Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 30 Aprili
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 30 Aprili 2027
Ijumaa · Juma la 5 la Pasaka
Sikukuu na watakatifu
Ijumaa ya Juma la 5 la Pasaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: nyeupe
Mt. Pio V, papa · Kumbukumbu ya hiari
Kufunga na toba
Siku ya toba
Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.
Masomo ya siku
Somo la kwanza
22Kwa hiyo ikaonekana kuwa imewapendeza mitume na wazee, pamoja na kanisa lote, kumchagua Yuda aliyeitwa Barsaba, na Silas, waliokuwa viongozi wa kanisa, na kuwatuma Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba. 23Waliandika hivi, “Mitume, wazee na ndugu, kwa ndugu wa Mataifa walioko Antiokia, Shamu na Kilikia, salamu. 24Tulisika kwamba watu fulani ambao hatukuwapatia amri hiyo, walitoka kwetu na wamewataabisha kwa mafundisho yaletayo shida nafsini mwenu. 25Kwa hiyo imeonekana vyema kwetu sote kuchagua watu na kuwatuma kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paulo, 26watu walio hatarisha maisha yao kwa ajili ya jina la Bwana Yesu Kristo. 27Kwa hiyo tumemtuma Yuda na Sila, watawaambia mambo yayo hayo. 28Kwa kuwa ilionekana vyema kwa Roho Mtakatifu na kwetu, kutoweka juu yenu mzigo mkubwa kuliko mambo haya yaliyo ya lazima: 29kwamba mgeuke kutoka kwenye vitu vitolewavyo kwa sanamu, damu, vitu vya kunyongwa, na uasherati. Kama mtajiweka mbali na hivi, itakuwa vyema kwenu. Kwa herini.” 30Hivyo basi, walivyotawanyishwa, waliteremkia Antiokia; baada ya kukusanya kusanyiko pamoja, waliwasilisha barua. 31Walipokua wameisoma, walifurahi kwa sababu ya kutiwa moyo.
Wimbo wa katikati
7Moyo wangu umeponywa, Mungu, moyo wangu umeponywa, nitaimba, ndiyo, nitaimba sifa. 8Inuka, moyo wa thamani; inuka, kinanda na kinubi; nitaamka alfajiri. 9Nitakushukuru wewe, Bwana, kati ya watu; Kati ya mataifa nitakuimbia sifa. 10Maana upendo wako usiokwisha, huzifikia mbingu; na uaminifu wako mawinguni. 11Uinuliwe, Mungu, juu ya mbingu; na utukufu wako uinuliwe juu ya nchi yote.
Injili
12Hii ndiyo amri yangu, kwamba mpendane ninyi kwa ninyi kama nilivyo wapenda ninyi. 13Hakuna mtu aliye na upendo mkuu kuliko huu, kwamba ayatoe maisha yake kwa ajiliya rafiki zake. 14Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafanya yale niwaagizayo. 15Siwaiti watumwa, kwa kuwa mtumwa hajui kile afanyacho bwana wake. Nimewaita ninyi marafiki, kwa sababu nimewajulisheni mambo yote ambayo nimesikia kutoka kwa Baba. 16Hamkunichagua mimi, bali mimi niliwachagua ninyi na kuwaweka mwende mazae matunda, na tunda lenu lipate kukaa. Hii liko hivi ili kwamba chochote muombacho kwa Baba kwa jina langu, atawapeni. 17Mambo haya ninawaagiza, kwamba mpendane kila mtu na mwenzake.
Watakatifu wa siku
- Mt. Pio V, papa
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki