Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 29 Aprili
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 29 Aprili 2027
Alhamisi · Juma la 5 la Pasaka
Sikukuu na watakatifu
Alhamisi ya Juma la 5 la Pasaka
Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Mt. Katarina wa Siena, bikira na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu
Masomo ya siku
Somo la kwanza
7Baada ya majadiliano marefu, Petro alisimama na kusema kwao, “Ndugu mwatambua kwamba kitambo kizuri kilichopita Mungu alifanya chaguo kati yenu, kwamba kwa mdomo wangu Mataifa wasikie neno la injili, na kuamini. 8Mungu, anayefahamu mioyo, anashuhudia kwao, anawapa Roho mtakatifu, kama alivyofanya kwetu; 9na hakutengeneza utofauti kati yetu na wao, akiifanya mioyo yao safi kwa imani. 10Kwa hiyo, kwa nini mnamjaribu Mungu kwamba muweke nira juu ya shingo za wanafunzi ambayo hata baba zetu wala sisi hatukuweza kustahimili? 11Lakini twaamini kwamba tutaokolewa kwa neema ya Bwana Yesu, kama walivyokuwa.” 12Kusanyiko lote lilinyamaza walipokua wakimsikiliza Barnaba na Paulo walipokuwa wakitoa taarifa ya ishara na maajabu ambayo Mungu alifanya pamoja nao kati ya watu wa mataifa. 13Walipoacha kuongea, Yakobo alijibu akisema, “Ndugu nisikilizeni. 14Simoni ameelezea jinsi kwanza Mungu kwa neema aliwasaidia Mataifa ili kwamba ajipatie kutoka kwao watu kwa ajili ya jina lake. 15Maneno ya manabii yanakubaliana na hili kama lilivyoandikwa. 16'Baada ya mambo haya nitarudi na kuijenga tena hema ya Daudi, iliyoanguka chini; nitainua na kuhuisha uhararibifu wake, 17ili kwamba watu waliobaki wamtafute Bwana, pamoja na watu wa Mataifa walioitwa kwa jina langu.' 18Hivi ndivyo asemavyo Bwana aliyefanya mambo haya yajulikanayo tangu enzi za zamani. 19Hivyo basi, ushauri wangu ni, kwamba tusiwapatie shida watu wa Mataifa wamgeukiao Mungu; 20lakini tuandike kwao kwamba wajiepushe mbali na uharibifu wa sanamu, tamaa za uasherati, na vilivyonyongwa, na damu. 21Kutoka vizazi vya wazee kuna watu katika kila mji wahubirio na kumsoma Musa katika masinagogi kila Sabato.”
Wimbo wa katikati
1Oh, mwimbieni Yahwe wimbo mpya; mwimbieni Yahwe, nchi yote. 2Mwimbieni Yahwe, tukuzeni jina lake; tangazeni wokovu wake siku hadi siku. 3Tangazeni utukufu wake kati ya mataifa, matendo yake ya ajabu kati ya mataifa. 10Semeni kati ya mataifa, Yahwe anatawala.” Ulimwengu pia umeimarishwa; hauwezi kutikiswa. Yeye huwahukumu watu kwa haki.
Injili
9Kama baba yangu alivyonipenda mimi, mimi pia nimewapenda ninyi; dumuni katika pendo langu. 10Ikiwa mtashika amri zangu, mtadumu katika pendo langu kama nilivyo shika amri za baba yangu na kudumu katika pendo lake. 11Nimesema mambo haya kwenu ili kwamba furaha yangu iwe ndani yenu na ili kwamba furaha yenu ifanyike kuwa timilifu.
Watakatifu wa siku
- Mt. Katarina wa Siena, bikira na mwalimu wa Kanisa
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki