilikuwa pamoja naye. 37Na upepo mkali wa dhoruba na mawimbi yalikuwa yakiingia ndani ya mtumbwi na mtumbwi tayali ulikuwa umejaa. 38Lakini Yesu mwenyewe alikuwa kwenye shetri, amelala kwenye mto. Wakamwamsha, wakisema, “Mwalimu, haujali sisi tunakufa?” 39Na akaamka, akaukemea upepo na akaiambia bahari, “'Iwe shwari, amani”. Upepo ukakoma, na kulikuwa na utulivu mkubwa. 40Na akasema kwao, “Kwa nini mnaogopa? Je hamna imani bado?” 41Walijawa na hofu kubwa ndani yao na wakasemezana wao kwa wao, “ Huyu ni nani tena, kwa sababu hata upepo na bahari vya mtii?”.

Watakatifu wa 20 Juni

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki